TIMU ya taifa ya
Uholanzi imefanikiwa kumaliza mwaka bila kufungwa mechi hata moja baada
ya kutoka sare ya bila ya kufungana na Colombia katika mchezo wa
kirafiki wa kimataifa uliofanyika jijini Amsterdam. Uholanzi ilifanikiwa
kucheza pungufu na wachezaji 10 pekee kwa karibu saa moja baada ya
Jeremain Lens kutolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 35 huku pia
wakiwakosa Sien de Jong na Rafael van der Vaart walioumia kabla ya
mapumziko. Kukosekana kwa wachezaji hao huku mmoja akitolewa nje moja
kwa moja kuliwapunguza makali Uholanzi ambao walikuwa wakicheza nyumbani
na kuwafanya kutumia muda mwingi wa mchezo kujilinda. Uholanzi ambayo
ilitoka sare ya mabao 2-2 na Japan Jumamosi iliyopita, imeshinda mechi
saba na kutoa sare tano katika mechi 12 walizocheza mwaka 2013.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment