Kikwete: Magufuli ameweza kuiongoza CCM



 
Kikwete ambae pia ni Mwenyekiti mstaafu wa CCM amewaambia wajumbe wa mkutano huo, alipopitishwa Magufuli kugombea urais mwaka 2015 kulitokea wanaCCM ambao walitilia shaka uzoefu wake ndani ya chama.
Rais Mstaafu wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete amewaeleza wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa Rais Magufuli amefanikiwa kushika hatamu za CCM.
Kikwete ambae pia ni Mwenyekiti mstaafu wa CCM amewaambia wajumbe wa mkutano huo, alipopitishwa Magufuli kugombea urais mwaka 2015 kulitokea wanaCCM ambao walitilia shaka uzoefu wake ndani ya chama.
"Mwanzo waliuliza, oh! Ataweza kuongoza CCM wakati hajawahi kuongoza hata tawi au kata...lakini niliwaambia kuwa inawezekana na leo kaweza," alisema Kikwete na kuongeza "Ilivyo sasa, kazi ya uenyekiti wa chama kama ilivyo kwa Urais, haina shule ya kwenda kusomea. Unajifunza humo humo ndani."
Kwa mujibu wa Kikwete ndani ya mwaka mmoja wa uongozi wake, Magufuli ameweza kuweka wazi mono yake juu ya chama na kuendesha mageuzi makubwa ndani ya chama chetu.
Kikwete pia aliongeza ni Mwalimu Julius Nyerere na yeye pekee ambao walitumia muda wao mwingi ndani ya chama na siasa wakati Rais Mstaafu Benjamin Mkapa alitumia muda mwingi katika diplomasia kabla ya kupata uongozi wa juu wa chama na serikali huku Mzee Ali Hassan Mwinyi akiwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama tu.
"Urais ni kazi ngumu sana,mimi nimefanya, Mzee Mkapa ameifanya, Mzee Mwinyi ameifanya, yaani katika kazi ngumu hii ni kiboko yao na mtani wangu (Rais Magufuli) mpaka sasa nakupa 'big up'."





Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: