Klabu ya Azam FC, imepata pigo kubwa baada ya kocha wake Aristica Cioaba, kufungiwa kutokaa benchi mechi tatu kwa kosa la kuwafokea waamuzi wa mchezo wao dhidi ya Ruvu Shooting ya Pwani ambao ulipigwa uwanja wa Azam Complex.
Mtendaji Mkuu wa Bodi ya ligi Boniface Wambura ameiambia Goal, wameamua kumfungia Cioaba, ili kuongeza nidhamu kwa waamuzi ambao mara nyingi wameshindwa kuwajibika na majukumu yao na kuwasingizia waamuzi pindi wanapopoteza mechi.
"Tumetumia kifungu cha 40(1), kumfungia Cioaba pamoja na kulipa faini ya sh. laki tano ili iwe fundisho kwa makocha wengine wenye tabia kama hizo ambazo zimekuwa zikileta picha mbaya na kuwadhalilisha waamuzi wetu," amesema Wambura.
Kiongozi huyo wa bodi ya ligi amesema adhabu ya Cioaba, imeanza mara moja baada ya kutangazwa na baada ya kumaliza wataendelea kumfatilia kwa karibu ili kujua kama atakuwa amejirekebisha au kuacha kabisa tabia hiyo ambayo asingependa kuona ikiendelea.
Hiyo ni mara ya kwanza kwa Cioaba raia wa Romania, kukumbana na adhabu kama hiyo tangu ajiunge na timu mwezi januari akichukua mikoba ya Muhispania Zeben Hernandez ambaye alitimuliwa kazi kutokana na mwenendo mbaya wa timu hiyo
Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
0 comments:
Post a Comment