Afikishwa mahakamani kwa kumbaka Ajuza wa miaka 90 Tabora



Mtuhumiwa Hamisi Donald akiwa chini ya ulinzi mkali mahakamani.
Mwanaume mmoja anayefahamika kwa jina la Hamisi Donald mwenye umri wa miaka thelathini na tano amefikishwa mahakamani hii leo katika Mahakama ya hakimu mkazi mkoa  wa  Tabora kwa tuhuma za kumbaka kikongwe mwenye umri wa miaka tisini huko katika kijiji cha Miswaki wilayani  Uyui mkoani humo.
Akisoma maelezo ya kosa mbele ya hakimu mkazi mfawidhi Joktan Rushwela,Wakili upande wa Jamhuri Hildeforce Mukandala ameieleza mahakama  hiyo  kuwa mnamo tarehe 4 disemba mwaka huu mtuhumiwa Hamisi Donald anadaiwa kumbaka bibi mwenye umri wa miaka tisini ambaye jina lake linahifadhiwa.
Huko katika kijiji cha Miswaki wilayani Uyui,Mtuhumiwa Hamisi Donald anadaiwa kutenda kosa hilo kinyume na kifungu namba 130 kifungu kidogo cha 1 na  cha  2 (a)  na   kifungu 131 kidogo cha 1 kanuni ya adhabu sura 16 iliyofanyiwa  marejeo mwaka  2002.
Kwa mujibu wa Wakili huyo wa Serikali Mukandala  aliambia mahakama hiyo  kwamba upelelezi wa shauri hilo umekamilika hivyo mahakama imepanga kuanza kusikiliza kesi hiyo mnamo tarehe 2 Januari 2018.  



Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: