UTAPELI WAINGIA LUDEWA VIONGOZI WA DINI WAHUSISHWA, AFISA TARAFA YUMO


Baahi ya wahanga wa Tukio hilo la utapeli wakiwa wamekusanyika nje ya Kituo cha polisi Ludewa Mjini.
Baadhi ya Viongozi wakiwa katika Kituo cha Polisi Ludewa Wakijadiliana jambo hilo
Wakwanza Kushoto ni Monica Mchilo Diwani Wa Kata ya Ludewa Akishauri jambo
Wakwanza Kulia ni Bw, Charles Keiya Afisa Tawala katika OFISI YA Mkuu wa wilaya Ludewa Akiwasiliana na Na Viongozi wenzake.
Na Maiko Luoga Ludewa,
Watu 90 wakazi wa Vijiji mbalimbali vya Wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe na Mmoja kutoka Makambako Mwingine Kutoka Iringa Wamejikuta wanashikwa na Mshangao baada ya Kutuma pesa katika namba Za Simu zilizoaminika kuwa ni za Matapeli Ili waweze kupata Ajira.

Wengi kati ya Wahanga wa Tukio hilo La Kutapeliwa ni Vijana wa Kike na Kiume ambao walijikuta wanaingia katika Mtego huo baada ya Kusomewa Tangazo la Ajira Katika Kanisa Roman Catholic Ludewa Mjini na Uongozi wa Kanisa Hilo Tangazo likionesha Nafasi Mbalimbali za Kazi. 

Uongozi wa Kanisa Romani Catholic Ulipokea Tangazo hilo Siku ya Jumapili ya Tarehe 17 December 2017  Kutoka kwa Muhusika wa kanisa Hilo Bi, Sophia Mwinuka ambae nae Baada ya Kuhojiwa na Waandishi wa Habari pamoja na Polisi Kituo Cha Ludewa Mjini alisema kuwa Alikabidhiwa Tangazo hilo na Mtu Asiyemfahamu Siku ya Jumasosi ya December 16/2017  na Mtu huyo Alikuwa Mwanaume ambae hamkumbuki kwa jina wala Sura.

Shirika hilo la kitapeli lisilo la kiserikali limejulikana kwa Jina la THE FACULTY OF LIVING POWER Lenye anuani ya P.O.BOX 553 Dar es Saalam linatajwa kuwa Linahusika na Kutoa Elimu ya neno la Mungu na UKIMWI kwa Jamii.
Aidha Shirika hilo Lilikuwa likitangaza nafasi mbalimbali za kazi katika Idara za neno la mungu na ukimwi, Ushauri na saha, kupima (vct) Huduma kwa watoto yatima, Elimu ya ukimwi Pamoja na huduma kwa watu waishio na virusi vya ukimwi.

Kijana aliyejulikana kwa Jina la Benward Kayombo anashikiliwa na Jeshi la Polisi Ludewa Mjini Kwa uchunguzi zaidi Kwakuwa kijana Huyo licha ya kuwa mwombaji wa Kazi katika Shirika hilo la Kitapeli alipewa nafasi ya Kugawa Fomu za Maombi kwa waombaji wengine hatahivyo nae inadaiwa kuwa Ametapeliwa kiasi cha Pesa kwaajili ya Maombi.

Kijana Huyo anashikiliwa na Polisi baada ya Kuingiwa hofu kutokana na Bosi wake kuto patikana kwa simu ndipo Bw, Benward aliamua Kwenda kuripoti Kituo Cha polisi na Kujikuta kuwa anashikiliwa Kwa Uchunguzi zaidi pamoja na Usalama wa maisha yake kwa Waombaji wengine Waliofika katika Kituo Cha polisi Ludewa Mjini Wakidai Pesa zao kutoka kwa Benward aliyewagawia Fomu za Maombi. 

Baada ya Utapeli huo Kujulikana na Wahanga kufika katika Kituo cha Polisi Ludewa Mjini wakihitaji msaada wa Serikali Pamoja na Kurudishiwa Pesa zao baadhi ya Viongozi wa Kata na wilaya ya Ludewa Ikiwemo Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ludewa pamoja na Diwani wa Kata ya Ludewa Mh, Monica Mchilo walitoa Wito kwa jamii kuwa makini na Utapeli wa Aina hiyo.

Hatahivyo Jeshi la polisi Linaendelea kumshikilia Mtuhumiwa Benward Kayombo na Siku ya Kesho December 22 mwa 2017 Mtuhumiwa huyo Atafikishwa Mahakamani na Wahanga wengine waliotapeliwa Walisema kuwa hakuna Haja ya Kumfunga Benward kwakuwa naye ametapeliwa na Shirika hilo Bila kujua.

Wahanga wa Tukio hilo walisema kuwa walikuwa wanatuma Pesa kiasi cha Tsh, 32,000 wengine 25,000 kwenda kwa Mtu aliye jitambulisha kwa jina la  Yustin Ndone Kabla ya kupewa Fomu ya Maombi baada ya Kutuma pesa hiyo ndipo waliipata Fomu ya Maombi kutoka kwa Bw, Benward Kayombo anaeshikiliwa na Jeshi la Polisi Ludewa Mjini hadi sasa.

Katika Hatua nyingine Afisa Tarafa Mwambao wa ziwa nyasa Bw, Linus Maramba alisambaza taarifa za Shirika hilo katika mwambao wa ziwa nyasa bila kujua kuwa Shirika hilo ni lakitapeli Pamoja na Uongozi wa Madhehebu mbalimbali wilayani Ludewa Ulihusika katika kusambaza Taarifa hizo.



Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: