Mzee Emmanuel Mkolwe Mkazi wa Kijiji cha Mundindi Aliyepata Msamaha wa Rais Magufuli |
Huyu ni Kalentina Mkolwe Mtoto wa Mzee Emanuel Mkolwe, |
Na Maiko Luoga Ludewa,
Mzee Emanuel Mkolwe Mwenye umri wa miaka 70 hadi sasa ambae ni mkazi wa Kijiji cha Mundindi katika kata ya Mundindi wilayani Ludewa katika Mkoa wa Njombe alikamatwa na kuhukumiwa kwa kosa la Mauaji tangu mwaka 1985 akiwa Kijana wa Umri wa miaka 35 kisha kusomewa hukumu ya Kifo katika Gereza Kuu la Isanga Mjini Dodoma.
Mzee Mkolwe Alimweleza mwandishi wa Habari hizi Maiko Luoga kuwa Alikamatwa mwaka 1985 kwakosa la Mauaji kisha akapelekwa katika Gereza la wilaya ya Ludewa IBIHI na Baadae alihamishiwa katika Gereza la MPECHI Njombe mjini ambapo mwaka 1991 Mzee Mkolwe Alihukumiwa Adhabu ya Kifo kisha akahamishiwa katika Gereza Kuu la Isanga Mjini Dodoma.
Katika Kipindi cha Utawala wa Raisi wa Awamu ya Tatu Mzee Benjamini Wiliumu Mkapa Mzee Mkolwe alipata bahati ya Kusamehewa Adhabu ya kifo na kuhukumiwa Adhabu ya Kifungo cha Maisha Jela na Mwaka huu 2017 Katika Utawala wa Rais wa Awamu ya Tano wa DR, John Pombe Magufuli Mzee Emanuel Mkolwe Amepata bahati ya Kusamehewa kupitia msamaha wa Rais na sasa Mzee huyo yupo Huru na Amerejea kijijini Kwake Mundindi wilayani Ludewa katika Mkoa wa Njombe.
Baada ya Kuachiwa Huru Mzee huyo mwenye Umri wa miaka 70 alipokelewa na Mwanae Kalentina Mkolwe Njombe Mjini kisha kumrudisha hadi Nyumbani kwao katika kijiji cha Mundindi wilayani Ludewa ambapo baada ya Kufika nyumbani kwake Mundindi Mzee huyo amekuta mke wake akiwa amerudi kwa wazazi wake na kati ya watoto wake watatu aliowaacha amekuta watoto wawili wamefariki hivyo kwasasa amebaki mtoto mmoja wakike ambae ni Kalentina Mkolwe aliyeenda kumpokea Njombe kwasasa Binti huyo ameolewa anaishi na Mume wake.
Licha ya kukaa muda mrefu Gerezani baada ya Kufika Nyumbani kwake Mzee Mkolwe Alipokwelewa na Mke wake ambae nae kwasasa ni mzee na Wanaendelea kuishi pamoja hatahivyo Mzee huyo ambae ni Mfungwa wa Muda mrefu anawaomba wadau Kumsaidia katika Ugumu wa Maisha aliokuwa nao wasiliana na Mwandishi wa Mtandao huu kupitia 0762705839.kwa msaada zaidi.
Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
0 comments:
Post a Comment