Tamko hilo ni pigo zito waandaaaji wa michuano hiyo ambao ni Baraza la Vyama vya Soka la Nchi za Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) lililo chini ya Rais Leodegar Tenga na Katibu Mkuu wake Nicholas Musonye.
Awali, Mwenyekiti wa Shirikisho la Soka Kenya(FKF), Sam Nyamweya alitangaza kuwa,michuano hiyo itaandaliwa kwa ushirikiano wa pamoja kati ya shirikisho lake na Serikali ya nchi hiyo.
Katibu wa Baraza la Michezo la Kenya,Hassani Wario alisema, Serikali yake haitashiriki katika kuandaa michuano hiyo kutokana na ufinyu wa bajeti yake kwa sasa.(P.T)
"Ni lazima tuwe wa kweli, hatuwezi kuungana na FKF na kudhamini mashindano hayo kwasababu hatuna bajeti kwaajili hiyo,"alisema Waria na kuongeza:
"Kuna vyama vingine ambavyo vinahitahi fedha kama ilivyo soka, kuogelea, wavu na hata Hockey, ni vigumu kujikita katika soka tu.
Hata hivyo, Musonye akizungumza na Mwananchi alisema:
"Tumeamua na ni lazima michuano hii ifanyike Kenya.
"Tunatafuta wadhamini wengine, lakini ninachoweza kukuhakikishia ni kwamba mashindano yatafanyika hapa na hayawezi kuhamishiwa sehemu nyingine.
Mara ya mwisho Kenya iliandaa michuano ya Chalenji mwaka 2009 ambapo Uganda ilifanikiwa kutwaa ubingwa.
0 comments:
Post a Comment