Diwani wa kata ya Lubonde Mh, Nicolaus Mgaya Akifanya usafi na wananchi wake, |
Wananchi wa kijiji cha Masimbwe wilayani Ludewa wakiendelea na zoezi la Usafi katika Eneo la Mselesele, |
Wakati Tanzania ikiungana na nchi nyingine Duniani Kuadhimisha kilelele cha siku ya Usafi Duniani Wananchi wa Kijiji cha masimbwe wilayani Ludewa katika Mkoa wa Njombe Jana November 20 mwaka huu 2017 waliadhimisha siku hiyo kwakufanya Usafi katika Kitongoji cha Mselesele.
Kilele cha siku ya usafi kinafanyika Kila mwaka ifikapo November 20 na wananchi wa Kata ya Lubonde waliamua kuadhimisha siku hiyo katika kitongoji cha Mselesele ilipo Kambi ya kampuni ya Kikorea CHEW WANG CAMPANY inayofanya kazi ya ujenzi wa Barabara ya Lami kilomita 50 kutoka Lusitu hadi mawengi.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika eneo hilo la usafi wakizungumza na Diwani wa kata ya Lubonde Mh, Nicolaus Mgaya jana walituma salamu za malalamiko kwa Uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa wakidai kuwa wanateseka na kutaabika kwa kukosa maji katika kitongoji chao hali ambayoinaweza kuhatarisha Afya za wananchi hao.
Uongozi wa Kata ya Lubonde Ukiongozwa na Diwani wa Kata hiyo Mh, Nicolaus Mgaya Licha ya kuwaagiza Wafanyabiashara katika eneo la Mselesele kuwa wanatakiwa kuwa na Vyoo Bora ili kuepukana na mlipuko wa Magonjwa pia Umewahakikishia wananchi kuwa Huduma hiyo ya Maji itawafikia wananchi katika Kitongoji chao.
Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
0 comments:
Post a Comment