Kombe la Shirikisho: TP Mazembe yajiandalia fainali


mediaAdama Traore (kushoto), mshambuliaji wa TP Mazembe kutoka Mali akikabiliana na beki wa Tunisia wa Etoile Sportive du Sahel, Hamdi Naguez (kulia).SALAH HABIBI / AFP
TP Mazembe imetoka sare ya kufungana 1-1 na klabu ya Tunisia ya Etoile Sportive du Sahel kwenye Uwanja wa Olimpiki katika mji wa Sousse, nchini Tunisia, wakati wa mechi ya kwanza ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho.
TP Mazembe, klabu ambayo ilishinda mataji 15nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, imetoka sare ya kufungana 1-1 ikiwa ugenini nchini Tunisia dhidi ya Etoile Sportive du Sahel kwenye Uwanja wa Olimpiki katika mji wa Sousse katika mchuano wa kwanza wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho.
Mchezo bila mshindi
Mchezo huu kati ya timu hizi mbili ulikua ukisubiriwa kwa hamu na gamu. TP Mazembe imemaliza ya kwanza katika kundi A ikiwa na alama 13, wakati ambapo Etoile Sportive du Sahel ikimaliza ya pili katika kundi B ikiwa na alama 11, lakini klabu ya Tunisia kwa sasa inashikilia taji la ubingwa. Katika muda wa dakika 90, timu hizi mbili zilijaribu kupata kila mmoja kushambulia kambi ya mwengine bila mafanikio ya kutosha.
Etoile Sportive du Sahel ilikua ya kwanza kuona lango la TP Mazembe. Kiungo wa kati wa Tunisia Hamza Lahmar, katika dakika ya 19 ya mchezo, alifaulu kuweka mpira wavuni baada ya kipa Robert Kidiaba, mwenye umri wa miaka 40 kujikuta amefanya makosa.
TP Mazembe ilipata mafanikio, katika kipindi cha pili. Roger Assalé, mshambuliaji wa Cote d'Ivoire wa klabu DR Congo, alijikuta pekee yake katika eneo la hatari na kufaulu kuiifungia klabu yake bao la kusawazisha. Kipa Aymen Mathlouthi alitarajia kua mchezaji huyo wa TP Mazembe atato pasi.
Mchezo wa marudiano utapigwa Jumapili tarehe 25 Septemba katika mji wa Lubumbashi nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo. TP Mazembe ina matumaini ya kushinda na kufuzu katika fainali kutokana na bao ililofunga ugenini.
TP Mazembe imecheza michuano tisa ya fainali, ikiwa ni pamoja saba katika Ligi ya Mabingwa CAF, mchuano mmoja katika Kombe la Afrika la Washindi Kombe na mchuano mwengine wa Kombe la Shirikisho.



Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: