WAZIRI AMUUNGA MKONO MBUNGE WA VITI MAALUMU LUDEWA,



Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Njombe Mh, Neema Mgaya Kushoto Akiwa na Naibu waziri TAMISEMI Mh, Josephat Kandege Katikati na Wakwanza kutoka Kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Ludewa Mh, Stanley Kolimba
Naibu Waziri wa TAMISEMI Mh, Josephat Kandege akiteta Jambo na Mbunge wa Viti maalumu mkoa wa Njombe Mh, Neema Mgaya Katika ukumbi wa CCM Ludewa mjini
Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Njombe Mh, Neema Mgaya Akitoa vifaa vya michezo kwa timu ya wanawake wilaya ya Ludewa ,Mapinduzi Queens Ambayo ni Bingwa wa Mkoa wa Njombe.
Baadhi ya wachezaji Timu ya Wanawake Wilaya ya Ludewa Mapinduzi Queens Wakitoa Shukrani zao kwa Mbunge wa Mkoa wa Njombe Mh, Neema Mgaya kwa zawadi alizowapa.
NA Maiko Luoga Ludewa,
 Ili kuhakikisha lengo la serikali ya awamu ya tano Kufikia Tanzania ya viwanda linatimia Baadhi ya viongozi Mkoani Njombe Wameanza kumuunga mkono Rais wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli Kwa vitendo.
 
Mh, Neema Mgaya ni Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa njombe kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM ameamua kutoa msaada wa Vyerehani 370 kwa vikundi vya wanawake wa mkoa wa Njombe vyenye zaidi ya Tsh, Milioni 90 ambavyo ni sawa na viwanda vidogovidogo zaidi ya 90 kwakuwa Vyerehani vinne ni sawa na kiwanda kidogo kimoja.

Akiwa wilayani Ludewa November 24 mwaka huu Mh, Neema Mgaya Alikabidhi vyerehani 64 kwa vikundi vya wanawake wa Tarafa za Liganga, Mawengi, Mlangali, Masasi, na Tarafa ya Mwambao pamoja na Kukabidhi vifaa vya Michezo kwa timu ya wanawake ya Mapinduzi Queens Ambayo ni Bingwa wa Mkoa wa Njombe.

Aidha Mbunge huyo wa Viti maalumu pia Alimkabidhi Afisa Elimu wa shule za sekondari wilaya ya Ludewa bw, Matenus Ndumbaro Vitabu vya Masomo ya ziada kwa shule 23 za sekondari zilizopo ndani ya wilaya ya Ludewa ambazo ni za Serikali pamoja na Shule za Binafsi kwaajili ya kuwasaidia wanafunzi kuongeza Maarifa kwa Muda wa ziada.

Kwaupande wake Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh, Josephat Kandege aliyefika wilayani Ludewa Kumuunga mkono Mh, Neema Mgaya Alimpongeza Mbunge huyo kwa uamuzi huo alioufanya wa kuwainua kiuchumi wanawake wa Mkoa wa Njombe.


Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: