Nguruwe wawili mbele ya Bunge la Uganda, mjini Kampala, Juni 17 2014.AFP
Alhamisi hii nchini Uganda, wanaharakati wamepeleka nguruwe mbele ya Bunge la Uganda katika mji mkuu, Kampala, kupinga dhidi ya uamuzi uliyopitishwa wa kufidia wabunge nchini humo.
Ilibainika wiki hii kwamba fedha zilizotengwa katika bajeti ya taasisi hiyo ili kufidia gharama za mazishi kwa wabunge.
Takriban Dola elfu kumi na tano zimetengwa kwa kila mazishi.
Baadhi ya wabunge wametetea mpango huo.
Baadhi ya wabunge wamesema kwamba huduma ya mazishi ya askari waliokufa wakilihudumia taifa yanalipwa na serikali na kwamba wabunge wanapaswa kupewa huduma kama hiyo.
Bunge nchini Uganda linatarajiwa kutumia Dola za Marekani 177,000 kuwatuza medali wabunge 1,200 waliohudumu katika bunge la nchi hiyo kati ya mwaka 1962 hadi 2012.
Vyombo vya Habari nchini humo vinaripoti kuwa sherehe za kuwatuza wabunge hao zitafanyika mwishoni mwa mwezi huu katika maadhimisho ya miaka 50 ya Bunge hilo.
Hatua hii imekuja baada ya Gazeti la serikali ya New Vision kutangaza kuwa bunge limepanga kutumia fedha hizo kufanikisha shughuli hiyo.
Hata hivyo raia wa Uganda, wameonekana wakipinga matumizi ya fedha hizo katika sherehe hizo wakati huu raia wa nchi hiyo wakiendelea kukabiliana na hali ngumu ya kiuchumi.
Wabunge 13 wamefariki dunia kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
0 comments:
Post a Comment