MSHAMBULIAJI nyota wa
kimataifa wa Brazil, Robinho amefanikiwa kuifungia Brazil bao la ushindi
akitokea benchi katika ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Chile na kumfanya
nyota huyo kufikisha mabao tisa aliyowafunga wapinzani wao hao wa
Amerika Kusini. Robinho ambaye sasa ameipita rekodi iliyoweka na Pele
kwa kufunga bao moja zaidi yake dhidi ya Chile, aliitwa tena katika
kikosi cha nchi hiyo mapema mwezi huu kwa ajili ya mechi mbili za
kirafiki baada ya kukaa nje kwa kipindi cha miaka miwili. Brazil
inatarajiwa kucheza mechi moja zaidi ya kirafiki dhidi ya Afrika Kusini
jijini Johannesburg Machi mwakani kabla ya kocha Luis Filipe Scolari
hajatangaza kikosi cha mwisho cha Kombe la Dunia. Fainali za Kombe la
Dunia mwakani zinaandaliwa na Brazil ikiwa ni mara ya kwanza toka mwaka
1950 walipofanya hivyo.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment