CHOMBEZO; HEHEEE, KANTANGAZEEE!!! SEHEMU YA 22



“ Kwema Shoga. Kabla sijakuzungumza kilichonileta acha kwanza niende chooni kujisaidia kwani kojo limenibana saa nyingi kweli!”
Sauti hiyo ninaisikia kwa fasaha, mwili wangu unapata ganzi. Ninakuwa na hasira sana ninawaza akiniharibia hapa na nguo zangu zisharowekwa kwenye maji, nikitimuliwa nitatoka vipi?! Kichwa kinauma kwa mawazo. Huyu amefata nini huku? Ninajiuliza.
“Msalani kuna mtu shost fanya subira kidogo.”
Ninamsikia Jesca akimwambia Njasi maneno hayo, nami ninasikiliza maneno yao, haja imeniruka imekwenda mbali nami kwani huyu keshakuwa siyo mtu mzuri kwangu.
“Hee?! Makubwa haya shost! Choo chako umuingize mgeni kwani choo cha wote hukumuonesha? Au mchuchu huyo Jesca?!”
“Haloooow, Kanchomekee!!! Chezea mie wewe utalala hoi!”
Jesca ninamsikia akicheka cheko la kedi, nami ninazidi kuvutika na mazungumzo yao. Umbea umenishika Siendi haja kubwa, wala ndogo. Nimebaki chooni kama mende!
“Sasa kama ndiyo mchuchu yupo chooni, basi mie nakwenda zangu shost, nikuache upige show yako kwa utuo.”
Njasi anamwambia Jesca nami ninaombea aruhusiwe tu ende zake kwani akikaa huyu chango mzaa maradhi ataniharibia tu. Anaweza kusababisha nikaondoshwa na Khanga tena huyu!
“Hapana shost, huwezi kuondoka hivyo juu juu, kama nywele za kichwani, nipe huo ubuyu kwanza kisha umsalimie shemeji yako, ndiyo wende zako. Mtu umeniacha kwenye Taharuki, kisha utaondokaje uniache ninaning’inia bure. Mwenzako ukimtia nyege ni budi ummalizie kabisa!”
Ninamlaani Jesca kama nini! Sasa anisalimie mie ili iweje?! Huyo Njasi siku hizi ni nuksi tu, amegeuka Mung’unye aharibikia ukubwani! mwache apige bunda bwana aaah atazingua tu huyo! Ninajisemea kimoyomoyo chooni, haja sina kabisa imekimbia.
“Shost mbona nimeyakanyaga mwenzako?! Nimejitia utaalazi wa kupiga show na mtu muathirika, nika shere nae mkuyati, kumbe shost ninajiingiza katika Mkenge! Huyo bwana mwenzangu ni fundi wa Matentelee lakini mmmmh sina amani hapa nilipo nina mashaka utasema nadaiwa na Kijumbe!”
Njasi keshaanza yake sasa! Nikimuacha hadi amalizie story yake hapa ninatolewa Dima na Khanga kama siyo uchi kabisa! Maana hii siyo Kantangazee tena naona itakuwa ni Kanchomekee!
“Hehee Shost usinambie, nani huyo kwani?!”
Jesca anapofika hapo uzalendo wa kukaa chooni tu kusikilizia ubuyu, unanishinda ninaamua kujichanganya, ili japo Njasi aone haya kwa vile uso umeumbwa na haya, asimalizie kusema mineno yake ya falaka!
Ninatoka chooni huku ninajifanya kujikohoza kwa nguvu, ili niwateke wanyamaze kuzungumza habari zangu na za Baby wangu. Alietangulia mbele ya haki ambae sitomsahau maishani mwangu.
Ninamuona Njasi akigeuza sura yake haraka kwangu nilipo ili aonane na huyo mchuchu wa Jesca, uso wake na wangu unakutana macho yake ninayaona yanatahayari!
“Haya nenda kwanza chooni, shem wako keshatoka kisha unimalizie ubuyu wangu.”
Jesca anamwambia, lakini Njasi bado alikuwa amepigwa na butwaa kwani Khanga anayoniona nayo hapa, siyo aliyonishuhudia nikiondoka nayo kutoka kule kwa Qeenlyn. Hivyo akili yake bila shaka inamwambia nishacheza show sana hapa!
“Shost huyu ndiyo mchuchu mwenyewe?!”
Njasi anamuuliza Jesca kwa mshangao, huku akiyaangaza macho yake huku na kule.
“Naam shost humkumbuki huyu wewe, anaitwa Dobe alikuwa pale katika Massage Sinza, kijana amenikaa rohoni huyu, kila siku nakumbuka mambo yake.”
“Mmmmh”
Ninamsikia Njasi akiguna kisha anashusha pumzi nzito.
“Shost ninaomba nisindikize tu mara moja, kwani huo mkojo wenyewe ushaniruka kabisa. Hapa nipo sawa ila ukiuma nitapiga hodi nyumba yoyote ili nijistiri.”
Ninaumiza kichwa mara moja, ninaona Njasi anataka kwenda kunimaliza akiwa peke yake na Jesca, wakati akisindikizwa.
“Heeeh! Njasi ulinambia mkojo umekubana saa nyingi na ulipofika hapa tu ukataka wende chooni, sasa kimekusibu nini hata iwe huna tena haja?!”
Jesca anaposema maneno hayo, kabla ya Njasi hajajibu lolote ninadakia.
“Jesca my love, tunamsindikiza wote mgeni haachwi mtu hapa!!!”
Ninamuona Njasi ananitazama kwa kuninyali, yaani ananiona kama vile ninasambaza VVU, angejua mwenzake nipo safi mbona na yeye angeyataka Matentelee? Kumbe Binaadamu anakuthamini ukiwa mzima na kumtimizia haja zake, ila unapopatwa na matatizo tu wanakutenga! Ama kweli kila mchuma janga hula na wakwao.
“Dobe ninakutangaza sasa hivi, tena ukome tabia yako hiyo nakwambia!”
Ninamtazama kwa dharau, ninatambua anataka kunitangaza kuwa nishaungua, ama kweli jambo usilolijua ni sawa na usiku wa kiza.
“Heee?! Umtangazee tena, amefanya nini? Hebu nambie shoga yangu, kwani ninaona kama una kitu ambacho unakificha vile. Nikiunganisha matukio tangu ulipokuja hapa ukiwa na furaha, na sasa ulivyobadilika hasa baada ya kumuona Dobe, tafadhali niambie nini kinachoendelea?! Ni sababu gani hasa iliyokuleta kwangu?!”
Jesca anamgeuka Njasi, nami ninataka kumkomesha pia maana amenidhalilisha vyakutosha. Japo sina ubishi Njasi ni mzuri wa umbo na mambo, lakini kila kizuri hakikosi kasoro, na kasoro yake ndiyo hii, ana dharau sana yaani.
“Jesca shoga yangu, naomba unisikilize kwa makini.”
Njasi anaposema maneno hayo ninaanza kumkemea kimya kimya ashindwe. Maana naona sasa anamwaga mboga, itabidi na mie nimwage ugali ili twende sawa.
“Nakusikiliza shoga yangu nambie, usinifiche chochote.”
Jesca ameshajaa upepo, anawahaka wa kujua hayo mambo.
“Labda nikuulize tu shost wangu, na naomba unambie ukweli. Dobe umeshatembea nae hata mara moja?”
“Bado shoga yangu.”
“Kama bado nakushauri achana nae, Dobe siyo mzima ni muathirika.”
Anaposema hivyo mie ninaangua kicheko kikubwa sana, huku sina wasiwasi kabisa. Jesca anashangaa sana.
“Ameathirika?!”
Jesca anamuuliza shoga yake. Mie ninaendelea kucheka kwa nguvu.
“Sasa wewe nae unacheka nini? Jambo la hatari wewe unachekelea?!”
Jesca ananiuliza kwa mshangao.
“Ndiyo ujue kuwa huyo si mzima, virusi aliyvokuwa navyo, bila shaka vishampanda kichwani ameshadata!”
Njasi anasema maneno hayo, lakini hajui mwenzake ninamfanya yeye aonekane kama anaetia fitina vile.
“Hebu nambie maana ushanichanganya shost huyu anaumwa nini?! Yaani ameathirika na VVU? Wewe umemjuaje?”
Jesca anamuuliza Njasi, nami sasa ninakaa kimya nisije kufikirika nimedata kama kule hospitali bure.
“Nilipokuja hapa, nilikwambia kuwa nimeshere mkuyati na muathirika? Basi mkuyati wenyewe ni wa huyu bwana. Mwanamtama ameathirika na VVU anakula dawa na mumewe ameshakufa kwa Ukimwi, na hivi ninavyoongea na wewe huyo Mwanamtama nimepata habari nyepesinyepesi kuwa ameshafariki dunia. Hivyo Dobe kwa kuwa ndiyo alikuwa mpenzi wake, ninahisi sote mie na Dobe tumeathirika. Nakupenda shoga yangu, ndiyo maana ninakutakia mema. Kama utaona ninakuzibia rizki yako, haya endelea ila utakuja kunikumbuka.”
Njasi anamalizia nukta yake ya mwisho ya kuharibu, nami ninatabasamu kwa kujiamini kabisa.
“Mmmmh makubwa haya sasa, Dobe kuna ukweli wa maneno haya?!”
Jesca ananiuliza huku amenikazia macho.
“Jesca hayo ni maneno ya mkosaji anayoyasema shoga yako. Mie ni mzima kama chuma sina virusi nipo tayari twende hospitali yoyote unayoijua wewe, na kuiamini kwa vipimo vyao ili tukapime sote humu ndani. Huyo amekuuliza wewe kama umeshatembea na mie, Je?! wewe una Uke wakutembea nami?! Huyu ni fitina anaumia kwa nini mie nifanye show na wewe! Kwani ndiyo chaguo langu, wanawake nimeshafanya nao show wengi tu. Ila mtu wa namna yako, ni shida sana kukutana nae, huyo amejaa wivu tu.”
Ninaamua na mie kumgeuka kwani ninachelea kutolewa dima na Khanga, na kule kwa Baby kuna kufuli unadhani nitakuwa mgeni wa nani kama siyo kwenda kulala vituo vya basi. Na huu upande wa Khanga nao niliokuwa nao na baridi hili, itakuwaje? Na hao Mazabania utawaachia wapi, kama hawajataka kula Ashaakum nikilala?! Hapa hatoki mtu yaani ninapambana hadi hatua za mwisho.
“Njasi wewe umejuaje kama Dobe ameathirika?! Kwa sababu ametembea na muathirika au umepima nae?”
Njasi anakosa jibu la maana lenye msingi.
“Ok mie kwa bahati nzuri ninavipimo ndani kwangu. Nilipokuwa safari Marekani nilipata kuhudhuria semina moja ya SHEMALES nikapewa vipimo vingi tu, vingine nimegawa lakini vingine ninavyo hapa hapa ndani, mnaonaje sote tukapima tukaujua ukweli wa haya?!”
“Safi sana tufanye hivyo, kwani Njasi amenidhalilisha sana, ameshasababisha nitembee uchi huyu, keshanitangaza sana kuwa mie ninao, kama ulivyomsikia hapa. Naona leo utakuwa umekata mzizi wa fitina kabisa.”
Ninadakia kumwambia Jesca, ninamuona Njasi anarudi matawi ya chini kwa namna nilivyokuwa nimejiamini kupita kiasi. Jesca anafungua kabati lake anatoa bahasha kubwa katika droo la kabati, kisha anatoa vifaa vya kupimia VVU ambavyo havina tofauti kubwa sana na vile nilivyopimia leo hospitali.
“Ninaomba nianze mie kwanza kupimwa.”
Ninasema kwa kujiamini sana. Jesca anachukua spiriti anachukua pamba, anaichovya kwenye spiriti kisha ananisugua kidogo na hiyo pamba katika kidole cha kati, ananitoboa na sindano maalumu damu inatoka. Kisha damu yangu anaikinga katika hicho kifaa cha kupimia, matone kadhaa yanadondokea hapo. Jesca anatoa ufafanuzi wa namna ya kuelewa matokeo ili sote tuone kwa macho yetu.
“Hichi kifaa baada ya dadika mbili tu, kitakuwa kimeshaisoma damu hii, na ikiwa imeiona haina maambukizi itachora mstari mmoja mwekundu hapo mbele, na kama ikiwa na maambukizi itachora mistari miwili hapo hapo.”
Jesca aliposema maneno hayo, anakiweka hichi kifaa katika meza ya kioo iliyokuwa hapa chumbani, kifaa kinakaa sawa na mie ananipa pamba niweke katika kidole changu ili kukata damu isitoke zaidi. Macho sita yanakitazama hichi kifaa huku tukiwa kimya kabisa, mara mstari mmoja mwekundu unachora katika kifaa hiki! Ninainua uso wangu ninamtazama Njasi, ninamuona anatahayari anakuwa hana amani kama mtu aliefumaniwa.
“Haya kantangazee sasa kama sina VVU, siyo unitangazee kuwa ninavyo tu, ukatangaze na hili la kupima mbele yako pia!”
Ninamwambia Njasi ambae anakuwa hana neno, maneno yote yamemkauka kabisa kinywani mwake. Jesca ananibusu busu zito mbele ya Njasi.
Mmmmmwaaaaaaaaaaaaaah Mie ninamtazama Njasi kwa jicho la husuda.
“Haya zamu yako Njasi upime na wewe mbele yetu, kwani usiwe hodari kutangaza ya watu tu, na wewe pia tukutambue tukatangazane vizuri.”
Ninamwambia Njasi, huku nikiwa na furaha na najiamini sana, kuwa japo hapa kwa vipimo hivi siwezi kuondoka na Khanga, hivyo kwa hilo tu ninajiamini.
“Haya shost unahukumu kwa macho kisa tu kuna mtu ameambukizwa basi na wewe unaona mwengine aliekuwa nae atakuwa nao, VVU havipo hivyo. Wapo watu mke na mume wanaishi mmoja ana virusi vya VVU na mwengine hana kabisa, na wanafanya mambo yote ya ndani ya kuta 4. Ila ni muhimu tu mkishajitambua kuwa mmoja ni muathirika, mvae kinga ili msiambukizane”
Njasi anasogea apime lakini ninamuona anabadilika uso wake, mapigo ya moyo yanamuenda mbio kama mshale unaosababisha sekunde! Jesca anamtoboa na kukinga damu yake katika kile kifaa, kisha kama ilivyokuwa kwangu sote tunatazama kipimo hiki kwa makini. Mara baada yakusomwa kwa kipimo macho yetu yanashuhudia kipimo kile kikileta majibu, Ninamtazama Njasi usoni, ninamuona machozi yanamtoka!!!

ITAENDELEA KESHO KATIKA MUDA WAKE






Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: