MARUFUKU KUFULIA MAJI YA MITO LUDEWA


               NA MAIKO LUOGA LUDEWA,
Wananchi wilayani Ludewa wametakiwa kuacha mara moja tabia ya kutumia maji ya mito katika maeneo yao kufulia nguo kwakuwa kwakufanya hivyo ni kuhatarisha afya za wengine.

Akitoa zuio hilo Hivi karibuni kwa wananchi wa Ludewa mjini Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Bi, Monica Mchilo Alisema kuwa kuna baadhi ya wananchi wamekuwa wakibeba nguo zao na kwenda kufua kwenye mito iliyo jirani na maeneo yao kitendo ambacho hakikubaliki kwakuwa miongoni mwa Wana Ludewa wanayatumia maji hayo kwa matumizi ya Nyumbani ikiwemo kunywa na kupikia.

Aliongeza kuwa Uongozi wa Halmashauri pamoja na kata ya Ludewa utaweka Ulinzi mkali katika Mito inayowazunguka wananchi hao ili kuzuia kabisa tabia za watu wanaofua nguo zao ndani ya mito hiyo.

Kwaupande wao baadhi ya wananchi wa Ludewa Mjini walimweleza Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa kuwa Akina mama Wajawazito wanaoishi wakiwa wanasubiri siku zao za kujifungua katika eneo la Mwembeni kuwa ndio wahusika wakuu wa Kufua nguo zao katika Mito hali ambayo imemlazimu Bi, Monica Mchilo kutoa agizo kwa Mtaalamu wa Afya wilaya ya Ludewa Kuwachukulia hatua maramoja wajawazito hao wanaohatarisha Usalama wa Afya za wengine.

    ''Nakuagiza wewe mtalamu wa Afya nenda ukazungumze na wale akina mama wajawazito wanaojingojea pale mwembeni kuwa wale wauguzi wao wakachote maji na kufulia palepale kwenye kambi ya wajawazito maana pale tumewajengea bafu na kilakitu sasa inakuwaje wafulie mtoni huko ni kuwatafutia matatizo ya kiafya watu wengine maana maji yale ya mtoni wengine wanayatumia kwakunywa na kupikia majumbani mwao sasa tusiwahatarishe wenzetu Afya zao''
 Alisema Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Bi, Monica Mchilo Ambae pia ni Diwani wa kata ya Ludewa Mkoani Njombe, 



Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: