Ni baadhi ya wananchi waliojitokeza katika mkutano huo wa Kijiji Ludewa Mjini |
Aliyesimama ni Monica Mchilo Diwani wa kata ya Ludewa na Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Ludewa akizungumza na wananchi waliojitokeza katika mkutano. |
NA MAIKO LUOGA, LUDEWA
Kamati ya mradi wa Trekta kijiji cha Ludewa Mjini katika kata na wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe jana ilitoa taarifa ya mapato na Matumizi ya Mradi huo kuanzia mwezi January Hadi September mwaka huu 2017.
Akisoma taarifa hiyo kwa wananchi waliojitokeza kwa wingi katika mkutano wa Kusikiliza taarifa za miradi mbalimbali ya maendeleo ya Kijiji cha Ludewa Mjini mkutano uliofanyika siku ya jana Jumatatu November 13 mwaka huu 2017 katika Eneo la Ofisi ya kijiji cha Ludewa mjini katibu wa mradi huo Bw, Helmani Luoga amesema kuwa Salio anzia ilikuwa Kiasi cha Tsh, Million 19,816,108.02.
Aliongeza kuwa Jumla kuu ya pesa ya mradi huo wa Trekta kuanzia mwezi Januari hadi September ilikuwa Milioni 26,585, 608.02 na Matumizi ilikuwa ni Millioni 7,139,750 na Kiasi kilichobaki Benk Million 19,445,858.02 huku kiasi cha madeni ikiwa ni Tsh 150,000.
Baada ya kusomwewa taarifa hiyo ya Mapato na matumizi ya Mradi wa Trekta kijiji cha Ludewa Mjini Wananchi walioshiriki mkutano huo walionesha kutokuwa na imani na Taarifa hiyo huku wakisema kuwa Taarifa hiyo inaonesha pesa ya mradi inatumika zaidi kuliko inayoingia kwenye mradi.
Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
0 comments:
Post a Comment