Vikundi vya dini Senegal vyapinga ujio wa Rihanna


Mwanamuziki Rihanna
Mwanamuziki wa nyota wa kimataifa Rihanna anategemewa kuhudhuria mkutano mkubwa nchini Senegal, lakini vikundi vya dini nchini humo vimekataa kumpokea, chombo ch habari cha Jeune Afrique kimeripoti.
"Tumeukataa ufreemason na mapenzi ya jinsia moja" , Shirika la vikundi 30 vya kidini wamesema, wakimshutumu mwanamuziki huyo kwa kutumia ishara za  kuwa mjumbe wa chimbuko la Illuminati , linaloaminika kuwa ni kundi maalum la watu ambao huthibitisha masuala na uongozi wa dunia na inasadikika kuwa hufanya shughuli zao kisiri kudhibiti kila kitu na kuunda utawala mpya wa Dunia.
Shutuma hizo zimekuja kufutia wasanii mbalimbali waliowahi kufanya nao kazi huko nyuma,kudhibitika kujihusisha na masuala hayo.
Rihanna anatarajiwa kutembelea nchi hiyo ya Afrika Magharibi akiwa kama balozi wa Shirika la Elimu 'Global Partnership Foundation.'
Shirika hilo linamaudhui ya kuchangisha fedha za kuwafundishia mamilioni ya watoto na vijana katika nchi zinazoendelea.
Chombo cha habari cha Jeune Afrique kimemnukuu Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchi hiyo akisema kuwa atawahakikishia usalama washirika wote wa mkutano huo.




Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: