Vikwazo vyaanza kuwekwa kwa wachezaji wa kimataifa kwenda China.



Kwa miaka ya hivi karibuni ligi ya mpira wa miguu nchini China imekuwa gumzo.Ligi hiyo imekuwa gumzo kutokana na pesa nyingi zinazotumika kujenga timu zao.Zamani tulikuwa tunaona wachezaji waendao China ni wale waliochoka lakini siku za karibuni mambo yamebadilika.Wachina wamekuwa wakichukua mchezaji yeyote wamtakae kwa hela kubwa sana.Hali hii imepelekea wachezaji wengi Ulaya kuanza kuzitolea mate pesa za China.
Matumizi makubwa ya pesa katika soka lao yameleta majina makubwa katika mpira wao.Si ajabu kuona majina ya Manuel Pellegrini,Andre Villas Boas wachezaji kama Gervinho,Hulk,Asamoah Gyan wakiwa katika ligi hiyo.Hii yote imetokana na uwekezaji mkubwa katika ligi yao.Carlos Teves ameenda China na kuwa mchezaji anayelipwa zaidi duniani akilipwa £615,000 kwa wiki katika timu ya Dhanghai Dhenhua.Huku pia Oscar akienda Shanghai SIPG.
Wachina wananunua tu wachezaji kutoka nje ya China haswa kutoka America ya Kaskazini.Kila kukicha wanazidi kuhusishwa na kuleta wachezaji wapya kutoka ligi mbalimbali duniani.Klabu za China zinazidi kuhusishwa na usajili wa wachezaji wakubwa,wiki hii wakitajwa kuwa katika mbio za kumpeleka Costa katika ligi yao.
Utitiri huu wa wachezaji wanaoingia China umewafanya wachezaji wanaotokea China thamani yao kushuka.Na sasa China wameamua kuweka sheria inayovibana vilabu vya nchini mwao kuhusu wachezaji wa kutoka nje.China wamefikia uamuzi huu ili kudhizibiti timu zao katika masuala ya utumiaji fedha na pia kuweza kujaribu kuleta heshima kwa wachezaji wao wa ndani.
China wameamua kuijenga timu yao ya taifa,na kutokana na sheria hii baasi wachezaji wengi wazawa watapata nafasi ya kuzichezea timu za China.Matajiri Wakichina wamekuwa wanaingiza tu nchini humo wachezaji ambao sio wazawa wa China.Hali hii inawakosesha namba wachezaji wazawa kwani wengi wa wanaokuja ni bora kuliko wao.
Si hivyo tu bali wachezaji vijana kutoka katika vilabu vya nchini humo wanakosa nafasi katika timu za wakubwa hivyo kuhatarisha vipaji vyao na soka la taifa lao.
Katika kikao kilichofanyika wikiendi iliyopita,kamati ya ligi kuu ya China imeamua kuanzia sasa timu za nchi hiyo zitakuwa zinasajili wachezaji wa nje watano tu.Kati ya wachezaji hao watano sio wote watakaocheza uwanjani bali kutacheza watatu tu.Chama cha China kimekuja kutoa tamko hili lengo lao kubwa likiwa ni kuimarisha timu yao ya taifa.
Chama cha soka vha China kinataka wachezaji kutoka timu za vijana wapewe nafasi.Na sasa kila timu itatakiwa kutumia wachezaji wa timu za vijana kuanzia wawili.China wameamua kuangalia soka la vijana ambalo ndio msingi haswa wa mpira.



Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: