Maumivu makali yafuta ziara ya muziki ya Lady Gaga


 
Mwanamuziki Lady Gaga akiwa jukwaani
Mwanamuziki Lady Gaga amevuta siku kumi zake za mwisho za ziara yake ya dunia ya kimuziki kwa nchi za Ulaya kutokana na "maumivu makali".
Katika taarifa yake aliyoituma kupitia mtandao wake wa Twitter, mwanamuziki nyota huyo amewaomba radhi mashabiki wake na kusema kuwa  "nimevurugwa", lakini nahitaji kujiweka sawa "mimi mwenyewe na afya yangu" kwanza.
Mshindi huyo wa tuzo za mwanamuziki nyota  za Grammy, anasumbuliwa na tatizo la  maumivu makali ‘fibromyalgia,’ hali ambayo ni ya muda mrefu inayomsababishia maumivu katika mwili.
Miongoni mwa maonesho yaliyofutwa ni pamoja na lile la London na Manchester.
Katika taarifa yake hiyo amesema, "ni uamuzi mgumu" nilioamua kuufanya  Ijumaa usiku" baada ya kupata msaada mkubwa kutoka kwa timu yake ya matibabu".
Imeelezwa kuwa waliokuwa na tiketi wanaweza kuanza kuomba kurejeshewa malipo yao kuanzia Februari 6, iliongeza taarifa hiyo.




Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: