MIFUGO KUPIGWA CHAPA, PEMBEJEO ZA SHUKA BEI LUDEWA



        NA MAIKO LUOGA, LUDEWA
Wafugaji wa Ng’ombe wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe wameagizwa kuweka alama za Utambulisho wa mifugo yao ili kuepuka matatizo yanayoweza kujitokeza kati ya wakulima na wafugaji.

Agizo hilo lilitolewa hivi karibuni na Afisa mifugo na uvuvi wilaya ya Ludewa Bw, Marko Mhagama na kuongeza kuwa lengo la kuweka alama hizo katika mifugo kwanza ni kuwatambua wafugaji na idadi ya mifugo yao, Kuzuia wizi, magonjwa pamoja na Ugomvi kati ya Wakulima na wafugaji.

Wakizungumza na Kituo hiki Baadhi ya Wafugaji wilayani Ludewa katika Mkoa wa Njombe licha ya kuipongeza serikali kwa utaratibu huo pia walihoji kuwa itakuwaje endapo mfugaji atahitaji kuuza mifugo yake ambayoimesha wekwa alama swali ambalo limejibiwa na Afisa mifugo wilaya ya Ludewa.

Katika hatua nyingine serikali imetangaza Bei Elekezi ya Mbolea ya kupandia na Kukuzia kwa wakulima katika Halmashauri ya wilaya ya Ludewa kwa mwaka huu 2017 hivyo Mbolea ya kupandia aina ya DAP itauzwa kwa TSH, 53,871 na Mbolea ya Kukuzia UREA itauzwa kwa Tsh, 41,292.

Kufuatia Bei hizo elekezi Wakala wa Pembejeo kwa wakulima Wilaya ya Ludewa wameaswa kuwauzia wakulima pembejeo kwakuzingatia bei zilizopangwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa muuzaji yeyote atakayekiuka Maagizo ya Bei elekezi.



Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: