*ASKOFU MHAGAMA AONGOZA MISA YA CHRISTMAS, LUDEWA.*

Na Maiko Luoga Ludewa, 

Kila ifikapo December 25 ya kila mwaka Wakristo wa Tanzania huungana na Wakristo wengine Duniani Kuadhimisha Siku ya Kuzaliwa Kwa Mkombozi wa Ulimwengu YesuKristo mwana wa mungu Ambapo siku hii hujulikana zaidi Kwa jina la Christmas.

Siku ya Leo Jumatatu December 25 mwaka huu 2017 Wakristo wa Kanisa Anglican Ludewa Mjini wameungana na Kusali pamoja katika kanisa Kuu Anglican Ludewa Mjini Kanisa la Watakatifu wote Mtaa wa Ludewa Wakitafakari katika mioyo yao Juu ya Kumpokea yesu ndani ya moyo ili awe bwana na Mwokozi wa maisha yao wakiwa Duniani. 

Misa hiyo takatifu ya Christmas Katika Kanisa Anglican Ludewa Mjini Leo imeongozwa na Mhashamu Baba Askofu wa Kanisa Anglican Diocese ya South West Tanganyika (Njombe) BABA Mathew Mhagama aliyeambatana na Mkewe mpendwa Mama Scholastika Mhagama Huku Askofu huyo Akiwataka Waumini katika Diocese yake kuishi katika maisha ya Kikiristo yenye kumpendeza Mwenyezi Mungu. 

Aidha Askofu Mhagama amewashirikisha Waumini wa kanisa Anglican Ludewa Mjini juu ya Mipango yake ya Kujenga Diocese ya South West Tanganyika kwakuwaomba waumini hao wachangie Michango kwaajili ya kununua Trekta jipya na lakisasa kwaajili ya Kilimo litakalofanya kazi ya kilimo katika Kijiji cha Ibumi na Waumini wameshaanza kumuunga mkono Kwa wazo hilo kwakutoa michango yao Baada ya Misa ya Christmas. 

Akiongea Baada ya Kuhitimisha Misa hiyo ya Kuzaliwa Kwa Yesu Kristo Mchungaji Wa Kanisa Anglican Mtaa wa Ludewa Canon Jofrey Mturo amewataka Waumini wa Anglican Tanzania Kuishi Maisha ya Kumpendeza Mungu Katika siku zote za maisha yao Huku Waumini wa Kanisa Anglican Ludewa Mjini wakisema kuwa Wameipokea Vyema siku hii ya leo na Wanaendelea kumuomba mungu ili Aweze kuwafikisha salama katika Mwaka 2018.

Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: