Simba yaanza mazoezi kuziwinda Ndanda FC, Green Warriors




 
Simba wakiwa mazoezini leo
Kikosi cha vinara wa ligi kuu Tanzania Bara Simba SC leo kimeanza mazoezi baada ya mapumziko mafupi ya siku mbili huku kikijumuisha pia wachezaji wake waliokuwa kwenye majukumu ya kitaifa.
Simba wanajiandaa na mchezo wa kombe la Shirikisho la Azam Sports dhidi ya Green Warriors, utakaopigwa kabla ya kuivaa Ndanda FC katika mchezo wa raundi ya 12 ya ligi kuu Tanzania Bara, utakapoigwa Desemba 30 mwaka huu katika dimba la Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
Jumla ya wachezaji sita wa Simba walikuwa sehemu ya kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ na leo wamejiunga na kikosi hicho rasmi. Wachezaji hao ni Aishi Manula, Erasto Nyoni, Mohammed Hussein, Shiza Kichuya, Jonas Mkude na Mzamiru Yassin.
Kikosi hicho kilipata mapumziko ya siku mbili baada ya mchezo wa kirafiki uliopigwa Ijumaa wiki iliyopita dhidi ya African Lyon kutoka ligi daraja la kwanza, Simba ikiibuka na ushindi wa mabao 4-0.



Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: