Somalia: afisa mwandamizi wa jeshi auawa mjini Mogadishu


mediaWanajeshi wa Somalia wakipiga kambi mbele ya hoteli ya Maka al-Mukarama ambayo ilishambuliwa na wapiganaji wa Al Shabab, mjini Mogadiscio, Machi 28, 2015.REUTERS/Feisal Omar
Afisa mwaandamizi na walinzi wake wanne wameuawa Jumapili hii Septemba 18 mjini Mogadishu, nchini Somalia katika shambulizi la kujitoa mhanga linalodaiwa na kundi la wanamgambo wa Kiislam la Al Shebab.
Gari "lililokua limejaa mabomu liligongana na lori la kijeshi kando ya barabara" na kusababisha vifo vya "askari wengi, ikiwa ni pamoja na afisa mwaandamizi mwenye cheo cha juu," kulingana na chanzo cha polisi.
Shambulizi hilo liliolomuua Jenerali Mohamed Jimale Goobaale na walinzi wake wanne lililotokea karibu na makao makuu ya jeshi.
Jimale alikuwa amenusurika majaribio mengi ya kumuua, ambayo yamekua yaliendeshwa na wanamgambo wa kundi la Al Shabab.
Wapiganaji wa kundi la Al Shabab wamekiri kutekeleza shambulizi hili wakisema kuwa jenerali huyo alikuwa akipanga na kutekeleza mashambulizi mengi dhidi yao.
Nchi ya Somalia imeendelea kukumbwa na mashambulizi mbalimbali yanayolenga wanajeshi, askari polisi na maafisa mbalimbali wa serikali



Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: