Mkufunzi wa PETS Bw,John Makolokolo Akiendelea Kutoa Darasa kwa wajumbe wa PETS Kijiji cha Ludewa Mjini |
Baadhi ya Wajumbe wa PETS wakiendelea Kufuatilia Somo kutoka kwa Mkufunzi wa PETS Ludewa mjini |
Bw, John Makolokolo Akitoa Darasa kwa Washirikiwa PETS |
Na Maiko Luoga LUDEWA
Viongozi wa Serikali wilayani Ludewa mkoani Njombe wametakiwa kuwa wawazi na waaminifu kwa wananchi wanaowaongoza katika maeneo yao kwakuweka bayana Pesa za miradi zinazoingia katika Vijiji Au kata husika.
Wito huo ulitolewa leo November 27 na Mwenyekiti wa Mfumo wa Ufuatiliaji wa Rasilimali za Umma Kuanzia zinapotoka hadi zinapoishia Maarufu kwa jina la Pets kutoka Makao makuu ya Mfumo huo jijini Dar es laam Bw, John Makolokolo wakati akizungumza na Baadhi ya viongozi wa Kijiji cha Ludewa mjini.
Alisema Maranyingi Serikali imekuwa ikitoa pesa kwaajili ya wananchi wa vijiji husika lakini baadhi ya viongozi ambao si waaminifu wamekuwa wakizitumia pesa hizo kwa masilahi yao binafsi bila kutoa taarifa za mapato na matumizi ya pesa hizo na kuishia kuzua migogoro kati ya Viongozi hao na wananchi wanaowaongoza.
Katika mkutano wa kijiji cha Ludewa mjini uliofanyika siku ya leo November 27 mwaka huu 2017 licha ya viongozi wa kijiji na kata kutoa mrejesho wa mambo yaliyojadiliwa katika mkutano uliopita pia wananchi wa Ludewa Mjini wamechagua kamati ya PETS kama Mfumo wa Ufuatiliaji wa Rasilimali za Umma Kuanzia zinapotoka hadi zinapoishia.
Kamati hiyo ambayo itakuwa na kazi kubwa ya kufuatilia na kuhoji mwenendo wa Miradi mbalimbali inayoendelea katika Kijiji cha Ludewa Mjini na baada ya Kuchaguliwa wajumbe hao wakazungumza na Uongozi wa PETS wakiwaahidi wananchi Wa kijiji cha Ludewa Mjini kuwa watafanya kazi ya kufuatilia miradi ya serikali ndani ya kijiji chao Bila wasiwasi na hofu yeyote.
Katika hatua Nyingine Diwani wa kata ya Ludewa Mh,Bi, Monica Mchilo Akizungumza na mtandao huu alisema kuwa Mkutano wawananchi wa kijiji cha Ludewa mjini uliofanyika siku chache zilizopita uliazimia kuwa viongozi wa kijiji na kata ya Ludewa watoe maelezo ya uhakika juu ya Pesa iliyotozwa kwa wananchi ikitajwa kama pesa ya Usumbufu.
Wananchi ambao walikuwa wanakamatwa na mgambo wa kata ya Ludewa kwakosa la kutotoa mchango wa ujenzi wa Mabweni katika Shule ya sekondari Chief Kidulile Ludewa mjini walitakiwa kulipa kiasi cha Tsh,10,000 ambapo kiasi cha Tsh, 5000 walilipwa mgambo na 5000 nyingine iliingia kwa mtendaji wa kijiji Cha Ludewa Mjini kama pesa ya Usumbufu Bila kutoa risiti kwa wananchi hao.
Baada ya Malalamiko hayo ya wananchi Diwani wa kata ya Ludewa Bi, Monica Mchilo alilazimika kufuatilia utaratibu wa mchango huo wa pesa ya Usumbufu kwa mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa Bw, Ndatwa Ludigija na kubaini kuwa mchango huo ulikuwa batili hivyo Jumla ya kiasi cha Tsh, 460,000 imerejeshwa kwa wananchi ambao kwapamoja walikubaliana kuwa pesa hiyo ikatumike katika ujenzi wa Mabweni katika shule ya Sekondari Chief Kidulile.
Hatahivyo Diwani huyo Alitoa wito kwa viongozi wanaochukua michango kwa wananchi kuhakikisha kuwa wanatoa Risiti na wananchi pia wahakikishe kuwa wanadai Risiti ili kuweza kuwabaini Viongozi ambao si Waaminifu katika kata ya Ludewa Mkoani Njombe.
Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
0 comments:
Post a Comment