WAKULIMA NJOMBE KUJIANDAA MAPEMA

NJOMBE

Wakati Wakulima Wakionekana Kukata Tamaa ya Kupatiwa Pembejeo za Ruzuku zaKilimo
Ambazo Zimekuwa Zikitolewa na Serikali Kwa Kila Mwaka Kutokana na Kucheleweshwa,
Hatimaye Mkoa wa Njombe Umetangaza Kugawa Jumla ya Mbolea ya Kupandia na Kukuzia
Tani 5304 Huku Mbegu Zikiwa Tani 530 Kwa Halmashauri Zote za Mkoa wa Njombe.

Pembejeo Hizo Zimetajwa Kwenda Kuwanufaisha Wakulima Ambao Si Watumishi wa Serikali
Wala Wakulima Wakubwa Bali Walengwa ni Wale Ambao Wataweza Kugharamia Bei ya
Pembejeo Ambazo Serikali Itachangia Asimilia 30.

Akitangaza Mgao Huo Katibu Tawala Sehemu za Uchumi na Sekta ya Uzalishaji Mkoa wa
Njombe Lameck Noah Amesema Pembejeo Hizo Kwa Mwaka Huu Hazitakuwa Kwa Mfumo wa
Vocha Bali Serikali Itatumia Kampuni ya Mbolea Tanzania TFC Pamoja na Kampuni ya

Mbegu na Wakala wa Mbegu wa Serikali ASA.

Bwana Noah Amesema Waraka wa Mgao wa Pembejeo Hizo  Umeshatumwa Katika Halmashauri

Zote za Mkoa wa Njombe Ambako Kamati Husika Zimeagizwa Kuketi Haraka Iwezekanavyo.



Katika Hatua Nyingine Amesema Kwa Wakulima Ambao Tayari Wameshapanda Hawapaswi
Kuendelea Kuilalamikia Serikali Kwa Kuchelewesha Pembejeo Hizo Kwani Ilikuwa

Inaangalia Utaratibu Rahisi wa Kuwafikishia Pembejeo Hizo Tofauti na Malalamiko

Ambayo Yamekuwa Yakiibuka Toka Kwa Mawakala.

Hata Hivyo Amewataka Wakulima Kuzitumia Pembejeo Hizo Vizuri Ikiwa ni Pamoja na

Kulima Kilimo Kinachoendana na Hali ya Hewa Kwani Katika Msimu Huu wa Kilimo

Mamlaka ya Hali Ya Hewa Nchini TMA Ilitangaza Kuwepo Kwa Mvua Chache Tofauti na

Miaka Mingine.




Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: