CHOMBEZO; HEHEEE, KANTANGAZEEE!!! SEHEMU YA KUMI NA SITA



Ninafanikiwa kutoka huku ninapotoka ninamuona Baby anakurupuka pale chini alipolala khanga yake anaiacha chini mbio anawahi mlango akiwa uchi kama alivyozaliwa. Njasi anafanikiwa kuinuka nae anataka kukimbia hasa anaponiona mie ninajikung’uta huku mashaka yamenijaa anahisi asije kudondoka akamfata yeye.
Nipo kama nilivyozaliwa ninainama naichukua Khanga yangu ninaikung’uta mara kadhaa ninaivaa, kisha ninachukua kiatu ninainua Kitanda ninafanikiwa kumuua Nge aliekuwa mbele ya uso wangu wakati Yule aliekuwa ananitambaa sijui kama ni mdudu gani wala sijamuona tena na sijui hata amedondokea wapi!
Ninatoka sebuleni kabla sijakaa katika sofa, mara ninauona mlango wa mbele unafunguliwa mara meneja anaingia ndani ya sebule.
Haa kumbe mlango hawajaufunga hawa dah! wakati ninamshangaa meneja mara njemba tatu nazo zinasogeza mlango kwa maana yakuufungua zaidi, wanajichoma ndani kwa kujiamini sana. Wanatembea hadi nilipo mikono yao wameiweka katika vifua vyao kama wamefunga swala wananitazama kwa dharau. Ninawatizama kwa mashaka, ninatizamana nao macho kwa macho!!!

“Dobe upo chini ya ulinzi kwa kosa la kumuibia muajiri wako. Hivyo tunakwenda na wewe kituoni kwa maelezo zaidi”.
Askari ananiamrisha na kuniweka chini ya ulinzi.
“Sawa nimesikia ngoja nikavae kwani ndiyo nilikuwa ninataka kuoga hata sijaoga hapa.”
Ninawajibu hawa askari, ili wanipe nafasi ya kujimwagia maji tu ili kuondosha Janaba, kwani majumba ya Mahabusu niende na majanaba, moyo wangu unakataa.
“Kuoga hapana hatuna muda wa kupoteza ila kubadili nguo hilo ninakuruhusu unaweza kuvaa ukiwa chini ya usimamizi wa askari.”
Ninainuka kuelekea chumbani kwa Baby Girl ili akanione kama nimekamatwa ili anifanyie maarifa. Kwani sina hata senti nyekundu nilipo na mambo haya dhamana bila kuwa na mpunga mfukoni huwa inakwenda pole pole sana.
Ninamuona askari mmoja akinifata kwa karibu huku mkono wake wa kulia akiuweka karibu kabisa na kiuno chake. Nikafahamu hapo kiunoni lazima kuna mguu wa kuku umewekwa!
Ninapoingia ndani chumbani yule askari anabakia nje ya chumba kunisubiri. Ninapiga hatua kadhaa kumuelekea Baby Girl kitandani alipojilaza akiwa amelala chali hana nguo, lakini pia akiwa anahema kwa tabu sana. Inaonekana Presha ya kushuka inamsumbua kwani amekimbia mbio, lakini pia mshtuko alioupata wa Nge umemsababishia kupoteza fahamu yake na presha kushuka chini.
Ninajitahidi kumuamsha na kumsemesha lakini sipati ushirikiano wake. Baby nikiuinua mkono wake juu nikiuachia unaanguka peke yake! Nimetaharuki hapa sina namna kwa kweli kwani moyo wangu unaniuma mie kwenda polisi wakati Baby yupo katika hali hii.
Ninachukua Khanga ninamfunika kisha ninatoka nje ya mlango ninamwambia huyu askari.
“Ninaomba msada waje wanawake wamvalishe nguo Baby wangu, kisha tumpeleke hospitali kwani hali yake mbaya sana.”
Askari ananitazama kwa makini.
“Wewe twende kituoni kisha ya huku nyuma yawache kama yalivyo.”
Ninashindwa kumuelewa kabisa.
“Yaani mtu yupo hivi unasema niyaache kama yalivyo?!”
Ninamuuliza kwa ghazabu lakini yeye badala yakutilia maanani ananidharau na kunitolea tabasamu lake baya.
Ninaelekea sebuleni ili kutaka msaada, lakini huyu askari niliekuwa nae ananishika kwa nyuma kwenye kiuno na kunisukumia mbele kama vile anipeleke kituuteni. Ninajaribu kugeuka lakini ninashindwa nguvu nae, hivyo ananipelekesha hadi mlangoni ninazuwia mlango kwa mikono yangu na miguu, huku nikilalamika.
“Nimefanyaje hadi mnipeleke msobemsobe namna hii, mtu amezidiwa ndani wewe hunielewi bwana aaaagh mie mtaniulia hapa lakini siendi kama Baby hajapelekwa hospitali!”
Ninaposema maneno hayo, mara ninaanza kupigwa ngumi za mbavu ili niachie mikono yangu. Lakini mie bado nimeng’ang’ana tu.
“Mtamuumiza jamani, kwa nini msitumie busara tu kuliko hiyo nguvu isiyokuwa na ulazima.”
Njasi analalamika kwa uchungu. Nami ninapata nguvu. Ninaanza kuleta ligi ya ubishi yakutotii sheria bila shuruti.
“Dada usitufundishe kazi, sie tunatimiza wajibu wetu, huyu anapokaidi agizo halali ni kuvunja sheria kwa hiyo sheria inaturuhusu kutumia nguvu kadiri iwezekanavyo kama muhalifu hataki kutii sheria bila shuruti.”
Askari anaposema maneno hayo, mie ninageuza sura yangu ninamtazama Meneja wangu, ninamuona ameweka mikono kifuani mwake, kisha ameuinua uso wake juu ili nisiyaone macho yake.
Askari wakaongeza nguvu wote watatu wakaja kunibeba nikatolewa nje ya nyumba nami ninawaletea Ujela ninaivua Khanga inadondoka chini vyombo nje, watu kibao!
“Mnanizalilisha namna hii, kwa sababu gani, wewe malaya nimekuibia pesa zako mie wewe, poa sana Polisi wamejengewa watu mie ninaenda lakini haibadili msimamo wangu kwako sikutakiiiii!!!”
Ninamchana Live meneja ambae alikuwa ametoka nje na askari.
“Wewe unaongea juu ya nini, mie ninataka wanaume wezi kama wewe! Utarejesha pesa zangu milioni tatu ulizoiba kazini kwangu jana!”
Maneno ya meneja yamenirudisha nyuma kidogo. Mie nimeiba milioni tatu zake? Tuseme hiyo nyumba alilipia pesa hiyo kweli? Ninashindwa kupata jibu.
Gari ndogo inasogezwa kwa haraka inafunguliwa milango ninaingizwa kwa haraka. Ninatupiwa Khanga yangu kisha kila upande anapanda askari, na askari aliekuwa ananiuliza maswali ninamuona anaingia katika gari nyingine na Meneja.
Ninamtazama Njasi ninamuona analia huku anazungumza na simu yake, lakini sisikii anazungumza nini wala na nani.
Baby Girl kwa heri wangu, mie ninakomeshwa kwa sababu ya maamuzi yangu tu, ama kweli mwenye pesa siyo mwenzako. Ninajisemea kimoyomoyo gari inaondolewa watu wakiwa wameanza kujaa.
“Wewe Dobe umejifanya kutuwekea jeuri hapa kwenu sasa subiri ufike kituoni, utajuta kutufahamu, yaani wewe unagoma kukamatwa wewe!”
Ninakamiwa hata kuko kituoni penyewe bado sijafika!
“Lakini naomba mngeuvaa uhalisia wangu kama nyie ndiyo mngekuwa mie mnge…….!
Sijamaliza kauli yangu ninanyukwa kibao matata sana ninaona nyota mbele ya macho yangu.
“Kelele wewe usitulinganishe na wewe sie.”
Haya ninalo tena, siku ya jana tu ilikuwa ninastarehe kwa raha. Nikahongwa pesa nikapikiwa chakula maalumu, ila naona siku ya leo ya majuto tu kwangu. Kwani Kasheshe lilianzia uvunguni na Nge, sasa nipo mikononi mwa Polisi makofi nayo ndiyo hivi, basi inabidi niwe mpole tu kwani chombo cha dola hapana chezea kabisa.
Gari inasonga mbele tunaelekea kituo cha polisi mara ninamsikia askari aliekuwa pembeni yangu simu yake inaita, nae anaipokea.
“Ndiyo kiongozi, ehee sawa kiongozi, ahaa hamna shida nimekusoma Afande, nitafanya hivyo.”
Mie ninashindwa kuambua chochote cha maana.
“Dereva peleka gari Sinza moja kwa moja!”
Moyo wangu unaanza kwenda mbio Sinza tena siyo kituo cha polisi Tabata?!
“Jamani msende kunitesa mie siyo mwizi, yule dada ananipakazia tu mie siyo mwizi kabisa.”
Ninawaambia hawa askari lakini hakuna hata mmoja anaeshughulika na mie, kila mmoja ananinyamazia kimya.
Gari inatembea tunafika kituo cha Polisi Tabata Shule, gari haiingizwi kushoto kituoni, badala yake inanyoosha tu! Ninawaza mengi sana katika akili yangu lakini siyapatii majibu. Hivi hawa ni askari wa kituo cha Tabata vipi wanipeleke Sinza? Tabata ni wilaya ya Ilala sasa napelekwa wilaya ya Kinondoni kufata nini, hawa inavyoonekana siyo watu wazuri wanaweza kuniuwa bure. Akili yangu inaanza kuingia na wasiwasi na hawa watu kama ni askari wa kweli, au ni watu tu Meneja amewakodisha ili kunishughulikia.
Gari inachanja mbuga hadi katika makutano ya barabara ya Mandela na Tabata, dereva anapinda kushoto tunaingia barabara ya Mandela tukielekea Ubungo. Nimenyamaza kimya sina maneno yashaniishia yote, natizama hatima yangu tu. Ubungo napo tunapafikia tunapinda kulia kama tunakwenda Manzese, kisha tukapinda kushoto katika barabara ya Shekilango. Gari imetembea hadi Sinza Madukani inapinda kulia na mara tukatokezea katika nyumba nzuri ya Kifahari na ya kisasa. Geti linafunguliwa magari yanaingizwa ndani, kisha wanatulia kabisa. Yaani ilikuwa kama wanaosubiri amri ili watekeleze.
“Shuka chini Dobe.”
Askari wananiambia nami ninashuka chini huku ninavaa Khanga yangu.
Ninawaza mbona leo kazi ninayo? Wanaume hawa wakinilawiti nitakuwa mtu mie kweli?! Ninaongozwa hadi ndani ya nyumba hiyo na Mlinzi aliekuwa akizungumza na simu kwa lugha ya Kichaga cha Kimachame.
“Dobe karibu sana nyumbani naona hapa kuna mawili aidha unirudishie pesa yangu uliyoniibia au ukaozee jela, maamuzi unayo mwenyewe!”
Meneja ananambia maneno hayo huku akikaa katika Sofa matata sana la ngozi.
“Askari asante sana kwa kufanikisha hili zoezi, huyu ninawaomba niongee nae, kama hataki kutoa ushirikiano basi ninawapigia ili mumfate mfanye yenu, lakini akikubali kunirudishia pesa zangu basi sitawaita tena ila tu msicheze mbali.”
Meneja anamalizia maneno hayo ananitia uchungu sana. Wale askari wanaondoka ndani ya chumba hiki, Meneja ananitaka nikae katika sofa, lakini mie ninaamua kukaa chini ya Zulia. Ninayazungusha macho yangu katika ukuta wa nyumba, ninatizama picha nzuri na nyingi zilizowekwa.
“Dobe hukuja hapa kushangaa picha, bali nimekuleta hapa kwa sababu maalumu. Kama utatii ninachotaka kutoka kwako ukaniridhia, basi utaishi katika maisha mazuri hamna! Lakini ukijidai kuniona unavyoniona nitayafanya maisha yako yawe mabaya sana! Unanielewa?”
Ninamtazama Meneja bila kumsemesha jambo.
“Dobe nimetoa pesa milioni tatu kukupangia nyumba hii. Na hapa ulipokaa ndiyo nyumbani kwako kupya kutoka sasa. Imekuwa vizuri umekuja hapa na upande wa Khanga tu, mie nitakununulia nguo na kila utakacho utapata kwangu, ila ni sharti moja ukilifanya hilo basi utakaa kwa wema sana, na utainjoi maisha.”
Meneja anapoitaja milioni tatu ndiyo nakumbuka wizi nilioambiwa nimeiba milioni tatu kumbe alikuwa anamaanisha hivi? Haya mie nyumba ya milioni tatu ninaiweza wapi, kwa vitu gani Dobe mie nilivyokuwa navyo hata nipangiwe nyumba nzima.
“Sharti gani hilo?!”
Ninamuuliza meneja huku ninamtazama usoni mwake, hasira zimenijaa ila ninakuwa mpole kwani nikiwakumbuka wale watu walionileta wamejaa vifua kama nini, ninaona hapa nikijidai ubishi wanaweza Kunifula Kayaya.
“Dobe jambo langu unalijua, mie katika umri wangu wote sijawahi kukojozwa na Mwanaume, hivyo niliiweka nadhiri kuwa siku ikitokea nikampata mwanaume wakunikaza mie na ubaya wangu huu, nikakojoa basi nitataka mwanaume huyo awe mume wangu kwa gharama zozote, tena awe mume wangu peke yangu siyo wa shirika! Upo hapo, sasa amua kusuka au kunyoa?!”
Meneja ananambia maneno hayo uso wa Mbuzi hana masihala hata kidogo.
“Kama unataka hivyo basi ninaomba nikampeleke Baby hospitali kisha nitahamia hapa bila ya shida.”
Ninamdanganya ili nipate nafasi yakuwa huru na pia nijue hali ya Baby kwani anaweza kufa kisa mie kumwambia Nge! Lakini pia amenionesha mapenzi makubwa sana. Nilipo sina simu hata namna yakufanya mawasiliano nao kujua wanaendeleaje pia sina.
“Dobe nisikilize kwa makini sana. Huyo unaemwita Baby yule mtu mzima hovyo leo hii ninataka afilie mbali. Kwani yeye ndiyo kikwazo kwangu, na ninakuhakikishia ninamuondosha katika dunia hii, kwani najua atanitangaza tu!”
Meneja ananambia maneno hayo huku akiwa amechukia sana. Nikiwa nipo katika kuchanganyikiwa kwa maneno ya Meneja wangu, ninauona mlango unafunguliwa na mara anaingia mtu ambae hakika moyo wangu unapiga sarakasi ya Shufani kwa fadhaa!!!
HAYA MZIGO UNAMPELEKA DOBE PABAYA! NINI KITAENDELEA? TEMBELEA KESHO MUDA ULELE BILA KUPUNGUA SEKUNDE HATA MOJA.


Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: