TIMU ya taifa ya
Ufaransa imefanikiwa kukata tiketi ya kushiriki michuano ya Kombe la
Dunia mwakani nchini Brazil baada ya kufanikiwa kugeuza matokeo na
kuiondosha Ukraine huku Cristiano Ronaldo naye akiihakikishia Ureno
kwenda huko kwa kupiga mabao matatu peke yake. Timu hizo vigogo wa soka
vya Ulaya zinaungana na Croatia, Ugiriki, Ghana na Algeria kuelekea
katika fainali hizo zinazochezwa majira ya kiangazi mwakani baada ya
kufanikiwa kushindwa mechi zao za mtoano za mkondo wa pili jana.
Ufaransa wao waligeuza matokeo ya kufungwa mabao 2-0 katika mechi ya
kwanza kwa kuibugiza Ukraine kwa mabao 3-0 yaliyofungwa na Mamadou
Sakho, Karim Benzema na linguine la kujifunga la Oleg Gusey na kuifanya
nchi hiyo kufuzu kwa jumla ya mabao 3-2. Kwa upande wa Ureno wao
walifanikiwa kuigaragaza Sweden kwa mabao 3-2 na kufuzu kwa jumla ya
mabao 4-2 katika mechi mbili za mtoano walizokutana
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment