HALMASHAURI
ya Busokelo Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya imeanza kutekeleza kwa
vitendo miradi iliyozinduliwa na mbio za mwenge wa uhuru uliomaliza mbio
zake Oktoba 14, Mwaka huu nchi nzima.
Katika
mbio za mwenge katika Halmashauri ya Busokelo ilitolewa mizinga ya
nyuki 60 kwa vikundi 6 yenye thamani ya shilingi Milinoni 2.7 ambapo
kila kikundi kilipatiwa mizinga 10 tayari kwa ufugaji wa nyuki.
Kutokana
na vikundi hivyo kukabidhiwa mradi huo wa ufugaji nyuki Halmashauri
iliandaa mafunzo ya siku tatu kwa wenye viti na makatibu wa vikundi 8
pamoja na mafundi seremala kwa ajili ya kupatiwa mafunzo namna ya
ufugaji nyuki kwa njia ya kisasa inayochangia uhifadhi wa mazingira.
Msimamizi
wa mafunzo hayo, Anamary Joseph ambaye ni afisa mazingira wa
Halmashauri ya Busokelo alisema kupitia mafunzo hayo yatasaidia
kuhamasisha wananchi kuacha kufuga nyuki kienyeji jambo ambalo huchangia
kuharibu mazingira kutokana na njia wanayotumia wakati wa kuvuna.
Alisema
ufugaji wa nyuki kwa njia za kienyeji huharibu mazingira kwa sababu
wanapovuna hulazimika kuchoma moto ili nyuki waweze kukimbia na wao
kuvuna kirahisi lakini hali hiyo huchangia kuchoma moto misitu na pia
mazao yanayovunwa kuhosa ubora na kiwango ambacho kitamkomboa mkulima.
Awali
akimkaribisha Mkuu wa Wilaya katika ufunguzi wa mafunzo hayo
yaliyofanyika katika Kijiji cha Lufilyo Busokelo Wilayani Rungwe,
Mwenyekiti wa Halmashauri Meshack Mwakipunga alisema wameamua
kuwajumuisha mafundi seremala katika mafunzo hayo ili mizinga iwe
inatengenezwa jirani na wananchi na kwa gharama nafuu.
Alisema
mazingira ya busokelo yanaruhusu ufugaji wa nyuki hivyo wananchi
wakihamasishwa pia itasaidia kuongeza vipato vyao kupitia mazao ya
kilimo ambayo yatasaidiwa na nyuki kufanya uchavushaji wakati
wakijitafutia chakula.
Akizungumza
wakati akifunga mafunzo hayo Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Crispin Meela
alisema ni vema vikundi vilivyopewa mafunzo vikasimamiwa ili matunda
yaonekane na iwe fundisho kwa wengine ambao hgawataki kujiunga na
vikundi.
Alisema
uchumi wa mtanzania unatokana na juhudi za mtu binafsi kupitia vikundi
ambapo kupitia vikundi ni rahisi Serikali kuvisaidia kama ilivyofanya
kwa kuwapa mizinga ya nyiki ambapo mradi huo hauna gharama yoyote ambayo
kikundi kitapaswa kugharamia wakati wa kuendesha miradi hiyo.
Alisema
Nyuki hawana gharama yoyote ambapo wakishawekewa mizinga huingia
wenyewe na kuanza kutoa asali jambo ambalo mfugaji atatakiwa kuanza
kuvuna na kuuza asali ambayo itakuwa imevunwa kwa kufuata taratibu za
kitalaamu.
“
mnajua hawa nyuki hawana gharama zozote ambazo kikundi kitapaswa
kugharamia kwa sababu nyuki hawaugui kwamba watatakiwa kupatiwa chanjo,
hawali pumba, hawahitaji kuletewa maji bali huyafuata popote yalipo na
wala hawataki pembejeo kutoka serikalini hivyo changamkieni fursa hiii.”
Alisema Mkuu wa Wilaya.
Aliongeza
kuwa ili kudhibiti uharibifu wa mazingira na kujenga mazingira rafiki
kwa ufugaji wa nyuki ni vema wanaofuga nyuki kienyeji wakadhibitiwa kwa
kuwa ndiyo wanaochoma mazingira hivyo Halmashauri iwadhibiti kupitia
kanuni za vijiji na vitongoji kwa kuwaondoa kabisa misituni.
Mafunzo
hayo yatolewa na wataalamu wawili kutoka kampuni ya National Beekeeping
Supplies kutoka Mkoani Dodoma mafunzo ambayo yaliyofanyika kwa siku
tatu ambapo wamefundishwa namna ya uvunaji na ufungaji kwa kuzingatia
mahitaji ya soko la kimataifa.
0 comments:
Post a Comment