Wafungaji bora Uefa Champions 24 October 13
Pos. | Player | Goals | Team |
---|---|---|---|
1 | Cristiano Ronaldo | 7 | Real Madrid |
2 | Zlatan Ibrahimovic | 6 | Paris Saint-Germain |
3 | Marián Cišovský | 5 | Viktoria Plzen |
3 | Roman Shirokov | 5 | Zenit St. Petersburg |
5 | Aaron Ramsey | 4 | Arsenal |
5 | Sergey Khizhnichenko | 4 | Shakhtyor IK |
5 | Lionel Messi | 4 | FC Barcelona |
5 | Mohamed Salah | 4 | (FC) Basel |
9 | James Forrest | 3 | Celtic |
9 | Hilal Soudani El Arabi | 3 | Dinamo Zagreb |
Matokeo ya Uefa champions 23 October 13
Galatasaray 3-1 FC Kobenhavn
Manchester United 1-0 Real Sociedad de Fútbol
Real Madrid C.F. 2-1 Juventus
FC Bayern München 5-0 FC Viktoria Plzeň
Sl benfica 1-1 Olympiacos F.C.
Leverkusen 4-0 Shakhtar
Anderlecht 0-5 PSG
Manchester United 1-0 Real Sociedad de Fútbol
Real Madrid C.F. 2-1 Juventus
FC Bayern München 5-0 FC Viktoria Plzeň
Sl benfica 1-1 Olympiacos F.C.
Leverkusen 4-0 Shakhtar
Anderlecht 0-5 PSG
Bado nakumbali Robinho - Neymar
Robinho (kushoto) na Neymar (kulia) wakibadilishana jezi wakati wa mapumziko kwenye mechi kati ya Ac Milan na Barcelona. Neymar tokea udogo wake amekuwa akimpenda Robinho na alishamtembelea mara kadhaa nchini Brazil kumsalimia nyakati za udogo wake. Neymar mwenyewe aliwahi kusema ' nampenda Robinho na ningependa siku moja kuja kucheza na kuwa kama yeye'. Wiki hii baada ya mchezo kati ya Milan na Barca, Neymar alisema tena ' Bado nampenda Robinho kwasababu yeye ndiye mtu niliyekuwa nikimuangalia enzi za udogo wangu, nilitamani sana kuwa kama yeye, hivyo ataendelea kuwa mfano wa kufuata kwenye maisha yangu. Siku ya leo ni furaha kwangu kucheza mechi pamoja naye licha ya kuwa tupo timu tofauti'. |
Robinho na Neymar wakiagana baada ya mechi kuisha kwa droo ya goli 1 -1 |
Steve G ni bora kuliko wachezaji pendwa wa Sir Alex
Katika
mahojiano na waandishi wa habari kuhusu kitabu chake alichokizindua
wiki hii, kocha wa zamani wa Man utd Sir Alex Ferguson alisema wachezaji
wa Man utd, Ryan Giggs na Paul Scholes ni wachezaji wazuri kuliko
nahodha wa Liverpool Steven Gerrard. Baada ya kuongea hayo wachambuzi wa
soka walipitia rekodi zilipo za wachezaji hawa watatu wakagundua kuwa
Gerrard bado ni mchezaji bora zaidi yao. Ukiangalia takwimu zilizipo
hapo chini utaona kuwa Gerrard amecheza mechi chache kuliko Giggs na
Scholes lakini magoli aliyofunga na pasi alizotoa zinakaribiana na
wachezaji hawa wa Man utd, jambo ambalo linaonesha pindi Gerrard
akifikisha idadi ya mechi walizocheza Giggs na Scholes ni wazi kuwa
ataweza akuwafikia au kuwazidi kwenye magoli na pasi za magoli. Mbali ya
kumponda Steve G, kocha Alex Ferguson pia alishawahi kumhitaji mchezaji
huyu mara kadhaa ili asajiliwe na Man utd ila mchezaji mwenyewe
aligoma.
Kanzu ya Robinho dhidi ya Alexis wa Barcelona
Robinho
ameonesha kuwa yeye bado full kiwango baada ya kumpiga kanzu ya maana
Alexis wa Barcelona kwenye mechi ya Uefa champions. Angalia kanzu hiyo
hapo chini
Matokeo ya Uefa champions 22 October 13
FT: Shalke 04 0-3 Chelsea
FT: Arsenal 1-2 B. Dortmund
FT: AC Milan 1-1 Barcelona
FT: Marseille 1-2 Napoli
FT: Celtic 2-1 Ajax Amsterdam
FT: S.Bucarest 0-1 FC Basel
FT: FC Porto 0-1 Zenit
FT: Austria Vienna 0-3 Atletico Madrid
FT: Arsenal 1-2 B. Dortmund
FT: AC Milan 1-1 Barcelona
FT: Marseille 1-2 Napoli
FT: Celtic 2-1 Ajax Amsterdam
FT: S.Bucarest 0-1 FC Basel
FT: FC Porto 0-1 Zenit
FT: Austria Vienna 0-3 Atletico Madrid
Video: Kevin-Prince Boateng a.k.a Michael Jackson
Angalia video hii uone kipaji kingine cha Prince Boateng
Boateng akiwa na mpenzi wake mpya baada ya kuachana na mkewe
Ferguson atoa kitabu cha historia yake kwenye soka
Sir
Alex kocha wa zamani wa Man utd akionesha kitabu chake alichokizindua
leo. Ndani ya kitabu hiki kuna mambo mengi yahusuyo soka katika kipindi
chote alichokuwa kocha wa klabu ya Man utd. Pia ameongelea baadhi ya
wachezaji na wadau wa soka aliyowahi kukutana nao na kufanya nao kazi.
Baadhi ya wachezaji na wadau aliowaongelea ni kama ifuatavyo;
1. Cristiano Ronaldo: Amemtaja kama mchezaji mwenye kipaji kuliko wote aliyowahi kuwafundisha
2. Beckham: Ni mchezaji mwenye tabia mbaya alikuwa anajisikia mkubwa kuliko kocha
3. Rooney: Alimuomba Sir Alex kutaka kuhama Man utd mwishoni mwa msimu uliopita
4. Owen Hargreaves: Sir Alex amemtaja mchezaji huyu kuwa ni usajili mbovu aliyowahi kuufanya kuliko wote
5. FA: Sir Alex amesema chama cha soka cha England kilishawahi kumuomba aifundishe timu ya taifa mara mbili akagoma
6. Rafa Benitez: Amemtaja kuwa ni kocha mwenye tabia ya hovyo na asiyeeleweka
7. Roy Keane: Sir Alex amesema, hali ya maelewano ilikuwa njema ndani ya
klabu baada ya Keane kuondoka Man utd, kwani amemtaja mchezaji huyu
kuwa ni mkorofi na majibizano.
Haya ni baadhi tu ya mambo yaliyomo ndani ya kitabu, kwa bahari zaidi kuhusu kitabu hiki na yaliyomo unaweza kutembelea hapa bofya
|
Simba na Yanga zaingiza shilingi mil 500
Mechi
Ya Simba, Yanga Yaingiza Mil 500/- Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL)
ya watani wa jadi Simba na Yanga. Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) ya
watani wa jadi Simba na Yanga iliyochezwa jana (Oktoba 20 mwaka huu)
kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa sare ya mabao
3-3 imeingiza sh. 500,727,000. Washabiki 57,422 ndiyo waliokata tiketi
kushuhudia pambano hilo namba 63 kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 7,000,
sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 30,000. Ni tiketi 131 tu
ndizo hazikuuzwa ambazo ni 90 za VIP A, 40 za VIP B na moja ya VIP C.
Tiketi zilizochapwa kwa ajili ya mechi hiyo ni 57,558 ambayo ndiyo idadi
ya viti vilivyopo kwenye uwanja huo. Kila klabu imepata mgawo wa sh.
123,025,564.32 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni
sh. 76,382,084.75. Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya
uwanja sh. 62,555,371.69, tiketi sh. 7,309,104, gharama za mechi sh.
37,533,223.01, Kamati ya Ligi sh. 37,533,223.01, Mfuko wa Maendeleo ya
Mpira wa Miguu (FDF) sh. 18,766,611.51 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa
wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 14,596,253.39.
Baines amkimbiza Evra Manchester United
Beki tegemezi wa kushoto wa Man utd Patrice Evra ametangaza kuondoka Man utd mwishoni mwa msimu huu pindi mkataba wake utakapomalizika. Evra aliyasema hayo mbele ya waandishi wa habari akisema ' nafikiria kufikia kikomo kuichezea Man utd mwisho wa msimu huu. Nimeamua kuondoka kwasababu zangu binafsi na sio kama vile watu wanavyosema, lakini siwezi kuzisema ni sababu zipi. Man utd wananitaka niendelee kuwepo, lakini mimi nimeona basi'. Wachambuzi wa masuala ya soka pamoja na waandishi wa habari wanasema uamuzi huu wa Evra umesababishwa na kustaafu kwa Sir Alex pamoja na nia ya Man utd ya kutaka kumsajili beki wa kushoto wa Everton Leighton Baines, jambo ambalo limemfanya Evra ajihisi kuwa hana mchango kwasasa ndani ya klabu. |
Leighton Baines (kulia), mchezaji anayewindwa na Man utd, imesekana anaweza kusajiliwa kwenye dirisha dogo |
Sir Alex ndiye sababu kubwa inayomfanya Evra kuondoka, kwani Moyes ameonekana kutokumkubali Evra. |
Ronaldo au Ibrahimovic kwenda Brazil
Timu
za taifa za Portugal na Sweden zimechaguliwa kukutana kwenye play off
za kombe la dunia ambapo mshindi kati yao ndiye atakayekwenda Brazil.
Mechi hii imevuta hisia za washabiki wengi wa soka kutokana na umaarufu
wa Ronaldo na Ibrahimovic, wachezaji ambao kiukweli kila mtu angependa
kuwaona wakishiriki kwenye michuano hii nchini Brazil. Lakini kukutana
kwao kwenye play off ni wazi kwamba mmoja kati yao (Ronaldo au Ibra)
atakosa kwenye michuano hii. Mechi hii pamoja na nyingine zitachezwa
Novemba 15 na 19. Mechi zingine zitakuwa ni kati ya;
Ukraine v France
Greece v Romania
Iceland v Croatia
PORTUGAL
World ranking: 14
Best World Cup: 3rd place (1966)
2010 World Cup: Round of 16
Qualifying: Disappointing. Finished one point behind Russia having started as favourites.
Manager: Paulo Bento
Star man: Cristiano Ronaldo (Real Madrid)
SWEDEN
World ranking: 25
Best World Cup: 3rd place (1950, 1994)
2010 World Cup: Did not qualify
Qualifying: Finished eight points adrift of Germany. Always destined for the play-offs.
Manager: Erik Hamren
Star man: Zlatan Ibrahimovic (PSG)
0 comments:
Post a Comment