JE WAJUA? HUYU NDIYE MBWA TAJIRI KULIKO WOTE DUNIANI, ANA UTAJIRI WA KIASI CHA DOLA ZA KIMAREKANI 373 MILLION.


Pichani ni Mbwa anayeitwa Gunther VI aina ya German Shepherd ambaye ana utajiri wa kiasi cha dola za kimarekani Million 373.
Ni ajabu kusikia mbwa naye anakuwa katika orodha ya viumbe vyenye hela duniani japo kwa wenzetu nchi za magharibi hilo kwao ni jambo la kawaida sana, leo hii katika session ya Je wajua nimeona nikuletee huyu Mbwa ambaye anashika namba moja katika Mbwa ambao ni matajiri ambaye anakadiriwa kuwa na kiasi cha dola za kimarekani Million 373.
Vitabu vingi mbalimbali vimeandika kwamba Mbwa ni rafiki mkubwa wa mwanadamu ambapo hapa namzungumzi huyu mbwa tajiri duniani aitwaye Gunther VI, Mbwa huyo ambaye amepata urithi kutoka kwa baba yake aitwaye Gunther III’s ambaye ndiye alikuwa mrithi wa hela hizo.
Pichani ni Billionea Karlotta Liebenstein enzi za uhai wake akiwa na mmoja wa mnyama aliyekuwa akimpenda .
chanzo cha mbwa hawa kuweza kuingia katika rekodi ya dunia ni kutoka kwa mwanamama mmoja billionea mjerumani aliyekuwa akiitwa Karlotta Liebenstein ambaye alifariki mwaka wa 1991, inasemekana  alikuwa na mapendo sana na wanyama hivyo kabla ya kufa aliandika usiha kwa kila mnyama wake aliyekuwa akimfuga apewe  kiasi ambacho alichokisemkwa wanyama aliowapenda,  ambapo baba wa Gunther VI ndiye aliyeandikwa mrithi wa kiasi hicho cha hela nae haikupita muda akafa na kurithishwa hela zote Gunther VI.
Pia mbwa huyo anafanyiwa huduma za hali ya juu pamoja na kula vyakula vya hali ya juu ambavyo huwa hawali mbwa wengine, mbwa huyo Gunther anamiliki jumba kubwa na la kifahari jijini Miami Marekani ambalo jumba hilo linapakana na jumba la mkali wa miondoko ya pop mwanamama Lady Madona, Mbwa huyo ana gari yake maalu ya kutembelea na bwawa la kuogelea maarufu kama swimming pool. Hayo ndio mambo ya Dunia




Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: