Afisa Mazingira Wilaya ya Ludewa Bw, Erasmo Mshindo Akizungumza na Wananchi waliojitokeza Kwa wingi kufanya Usafi katika Eneo la Hospital ya wilaya Ludewa Mjini, |
Afisa mazingira wilaya ya Ludewa Bw, Erasmo Mshindo akishiriki Usafi na Wananchi Ludewa mjini. |
Ni mwonekano wa Baadhi ya Mazingira yaliyofanyiwa usafi katika eneo la Hospital Ludewa mjini. |
Na Maiko Luoga Ludewa.
Serikali ya Awamu ya tano ili tangaza kuwa kila jumamosi ya mwisho wa mwezi itakuwa ni siku ya kufanya usafi kwa nchi nzima lengo likiwa ni kuhakikisha jamii ya Wa Tanzania inaendelea kuwa salama katika mazingira pamoja na Afya za waTanzania.
Wananchi Wilayani Ludewa katika Mkoa wa Njombe leo November 25 mwaka huu 2017 ikiwa ni jumamosi ya mwisho wa mwezi November wameungana pamoja wakiongozwa na Katibu Tawala wilaya ya Ludewa Bi, Zaina Mfaume Mlawa na kufanya usafi kuzunguka eneo la Hospital ya Wilaya Ludewa Mjini.
Akizungumza baada ya zoezi la kufanya usafi kukamilika Katibu tawala wilaya ya Ludewa Bi,Zaina Mlawa alisema kuwa wananchi wa Ludewa mjini pamoja na Watumishi mbalimbali walijitokeza kwa wingi katika Hospital ya wilaya ya Ludewa na kushiriki zoezi hilo huku akisema kuwa mkakati wa Serikali ni kuzidi kuhamasisha wa Tanzania kuendelea kufanya usafi kuanzia Majumbani kwao hadi kwenye mazigira yanayowazunguka.
Kwaupande wake katibu wa afya wilaya ya Ludewa mkoani Njombe Bw, Godlove Katemba pamoja na Afisa mazingira wilaya ya Ludewa Bw, Erasmo Mshindo kwapamoja waliipongeza Halmashauri ya wilaya ya Ludewa kwakuamua kuwa usafi ufanyike katika eneo la hospital ya wilaya kwakuwa uongozi wa Hospital hiyo umekuwa ukilipa pesa kubwa kwa watu waliokuwa wakifanya usafi katika mazingira hayo ya Hospital.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kufanya usafi katika eneo la Hospital ya wilaya ya Ludewa walisema kuwa wanaendelea kuiunga mkono serikali ya Awamu ya tano chini ya Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dr.John Pombe Magufuli huku wakiiomba Halmashauri ya wilaya ya Ludewa kutembelea Katika maeneo ya Vijijini ili kuzidi kuhamasisha Usafi kwa lengo la kuboresha mazingira na Afya za Wananchi.
Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
0 comments:
Post a Comment