Azam FC kuivaa Polisi Dar, Chamazi


Wachezaji wa Azam FC wakiwa mazoezini
Katika kumalizia maandalizi yake katika kipindi hiki cha mapumziko ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), kikosi cha Azam FC, kinatarajia kukipiga dhidi ya Polisi Tanzania kwenye mchezo wa kirafiki utakaofanyika Uwanja wa Azam Complex kesho Jumanne saa 1.00 usiku.
Huo ni mchezo wa nne wa kirafiki kwa timu hiyo baada ya mapumziko hayo kupisha michuano ya Kombe la Chalenji iliyomalizika jana Jumapili nchini Kenya, Azam FC ilianza kwa kutoka sare na Friends Rangers (1-1) kabla ya kuzichapa Mvuvumwa (8-1) na Villa Squad (7-1).
Akizungumzia programu ya mchezo huo dhidi ya timu hiyo ya Polisi, kocha msaidizi wa Azam FC, Idd Cheche, amesema watautumia kama sehemu ya maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wa Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) dhidi ya Area C United, ligi kuu pamoja na kombe la mapinduzi.
Azam FC itafungua pazia la michuano ya kombe la shirikisho msimu huu kwa kukipiga dhidi ya timu hiyo kutoka mkoani Dodoma inayoshiriki Ligi Daraja la Pili Tanzania Bara (SDL), mchezo utakaofanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam Jumamosi hii saa 10.00 jioni




Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: