Sanchez kuhukumiwa kwenda jela?



Screen Shot 2017-01-17 at 9.31.35 AM
Kesi za wachezaji haswa wa La Liga kukwepa kodi ni jambo la kawaida.Na hii inaonekana haswa kwa wachezaji wa Barcelona. Lioneil Messi na Mascherano ni moja kati ya wachezaji ambao siku za karibuni wamekumbana na kesi za namna hii. Messi alikumbwa na kashfa kubwa ya kukwepa kodi akienda mahakamani mara kadhaa. Hii ilikuwa kero kubwa kwa Lioneil kwani ilifikia hatua akaanza kuiona ligi ya Hispania kuwa chungu na kuanza kuhusishwa kuhama.
Alexis Sanchez naye ameingia kwenye mlolongo huu. Kupitia video Sanchez amekiri mahakamani Hispania kwamba alikwepa ukwepaji wa kodi wa kiasi cha £ 900,000 alipokuwa akiitumikia Barcelona. Sanchez amekiri kufanya kosa hilo kipindi akiwa Barca kabla ya kuja Uingereza kujiunga na Arsenal. Ukwepaji kodi unaonekanakasumba kwa wachezaji wanaotoka bara la America ya Kusini na pengine hii inachangiwa na aina ya maisha waliyopitia utotoni.
Inasemekana Sanchez mwenye miaka 28 alificha uhusiano wake na kampuni ya Numidia mwaka 2012. Kuficha uhusiano huko na Numidia kulimsaidia Sanchez kukwepa kulipa £ 516,190 na kukwepa tena £ 347,642 mwaka 2013.Japokuwa baadae Sanchez alilipa kiasi chote hicho.
Sasa Sanchez atatakiwa kulipa faini kubwa ili kutopata kesi kubwa zaidi. Mawakili wa Sanchez wanatarajia kukutana na mahakama Hispania kukubaliana kiasi cha faini ambayo inaonekana itakuwa kubwa kwa kuwa alichelewa kukiri kosa hilo. Sasa Sanchez atahukumiwa kwenda jela japokuwa kwa sheria za Hispania hukumu ya kifungo cha chini ya miaka miwili unatumikia ukiwa mtaani. Tayari Messi alihukumiwa miezi 21 huku Mascherano akihukumiwa mwaka. Sanchez ni mchezaji wa sita kutoka Barcelona kufanya kosa hili baada ya Lioneil Messi,Etoo,Javier Mascherano na Adriano kuwahi kufanya kosa kama hili huko nyuma.
Mwaka huu huenda ni wa majanga kwa Sanchez.Hali yake na timu yake ya sasa sio nzuri kwani wikeindi hii alichukizwa na kutolewa uwanjani zidi ya Swansea. Sanchez hadi sasa inasemekana yuko kwenye mvutano na Arsenal kuhusu mkataba wake mpya ambao hadi sasa hajasaini.



Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: