ninakuhabarisha kutoka ludewa njombe tanzania
JITIHADA
za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutumia mzozo kati ya Mbunge wa Kigoma
Kaskazini, Zitto Kabwe, na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
zinaelekea kugonga mwamba.
Tanzania
Daima Jumapili limedokezwa kuwa CCM imewekeza vya kutosha katika hujuma
dhidi ya CHADEMA ikitumia baadhi ya wanachama wa zamani wa chama hicho
kuunda mgogoro na kukipasua.
Hata
hivyo, licha ya misukosuko na kelele kutoka kwa baadhi ya wanachama na
wanaodhaniwa kuwa ‘mapandikizi’, CHADEMA kimeweza kupuuza hujuma hizo na
kujikita katika harakati za ujenzi wa ngazi za chini za chama katika
vijiji na vitongoji.
Kwa
sasa viongozi kadhaa wa CHADEMA wamesambaa katika majimbo 103 nchi
nzima kujenga chama kwa kufuata maagizo ya Baraza Kuu lililoketi
mwishoni mwa mwaka jana, kama mwendelezo wa vuguvugu la mabadiliko, na
ujenzi wa chama kuelekea uchaguzi unaokuja.
Baadhi
ya wanachama walioondolewa kwa tuhuma mbalimbali wamekuwa
wanashirikiana na wana CCM waziwazi kusambaza maneno machafu dhidi ya
CHADEMA mtandaoni na mitaani. Baadhi yao wameshiriki kutengeneza mabango
na kuyapeperusha katika mikutano inayohutubiwa na Katibu Mkuu wa chama
hicho, Dk. Willibrod Slaa, katika mikoa ya Shinyanga na Kigoma.
Wanapinga
uamuzi wa Kamati Kuu kuwavua nyadhifa Zitto, Dk. Kitila Mkumbo na
Samson Mwigamba. Zitto amevuliwa wadhifa wa Naibu Katibu Mkuu, Dk.
Kitila amevuliwa wadhifa wa Mjumbe wa Kamati Kuu, na Mwigamba amevuliwa
wadhifa wa Mwenyekiti wa Mkoa wa Arusha kwa tuhuma za ‘usaliti’.
Katika
kumtetea Zitto na wenzake, baadhi ya wanachama wamekuwa wakitoa
matamko, huku wawili wakitangaza kujiuzulu nafasi zao katika mikoa ya
Lindi na Singida.
Huku
wakitoa shinikizo kwa chama Zitto asichukuliwe hatua zaidi, baadhi yao
mkoani Kigoma walikwenda mbali wakitaka chama kiahirishe ziara ya Dk.
Slaa mkoani humo hadi baadaye, kwa kisingizio cha usalama.
Hata
hivyo, Dk. Slaa alisisitiza kuwa masuala ya usalama yamezingatiwa
barabara, na kwamba ziara ziko pale pale, kwani hakuna mkoa au wilaya ya
mtu.
Tanzania
Daima limedokezwa kuwa uongozi wa CCM mkoani Kigoma, chini ya Dk. Aman
Walid Kabourou, umekuwa ukiratibu vitisho na fujo katika mikutano au
maeneo anayotembelea Dk. Slaa kwa lengo la kutisha wananchi.
Dk.
Kabourou aliwahi kuwa Mbunge wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya CHADEMA
kabla ya kukimbilia CCM miaka kadhaa iliyopita. Alipohamia CCM akapewa
ubunge wa Afrika Mashariki. Sasa ndiye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kigoma.
Makundi
ya vijana wa CCM na wana CHADEMA wenye matatizo na chama, wamekuwa
wakisambazwa kuelekea maeneo kadhaa kwa lengo la kuhujumu mikutano ya
Dk. Slaa.
Lengo ni kutumia fursa hii kujaribu kudhoofisha uwezo wa chama kinachohatarisha utawala wa CCM.
Miongoni
mwa mikakati ya kuivuruga CHADEMA inayofadhiliwa kwa gharama kubwa ni
kuwapandikiza vijana kufanya fujo katika mikutano ya Dk. Slaa.
Katika
mikutano hiyo vijana mbalimbali wamekuwa wakijitokeza na mabango ya
kupinga uamuzi wa kuondolewa kwa Zitto, kuzomea na kufanya vituko vyenye
lengo la kuharibu mikutano hiyo.
Miongoni
mwa matukio hayo ni lile lililotokea juzi katika Kijiji cha Mabamba
wilayani Kibondo, ambako zaidi ya vijana saba walikamatwa na kufikishwa
kwenye kituo cha polisi.
Hata
hivyo, baadhi ya watu waliokuwapo eneo la tukio waliwatambua kuwa wengi
wao ni vijana wa CCM ambao wamekuwa wakizunguka katika mikutano yote
anayofanya Dk. Slaa.
Katika
mikutano yake mkoani Shinyanga na Kigoma, Dk Slaa, alisema propaganda
za udini, ukabila na ugaidi zinazopandikizwa na CCM zimezidi kuimarisha
chama chake katika safari ya kuelekea Ikulu mwaka 2015.
Dk.
Slaa alisema wanaosema CHADEMA itakufa hawajui kinachoendelea, kwa
sababu ya uamuzi wa kuwachukulia hatua au kuwaondolea nyadhifa watu
wasiotaka kufuata maadili, katiba na miongozo ni njia ya kukipa uhai
chama hicho.
“Mimi
nilidhani CCM wangeshangilia chama chetu kufa, lakini hiki ninachokiona
kinanistaajabisha; yaani eti wanatuonea huruma sisi tusife? Huu ni
muujiza,” alisema.
Tanzania
Daima Jumapili, limekuwa likidokezwa kuwa viongozi wa CCM wamekuwa
wakifadhili harakati za kuidhoofisha CHADEMA ili wasipate upinzani mkali
katika uchaguzi ujao.
Wiki iliyopita kupitia ukurasa wake wa facebook, Naibu Katibu Mkuu wa CCM (bara), Mwigulu Nchemba aliandika kuwaMkurugenzi
wa Oganaizesheni na Mafunzo wa CHADEMA, Benson Kigaila aliyekuwa Kigoma
alipigwa na wafuasi wa Zitto hadi kushindwa kusimama hadi aliposaidiwa
na polisi.
Wakati
Mwigulu akituma maneno hayo kupitia ukurasa wake, Kigaila amesema kuwa
yeye yupo katika ziara ya kujenga chama mkoani Mbeya, na aliondoka
Tukuyu kwenda Njombe kwa kazi hiyo hiyo.
Wakati
wana CCM wakishangilia kile kinachoitwa mpasuko ndani ya CHADEMA, Dk.
Slaa anasema wanazidi kuimarika na watafanya vizuri zaidi katika chaguzi
zijazo.
Katika
mazungumzo yake na Tanzania Daima, wiki iliyopita, Dk. Slaa aliwataka
Watanzania wawe makini, kwani hao wanaotoa matamko ya kulaani Kamati Kuu
wanafanya kazi ya CCM, hata kama baadhi yao wana kadi za CHADEMA.
“Wanaojitokeza
kutoa matamko kulaani Kamati Kuu ya CHADEMA hawazungumzi bei ya umeme
kupanda, hawazungumzi hali mbaya ya elimu na afya nchini, hawazungumzii
suala la mishahara ya wafanyakazi, wamejikita kumjadili Mbowe na Slaa.
“Niwahakikishie
wanachama na Watanzania wanaotaka mabadiliko kuwa tuna usalama
uliokomaa tunajua hujuma zote, ndio maana jana Naibu Katibu Mkuu wa CCM,
Mwigulu Nchemba, aliwatangazia Watanzania kuwa Mkurugenzi wetu wa
Oganaizesheni na Mafunzo Benson Kigaila amepigwa na wafuasi wa Zitto na
amesaidiwa na polisi wala hajiwezi hata kusimama.”
Dk.
Slaa alisema wakurugenzi na viongozi mbalimbali wa chama hicho wapo
kwenye majimbo 103 nchi nzima kwa ajili ya ujenzi wa chama ngazi ya
msingi, kutekeleza uamuzi wa Baraza Kuu. Alisisitiza kuwa ziara hizo
hazina uhusiano na propaganda zinazosambazwa sasa kuhusu hatua ya chama
hicho kumvua vyeo Zitto.
TANZANIA DAIMA
0 comments:
Post a Comment