Cyril Ramaphosa atawazwa kuwa mrithi wa Jacob Zuma baada ya kushinda uchaguzi ANC


Ramaphosa (65) sasa amejiweka katika nafasi nzuri ya kushinda urais baada ya uchaguzi wa mwaka 2019.
Chama tawala nchini Afrika Kusini African National Congress (ANC) kimemchagua Cyril Ramaphosa kurithi hatamu za uongozi wa chama hicho.
Ramaphosa ambaye ni Makamu wa Rais wa Afrika Kusini amemshinda kwa kupata kura 2,440 dhidi ya 2,261 alizopata waziri wa Zamani na Katibu Mkuu wa Umoja wa Afrika (AU) na mtaliki wa Rais Zuma Bi Nkosazana Dlamini-Zuma.
Uwaniaji madaraka baina ya wawili hao umeleta mvutano mkubwa wa kisiasa, hali inayoleta hofu kuwa ANC inaweza kugawanyika kabla ya uchaguzi wa 2019.
Rais Zuma ameonya kuwa chama kimo hatarini na kimo kwenye njia panda.
Ramaphosa (65) sasa amejiweka katika nafasi nzuri ya kushinda urais baada ya uchaguzi wa mwaka 2019.



Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: