CCM wampa Magufuli kura zote za NDIYO


Rais Magufuli ambaye alikabidhiwa mikoba ya uenyekiti kutoka kwa Rias Mstaafu Jakaya Kikwete mwezi Julai mwaka jana amezoa kura zote 1821 ambazo zilipigwa katika nafasi hiyo.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi leo Jumatatu Desemba 18 wamemchagua kwa kishindo Rais John Pombe Magufuli kundelea kukiongoza chama hicho kwa miaka mitano ijayo.
Rais Magufuli ambaye alikabidhiwa mikoba ya uenyekiti kutoka kwa Rias Mstaafu Jakaya Kikwete mwezi Julai mwaka jana amezoa kura zote 1821 ambazo zilipigwa katika nafasi hiyo.
Katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) Rais wa Zanzibar Dr Ali Mohammed Shein pia alizoa kura zote 1819 amabzo zilipigwa katika nafasi hiyo. Kwa upande wa Bara Philip Mangula alipata kura 1826 kati ya kura 1827 zilizopigwa, huku kura moja ikiharibika.
Akihutubia wajumbe wa mkutano huo baada ya kutangazwa mshindi, Magufuli alisema kuwa Imani iliyooneshwa kwake atailipa kwa uchapakazi.
“Kazi kubwa zaidi iliyo mbele yetu ni kuhakikisha kuwa tunapata ushindi wa kishindo katika chaguzi zinazokuja. Hiyo ndiyo itakuwa namna pekee ya kuwalipa kwa Imani mnayotuonesha,”alisema Magufuli.
Katika hatua nyengine, mwanasiasa mkongwe Stephen Wasira 'afunika' kura za ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) akusanya kura 1505 kati ya kura halali 1779



Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: