WAKOSA ELIMU YA MSINGI, WATEMBEA KILOMITA SABA ,LUDEWA



NA MAIKO LUOGA, LUDEWA
  Wakazi wa kitongoji cha Lutemaluchi katika kijiji cha Kiyombo kilichopo katika kata ya Lubonde wilayani Ludewa hapa mkoani Njombe wanakabiliwa na tatizo la ukosefu wa Huduma ya Afya katika kitongoji chao pamoja na ukosefu wa Shule ya Msingi.

Kitongoji hicho kipo umbali wa klomita saba kutoka kijiji cha Kiyombo haliinayowalazimu watoto wa kitongoji hicho kutembea umbali mrefu kutoka majumbani kwao Lutemaluchi kuelekea Shuleni katika Kijiji cha Kiyombo na baada ya Masomo wanalazimika kurejea tena Nyumbani Lutemaluchi.

Mwanahabari wetu alifika katika kitongoji hicho na kukutana na watoto hao njiani wakielekea Shuleni kwa miguu kisha kuzungumza na wananchi wa Lutemaluchi ambao baada ya Kuliona tatizo hilo kwapamoja wameamua kuanza ujenzi wa Shule ya msingi katika Kitongoji chao yenye Vyumba viwili vya madarasa na Ofisi moja ya walimu.

Alipotafutwa Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Bw, Ng”wilabuzu Ndatwa Ludigija ili kuzungumzia Changamoto hiyo alisema kuwa Halmashauri inakiri kuwa watoto kutembea umbari wa kilomita saba ni tatizo kubwa huku aliwapongeza wananchi wa Lutemaluchi kwa hatua waliyochukua ya kuanza ujenzi wa shule ambayo itapunguza tatizo la watoto wao kutembea umbali mrefu kuelekea shuleni Kiyombo.

Aidha aliongeza kuwa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa inauagiza uongozi wa Kata ya Lubonde kupeleka mradi huo halmashauri ili uweze kuingizwa kwenye bajeti ijayo kwaajili ya kuwasaidia wananchi hao wa Kitongoji cha Lutemaluchi .

Licha ya kuanza ujenzi huo wananchi wa Lutemaluchi walimweleza mwandishi wetu kuwa wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa vifaa vya kumalizia jengo hilo la shule ya Msingi Lutemaluchi hasa vifaa vya kiwandani ikiwemo Bati, Saruji, Nondo Nk. Hivyo kufuatia matatizo hayo wananchi wa Lutemaluchi wanawaomba wadau kote nchini Kuwasaidia ili kufanikisha kumaliza kabisa jengo hilo la Shule ya Msingi Lutemaluchi.

   "Jamani watoto wetu wanakosa elimu hawajasoma kabisa kitongoji hiki vijana hawana elimu wanaenda shuleni hawafiki wanaamua kurudia njiani tatizo shule ipo mbali mno kule Kiyombo Mvua ikinyesha au mwezi wa sita kunabaridi kali sana sasa watoto hawa bado ni wadogo wanaamua kurudi nyumbani shule iko mbali sana umbali wa Kilomita saba Sasa ndugu mtaalamu wa Habari tunakuomba utusaidie tupate wadau pamoja na wafadhiri watuchangie hata Smenti na Bati" Walisema wananchi hao wa Lutemaluchi.



Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: