Mzee Ibrahim Akilimali
Mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara Yanga SC huenda ikamfuta uanachama mzee Ibrahim Akilimani baada ya kuonekana kuwa kinyume na matakwa ya klabu hiyo ya kuingia kwenye mchakato wa mabadiliko ya uendeshaji.
Maazimio hayo yametolewa na uongozi wa matawi ya Yanga yaliyopo Jijini Dar es Salaam ambapo makamu mwenyekiti wa tawi la Uhuru Kariakoo, Kais Edwin amesema mzee Akilimali amekiuka katiba ya Yanga ambayo inaruhusu mabadiliko.
Katika hatua nyingine viongozi hao wa matawi wameitaka serikali kuheshim katiba ya Yanga ili kuepusha mikanganyiko inayoweza kujitokeza ndani ya klabu hiyo kuhusu mfumo wa uendeshaji wake.
Hali hiyo imetokea siku chache baada ya Klabu ya Yanga kutangaza kuingia kwenye mchakato wa mabadiliko ya uendeshaji kwa kufuata mfumo wa uwekezaji kwa kuuza hisa, huku serikali ikisisitiza kuwa uuzaji wa hisa kwa wawekezaji kwenye vilabu vya wanachama haupaswi kuzidi asilimia 49 ili kutoondoa umiliki wa vilabu kwa wanachama.
Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
0 comments:
Post a Comment