CCM WILAYA YA MAKETE WAPATA MWENYEKITI MPYA ATEMA CHECHE BAADA YA KUTANGAZWA,




 Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Makete Ona Nkwama (kushoto) akipongezwa na mwenyekiti aliyemaliza muda wake Francis Chaula mara baada ya kuibuka mshindi
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Makete Ona Nkwama akizungumza mara baada ya kutangazwa mshindi
;;;;;
Hatimaye chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Makete mkoani Njombe kimefanya uchaguzi wake katika nafasi tofauti tofauti ikiwemo nafasi  ya mwenyekiti ambapo Ndugu Ona Amosi Sukunala Nkwama amechaguliwa kuwa mwenyekiti na hii ni baada ya uchaguzi huo kuahirishwa oktoba 2 mwaka huu.

Akitangaza matokeo hayo ya uchaguzi katika ngazi ya mwenyekiti, msimamizi wa uchaguzi huo Antony Akim alisema  Ndugu Ona ameshinda nafasi hiyo kwa kupata kura 283 akifuatiwa na Aida Chengula aliyepata kura 180 na ndugu Mwawite Ngailo akipata kura 77.
Katika hatua nyingine Ndugu Yusufu Kisimbilo Sanga alishinda katika nafasi ya Katibu mwenezi wilaya kwa kumuacha kwa tofauti ya kura 5 mpinzani wake wa karibu ndugu Tito Onia  huku nafasi za wajumbe wa mkutano mkuu Taifa zikichukuliwa na Joyce Sigala, Daniel  Okoka, na Egnatio Mtawa.
Mara baada ya kumalizika kwa  uchaguzi huo mwenyekiti aliyechaguliwa ndugu Ona Nkwama alisema atahakikisha rushwa inamalizika ndani ya chama hicho pamoja na kuyaondoa makundi yaliyopo katika chama hicho ambayo yameonekana kukigharimu chama.
"Nimesema wakati wa kampeni kuwa mimi ni kiboko ya rushwa na makundi ndani ya CCM, Nilikwenda China kusomea mambo hayo na nilipelekwa na Kinana kwa kazi hiyo, sasa sitanii nataka makete iwe wilaya ya Mfano, ole wenu mnaokula rushwa na mnaoendeleza makundi, nawafahamu wote kwa majina wanakokaa na wanakofanya kazi, acheni tukijenge chama chetu, Fransis alikuwa mpole sasa mimi ni mkali kweli" alisema Ona.
Uchaguzi huo ulifanyika November 26 mwaka huu baada ya kushindwa kufanyika Oktoba 2 kutokana na halmashauri kuu kukataa majina yote ya wagombea katika ngazi ya Mwenyeki kwa madai kuwa wamekosa sifa.


Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: