MKUU wa wilya ya Ileje mkoania Mbeya, Bi.Rosemary Senyamule, amewaasa
wahitimu wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Wiza kutojihusisha
na makundi ya uvutaji bangi pamoja na ukahaba hali itakayowapotezea
malengo yao ya baadaye.
Senyamule alitoa wito huo mwishoni mwa wiki akiwa mgeni rasmi katika mahafali ya kidato cha nne ya shule hiyo inayo milikiwa na Unyiha Associates Vwawa wilayani Mbozi ambapo wanafunzi 51walitunukiwa vyeti.
Alisema wanafunzi wanatakiwa kuwa na malengo yao ya baadaye ili waweze kutimiza ndoto zao.
“Sisi kama wazazi wenu, walezi tunatakiwa kuwahimiza kabla hamjaharibikiwa, kwa kuwa ninyi ndio taifa la kesho, epukeni makundi yasiyowafaa ambayo yatawapelekea kutotimiza ndoto zetu,” alisema Senyamule
Katika hatua nyingine mkuu huyo wa wilaya aliwataka wanafunzi hao kuto kuwa waoga wanapo fanya kazi zao,wakitambua dhahili kuwa uoga ni umasikini.
Kwaupande wake Mkuu wa shule hiyo, Simon Kibona Lukas Hassan, alisema shule yake imejiwekea mikakati mbalimbali ili kusaidia kupanua wigo wa kiwango cha elimu nchini na kuwawezesha wanafunzi wao kufanya vizuri katika mitihani yao ya taifa.
“Ili tupate mafanikio ya elimu lazima tuweke mikakati ya kuboresha mazingira ya kujisomea na kujifunza ili kusiwe na muingilianao wowote ambapo tutajitahidi kuhakikisha tunadumisha kiwango bora cha ufaulu wa shule yetu tulichonacho,” alisema Kibona.

0 comments:
Post a Comment