“Dokta haya maswali yenu ya namna hii ndiyo mnawafanya watu wafe kwa presha nyie. Sasa nikiambiwa mzima nifanyeje kama sikufurahia kuwa nimesalimika?! Na ukinambia nimeukwaa ni lazima nitahuzunika, hakuna mtu anaepima virusi vya Ukimwi, kisha aambiwe ameambukizwa akafurahi au akaweka Rusha Roho (KIGODORO) nyumbani kwake, nambie tu nijue moja. Maana unanichosha kabla hata ya majibu”
Ninamwambia huyu Dokta huku mapigo ya moyo yananienda mbio kinoma wahaka umenizonga, mashaka yamenijaa! Jasho linanitoka kama maji. Kifupi sina amani kabisa. Kupima siyo kazi mjamani, bali unapopokea vipimo ndiyo utaijua Junjunlai!
“Haya nimekusikia Dobe, sasa kipimo kinaonesha wewe……!”
Dokta anakatishwa kumalizia kunambia majibu yamgu na mtu anaefika hapa huku akinikenulia meno yake.
Moyo wangu unastuka ninapomuona, damu inatembea kwa kasi katika mishipa yangu. Inanizidisha jasho kunimwaika.
“Dokta anaendeleaje Dobe kwa sasa, keshakuwa vizuri?”
Dokta ananigeukia mie huku akiacha kunimalizia kipimo changu, anamjibu yeye.
“Mungu ni mwema kwa kweli. Ametupa ushindi na Dobe anaendelea vizuri sana”
Anasema maneno hayo kisha ananambia.
“Dobe huyu ndiyo aliekulipia gharama za matibabu yako“
Ninabaki kinywa wazi kabisa. Huyu ndiyo aliyonilipia?!!!
14
Ninamuona mlipaji na mfadhili wangu anatabasamu.
“Asante sana Jesca kwa mchango wako wa hali na mali.”
Ninamwambia mfadhili wangu nae anainama kupokea shukurani hiyo.
“Pole sana Dobe, ninakusubiri ili tuondoke sote nyumbani ukapumzike.”
Jesca ananambia maneno hayo huku anatabasamu.
“Asante ila ninaomba falagha kidogo ninamaongezi na Dokta.”
Dokta nae anamthibitishia hilo la falagha. Jesca au SHEMALE anatoka nje ya wodi, huku akiwa na wingi wa kujiamini.
“Dokta sasa naomba unambie hayo majibu tafadhali usinizungushe tena, wakaja watu wengine.”
Ninamwambia Dokta huku nimemkazia macho kwelikweli.
“Dobe punguza wahaka kwani nilikuwa nakueleza ila yule mfadhili wako akaingilia kati hivyo nikashindwa kutoa majibu mbele yake. Natambua majibu ya VVU ni siri ya mpimaji na anaempima.”
Dokta anasema maneno hayo kisha anainamisha macho yake kukitazama kipimo, alichokuwa nacho mkononi mwake, kisha ananigeuzia macho yake nami ninamtazama kwa makini.
“Dobe kipimo chako kinavyosoma hapa, inaonekana hujaathirika bado. Ila kitu cha kuzingatia hapa ni kwamba. Ikiwa umepata maambukizi katika siku mbili, au tatu nyuma, huwezi kuonekana katika kipimo kuwa umeathirika. Ila ninakushauri ukae kutoka tarehe ya leo uliopima hadi upate miezi mitatu upime tena. Ikiwa hapo hutoonekana umeathirika basi tunasema utakuwa upo salama. Ingawa unashauriwa pia katika kipindi hiki cha mpito upime mara tatu kwa uhakika zaidi, lakini ujichunge na ngono zembe.”
Dokta anaponipa majibu, mwili wangu unarowana zaidi na jasho, kama nimekoga na nguo!
Kweli mie mzima?! Kuanzia leo na siku zijazo, sitaki tena kukaza iwe mbele au nyuma. Ninaacha kabisa.
Ninajisemea kimoyomoyo huku nikiuona mwili wangu unapata nguvu kubwa sana. Ninayatafakari maneno ya Dokta kisha ninamgeukia.
“Dokta samahani sana, ninaomba nichome sindano uniuwe mkuyati wangu usiwe na nguvu tena!”
Ninamwambia kwa dhati, kwani inaweza kuniangaaza, kisha ikanipa mashaka bure.
“Sikia Dobe. Usifanye jambo hilo hata mara moja katika maisha yako. Uanaume wa mtu ni uume imara wenye nguvu. Unapotaka kujichoma sindano kisha utafanyaje ikiwa Mungu atakupa maisha marefu, si utadhalilika bure? Lakini ninakushauri kabla hujafikiria mara mbili jambo hilo, basi ungoje miezi mitatu ipite ili upime tena. Majibu ya baada kipimo hicho ndiyo yatakupa muelekeo.”
Furaha imenijia katika nafsi yangu sana kwani moyo wangu ulikuwa tayari ushanyong’onyea.
“Dokta naomba simu yangu na ruhusa, nishapona mie.”
Dokta anatabasamu kisha ananambia. Subiri nikuandikie ruhusa na simu yako nitakukabidhi utakapokuwa unaondoka.”
Dokta ananambia maneno hayo kisha anapiga hatua anakwenda ofisini kwake. Hakika amefanya hekima sana kubakia na simu yangu, lau angelikuwa ameshanikabidhi nisingengoja hiyo ruhusa yenyewe ningesepa tu.
Ninamuona SHEMALE jesca anaingia huku macho yake ameyatizamisha mahala nilipo. Anatembea kwa kujiamini hadi ananifikia nilipo.
“Dobe pole sana, nilikupigia simu leo akaipokea kijana mmoja akanambia mwenye simu umepata matatizo umeanguka, hivyo umeletwa hapa ndiyo nikaja lakini namna niliyokuona nayo mwanzo, nikatambua hakika ulikuwa unaumwa sana. Kwani nilishangaa kuwa ulikuwa ukinikataa kuwa hunitambui. Ila madakitari nilipokwenda kuwaeleza hali yako wakakupa huduma bora baada yakuwaambia gharama zote za matibabu nitatoa mie, wakanitaka nitoe kabisa nami sikusita kufanya hivyo.”
“Jesca asante sana kwa mara nyingine kwa msaada wako. Haya uliponipigia simu bila shaka ulikuwa na jambo ulilonitafuta nalo, je umeshanipata sasa niambie.”
Ninamuona Jesca akitabasamu kama kawaida yake.
“Dobe ulinambia unajifikiria hivyo nikakupigia simu ili nijue ulipofikia kwani nafasi ya kazi ninayotaka kukupa, ina watu wengi wanayoitaka. Hivyo nisingependa unijibie hapa laa, ningependa unijibu tukitoka hapa tukifika nyumbani.”
SHEMALE amekaza nami ninajua anachotaka ila amechelewa sana. Sasa hivi sitaki tena kuwa kama awali, nishakoma kabisa. Hata kama nipewe nini sitaki tena.
“Sawa nimekusikia. Ila nitaomba tukaongelee nyumbani kwangu kwani sijui hata kupoje tangu nilipoondoka. Mama mwenye nyumba wangu amefariki nawao ndiyo walionisababishia haya hadi nikawa hapa.”
SHEMALE ninapomwambia maneno hayo, ninamuona anabadilika sura na kuwa mtu aliechukia, japo hakupenda kunionesha machoni.
“Sawa Dobe nimekuelewa hakuna neno nitafanya utakavyo ili uwe na amani.”
Ninafarijika kwa kukubaliana na mawazo yangu.
Dokta anawasili ananipa cheti changu na dawa za kwenda kutumia ili afya yangu izidi kutengemaa. Ananipa simu yangu kisha ananipa mkono na kuagana nami. Ninageuka ninashika njia kuelekea nje ya wadi ya wagonjwa. SHEMALE Jesca hachezi mbali namimi, ninamuona anaunga tela kwa karibu kabisa.
Ninatoka hadi nje ya jengo, Jesca ananielekeza gari yake alipoiegesha ninamfata na tunapoifikia gari yake, anatoa lock za milango tunafungua milango na kuingia ndani. Jesca anawasha gari tunaanza safari kuelekea Tabata Segerea.
Mwendo wa kimya kimya ndani ya gari hakuna mwenye kumsemesha mwenzake.
“Jesca washa radio basi kwani naona ni kimya tu kama tunawenda kuzika.”
Ninaanzisha mazungumzo na yeye hanijibu bali anafanya vitendo anawasha radio kwa sauti ya wastani, kisha macho yake mbele anaendesha kwa umakini kabisa. Tunakwenda katika mwendo huo hadi tunafika Tabata Segerea nyumbani kwangu. Lakini ninapoukaribia mlango wa nyumba, ninapigwa na butwaa. Mlango umefungwa umetiwa kufuli kubwa kuonesha hakuna kuingia mtu tena humu ndani!
“Haya Dobe fungua mlango tuingie ndani tuzungumze.”
Jesca ananambia maneno hayo kama haoni kuwa mlango umefungwa na kufuli na mie sina funguo yake. Ninajiuliza ninaishishe sasa. Sijui msiba ulipo, lakini hata kama imeamriwa nyumba ifungwe sawa sina ubishi juu ya hilo lakini kuna vitu vyangu. pamoja na nguo ninazipataje?”
Ninawaza sipati jibu la maswali haya.
“Dobe vipi tena mbona tunaganda nje tu, kulikoni au umesahau ufunguo wako?”
Ninamtazama kisha ninautazama mlango kwa kukata tama
“Mie wakati nimeondoshwa hapa sikuwa na fahamu. Hivyo sitambui funguo ya kufuli hii ilipo, lakini pia mlango huu huwa haufungwi na kufuli!”
Ninamjibu Jesca aliekuwa anataka kunitia ujinga kwa kumuweka nje.
“Ok kwa hiyo unakubaliana na mimi sasa kuwa tukazungumzie nyumbani au bado unataka kuzungumzia kwako?”
Ninatafakari kwa kina kisha ninajiuliza ikiwa nitaendelea kukataa kwenda kwa Jesca na hapa ndiyo mlango ushatiwa kufuli nitakuwa mgeni wa nani? Lakini pia maisha bila kazi nitaishije. Ninapofikiria hivyo ninajikuta ninakubaliana na Jesca kwenda nae nyumbani kwake kwa shingo upande.
“Usiwe na wasi Dobe, kwangu pia ukitaka kulala nina vyumba vya kutosha, ikiwa hapa hutofunguliwa tena mlango sawa?
“Sawa.”
Jesca anafurahi hadi jino la mwisho, huku akitangulia kwenda kwenye gari. Nami ninamfata kwa karibu. Mie sipendi kabisa kwenda kwake lakini ninafanyaje, kwani sasa nimekuwa wakuogopwa kama ukoma!
Jesca anaingia garini kisha ananifungulia mlango niingie nami ninajiachia kwenye gari yake habari sipati. Jesca anaendesha gari tunatokomea hadi katika wilaya ya Kinondoni, Nyumbani kwake anapiga honi geti linafunguliwa anaingiza gari hadi ndani. Tunapofika ninapitishwa moja kwa moja hadi chumbani kwake, ninafikishiwa kitandani!
“Dobe punguza nguo zako kusudi zisijikunje, upumzike kwanza nifanye maarifa ya chakula tule kabisa kisha tutaanza mazungumzo yetu.
Ninamjibu sawa kisha Jesca ananiletea Khanga nivae ili kunusuru nguo zangu zisikunjike. Kwa adha ya Khanga ilivyonisibu, inabaki kidogo tu nikatae kuivaa!
Ninazivua nguo zangu, ninavaa Khanga, kisha ninajibwaga kitandani . Jesca anachukua nguo zangu anatoka nazo nje.
“Muda unakwenda, sasa hivi itaingia magharibi.”
Ninamwambia Jesca ili ahimize hicho chakula.
“Usiwe na wasi bwana Dobe utakula sasa hivi.”
Ninakuwa mpole ninasubiri chakula kwani utumbo sasa ninausikia kuwa unadai amana yake.
Ninaiwasha simu yangu kutazama ujumbe wowote kama umetumwa, lakini naona simu haina jipya.
Jesca anabeba nguo zangu anaondoka nazo nami simfatilii ninajilaza tu kitandani bila kujua ameelekea wapi katika hiki chumba chake chenye choo ndani.
Baada ya dakika kama ishirini na tano hivi Jesca anaingia na chakula anaweka chumbani kwenye meza ndogo.
“Haya ulilalamika njaa chakula hichi hapa ushindwe mwenyewe.”
Nitamtazama Jesca kisha ninatabasamu kichovu.
“Asante sana kwani wadudu wa njaa wananitakua siyo mchezo.”
Ananinawisha maji kisha ananipa chakula katika sahani, ninaanza kula kwa haraka kwani hali mbaya sana tumboni. Ladha ya chakula ninachokula hakiingii katika chakula cha Baby girl hata robo! Ninakula nifanyeje nisije kufa kwa njaa.
Jasho linanitoka kwa wingi, ninamaliza kula ninaingia msalani ninashindwa kuyaamini macho yangu kwa kitu ninachokiona!
Nguo zangu jesca amezitia kwenye beseni la maji, ameweka na sabuni ya unga juu zimerowana ndembendembe!
Ninazihakiki kama ndizo nguo zangu hasa, ninazitambua ndizo. Ninashindwa kwenda haja ninatoka ninamkuta akiondosha vyombo.
“Jesca sasa ndiyo umefanya nini? Mbona nguo zangu umeziroweka tena wakati mwenzako sina nguo za kuvaa zaidi ya zile?”
Anatabasamu kijinga!
“Nisamehe mpenzi kwa kuziweka nguo zako katika hali ya kuziandaa kuzifua. Nguo zilikuwa na vumbi kama nini, huwezi kuwa na mie kisha uwe mchafu Dobe.”
Nikiwa ninatafakari kuhusu nguo zangu, mara mlango wa chumbani unabishwa hodi. Jesca anainuka kwenda kumsikiliza anaegonga mlango nami ninaingia chooni kujihifadhi lakini pia kufanya haja zangu.
“Ohooo karibu shoga yangu, karibu sana. Mbona umepotea hivi jamani kwema?”
“ Kwema Shoga. Kabla sijakuzungumza kilichonileta acha kwanza niende chooni kujisaidia kwani kojo limenibana saa nyingi kweli!”
Sauti hiyo ninaisikia kwa fasaha, mwili wangu unapata ganzi. Ninakuwa na hasira sana ninawaza akiniharibia hapa na nguo zangu zisharowekwa kwenye maji, nikitimuliwa nitatoka vipi?! Kichwa kinauma kwa mawazo. Huyu amefata nini huku? Ninajiuliza.
Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
0 comments:
Post a Comment