TFF yaongeza siku tano kwa vilabu kuwasilisha nyaraka za usajili


Makao makuu ya TFF, yaliyoko Ilala, Dar es Salaam
Shirikisho la soka nchini Tanzania (TFF) limeongeza muda hadi Jumamosi Desemba 23, 2017 kwa vilabu kuwasilisha nyaraka za usajili wa dirisha dogo katika ofisi za makao makuu ya TFF Karume, Ilala jijini Dar es Salaam.
Hatua hiyo inatokana na hitilafu iliyotokea siku ya mwisho ya usajili usiku wa Desemba 15, mwaka huu baada mtandao wa mfumo wa usajili kufeli na kusababisha vilabu kushindwa kukamilisha usajili kwa wakati kupitia mfumo huo.
TFF imesema inaendelea na jitihada za kuwasiliana na mwendeshaji wa mfumo huo waliokasimiwa na FIFA walioko Tunis, Tunisia kutatua tatizo hilo la kimtandao haraka iwezekanavyo ili kuweza kukamilisha usajili wa dirisha dogo. 
 Shirikisho hilo limesisitiza vilabu vyote kusajili kwa wakati pale inapotokea dirisha la usajili limefunguliwa




Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: