Nane watiwa mbaroni kwa kuzuia msafara wa Waziri Nchimbi.

Jeshi la polisi mkoani Ruvuma linawashikilia watu wanane ambao ni waendesha piki piki maarufu kama madereva yebo yebo wa mjini Songea mkoani Ruvuma kwa tuhuma za kupanga njama na kufungu bara bara itokayo Songea mjini kuelekea Matarawe kwa muda wa zaidi ya masaa mawili kwa madai kuwa daraja dogo lililopo katika bara bara hiyo limekuwa chanzo cha ajali za mara mara.

Kitendo hicho cha kufungwa kwa bara bara hiyo kiliwafanya watumiaji wengi wa bara hiyo kukosa huduma zinazopatikana baina ya mitaa hiyo miwili ya mjini na Matarawe kwa muda wote mpaka msafara wa Mbunge wa jimbo la Songea mjini ambaye pia ni Waziri wa mambo ya ndani Emmanuel Nchimbi aliposimamishwa kwenye kivukohicho chenye daraja linalounganisha kata ya Mjini na Matarawe na baadhi ya wananchi wakiwemo waendesha piki piki kumueleza Mbunge wao sababu ilyowapelekea kuifunga bara bara hiyo.

Akizungumza mmoja wa waendesha piki piki hao mbele ya Mbunge Nchimbi alisema kuwa kivuko hicho chenye daraja jembamba kimekuwa chanzo cha ajali nyingi za magari,piki piki,baiskeli na waenda kwa miguu pia kwa sababu ya wembamba wa daraja na miinuko iliyopo pande zote mbili za kata hizo ambayo huvifanya vyombo vya usafiri kupita kwa kasi kubwa kwenye kivuko hicho chembamba.


Alisema kuwa katika kipindi kifupi cha siku tatu zaidi ya ajali tatu zimetokea kwenye kivuko hicho ambazo zilisababisha vifo vya watu wanne na kilio hicho cha ufinyu wa daraja hilo ni cha muda mrefu na baadhi ya viongozi wa halmashauri ya Manispaa ya Songea,wilaya na mkoa wamekuwa wakipita katika eneo hilo mara kwa mara na kushuhudia hali hiyo hatarishi bila kuchukua hatua yoyote.

Baada ya kusikiliza kilio hicho Mbunge wa jimbo la Songea mjini Emmanuel Nchimbi aliwajibu wananchi hao kuwa yeye ndiye aliyefanya jitihada za kutengeneza bara bara mbali mbali za Manispaa ya Songea kwa kiwango cha lami hivyo kutengenza kivuko hicho siyo tatizo la kuwafanya wao kufunga bara bara na kuzuia huduma mbali mbali kuendelea na kufanya hivyo ni kosa kwa sababu msfara wa mbunge ulikuwa ukielekea kwenye kata ya Matarawe kwa ajili ya kusikiliza kero za wananchi nao wangeweza kutumia fursa hiyo kueleza kero hiyo badala ya kufunga bara bara.

Lakini bada ya Mbunge kuzugumza na wananchi pamoja na waendesha piki piki waliokuwepo kwenye eneo hilo la livuko msafara uliendelea kuelekea shule ya Sekondari Matarawe kwa ajili ya mkutano ndipo kundi la waendesha piki piki lilipojitokeza na kuifunga tena bara bara hiyo kwa kuweka mawe,miti na kuchoma matairi ya magari mpaka jeshi lilipolazimka kutumia mabomu ya macho kuwatawanya nakuondoa vizuizi hivyo ili kuwezesha msafara wa mbunge baada ya kumaliza mkutano ambao ulipita huku ukiwa na ulinzi zaidi wa askari polisi.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsimeki aliiambia Radio One Stereo kwa njia ya simu kuwa watu wanane wanashikiliwa kuhusiana na tukio hilo na uchunguzi zaidi unafanyika na watakaothibitika watafikishwa mahakamani.

Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: