HAKUNA MAPENZI YA KWELI ( My story 4 )


Naomba kumalizia sehemu hii ya mwisho juu ya maisha yangu ya ndoa. sehemu hii ndiyo ya mwisho na ya kusikitisha zaidi na hii ndiyo hasaa lengo kubwa la kuandika makala haya katika Blog yangu, naamini watu wengi watashangaa sana kuona kuwa nimeeleza maisha yangu hapa lakini mimi napenda sana iwe hivyo ili kila mtu aweze kujifunza kile ambacho kilinipata, nimeandika kwa hiyari yangu mwenyewe bila kushurutishwa na mtu yeyote na pia napenda kueleza hapa kwenye komputer naandika kwa mikono yangu bila mtu yeyote kunishurutisha. Najua wapo watakaoniona kama mjinga fulani, hivi lakini wengine watachukua changamoto iliyo ndani ya makala hii, simulizi hii ni ya kweli na ndiyo maisha yangu halisi na kila kitu kilichoandikwa hapa ni cha kweli na hakuna kitu chochote kilichoongezewa.
Tuendelee na stori yetu sasa...


Baada ya sakata hilo wazazi waliweza kuja na kutafuta suluhisho lakini ni kama vile kupooza tu lakini hali ilizidi kuwa mbaya zaidi kwani huyu mke wangu aliamua kwenda kwa waganga ili anifunge nisiweze kumfuatilia, alipewa Dawa ili aniwekee kwenye chai na nyingine aliambiwa aipeleke makaburini anyunyize juu ya kaburi huku akinuiza kuwa mimi ninyamaze kama kaburi ilivyo nyamaza na nikubali kila kitu atakachoniambia, haya yote niliyajua baada ya siku hiyo alipotoka kwa mganga niliweza kufuatiliandani ya mkoba wake na kukuta hizo dawa. Niliamua kufanya hivyo baada ya kujulishwa kila kitu na rafiki yake aliyekuwa anaitwa Eliza kunijulisha kuwa walienda kwa Mganga na kunieleza kila kitu walichoelezwa na Mganga kukifanya na pia nilikuta karatasi aliyokuwa ameandika maelezo ya Mganga ili asije akasahau.

Nilikuwa namwamini Mungu wangu sana na niliamua kumwachia Mungu kila kitu. nilizitoa zile Dawa nikaweka juu ya kitanda ( kumbuka wakati huo Mama Max hakuwepo niko mwenyewe ndani ya nyumba na hata ungeniuliza yuko wapi nisingepata jibu la kukupa) Baada ya kusoma habari zote za ile karatasi nilipiga magoti na kumuomba Mwenyezi MUNGU juu ya jambo hilo na kuangalia upya mwenendo wa Familia yangu kwani naona inanishinda. Nilisali dua ya kuyakabidhi maisha yangu kwa MUNGU na kuikabidhi pia familia yangu kwake. Baada ya Dua hiyo nilichukua maji ya Baraka na kuinyunyiza juu ya zile dawa zote huku nikisema kuwa kama Nguvu za mganga zitaweza kushinda Nguvu za MUNGU ninaye mwamini basi hata kama Nikihangaika sitaweza kujiokoa mwenyewe. baada ya hapo nilizirudisha zile dawa ndani ya Mkoba wake na kuuweka sehemu ile niliyokuwa nimeuchukulia na kutoka. Baada ya hapo niliamua kwenda kanisani kwenye mazoezi ya kwaya kama kawaida yangu lakini nikiwa na imani kuwa hakuna kitu chochote kitakachonipata kwani nilikuwa namwamini MUNGU. na pia nilijua kuwa yale maji ya baraka yatakuwa yameshaua ile nguvu za mganga na zile dawa hazitaweza kufanya kazi.

Baadaye nilivyorudi nilimkuta amesharudi na anaendelea na maandalizi ya Chakula chqa jioni, nilimuuliza habari za kushinda na mtoto anaendeleaje naye alinijibu kuwa kila kitu kiko sawa, niliamua kubaki kimya bila kuuliza kitu chochote kile .

Baada ya wiki moja kupita alinianga kuwa anaenda nyumbani kwetu kisangara kusalimia. kwanza nilishangaa kwani najua kuwa yeye na Mama yangu hawapatani na sasa anataka kwenda kumsalimia, sikuhoji nilikubali huku nikitegemea kuwa kama ataenda kwa siku mbili basi baada ya siku ile ningeenda mimi siku inayofuata kuhakikisha kuwa kama ni kweli yuko nyumbani kwa mama. Kabla hata hajaondoka Eliza alikuja kazini na kunieleza kuwa Mama Max alipanga kwenda Same ili kutafuta dawa nyingine baada ya zile kushindwa kufanya kazi, alisema kuwa sasa hivi anataka akuondoe Duniani kabisa ili aweze kufanya mambo yake kwa uhuru zaidi, aliniambia kuwa Mama max amemwomba amsindikize huko kwa Mganga siku na akamwambia kuwa atakuja kuongea naye ili aje kunieleza mimi kabla ya kumpa jibu kama atamsindikiza ama la!
Nilimwomba Eliza akubali kumsindikza ili aweze kujua kila kitakachoendelea na kunijulisha. alikubali na wakasafiri wakiwa watatu yaani Mama Max, Max. na Eliza Nilishajua kuwa hakuna safari ya nyumbani bali ni uongo tu ili aende kwa mganga wake.


Baada ya siku mbili walirudi na Eliza alinieleza kuwa wamepewa Dawa za Kuzika Makaburini na nyingine za kutupa mtoni na Eti baada ya siku 3 mganga atamtuma Nyoka aje kuniuma nami nitakufa baada ya hapo kwa kuumwa na nyoka. Niliumia sana na nikaendelea Kumwomba Mungu, Niliweka Novena ya Kuomba huruma ya MUNGU kwa Muda wasiku 9 Nilisali sana hasa katika kipindi hiki cha siku tatu nilizoelezwa kuwa nitauwawa na nyoka. Siku tatu zilipita bila kuona dalili hali kadhalika siku ya Nne na ya Tano na ya sita, hakuna kitu kibaya kilichonipata Nilifurahi kiasi fulani baada ya kujua kuwa MUNGU yupo upande wangu. Sikufurahi kwa sababu vita bado ilikuwa inaendelea ila nilicho furahi ni kuwa nilikuwa jasiri sana na wala sikuwa mtu wa kukata tamaa haraka kiasi hicho, niliamini kuwa MUNGU ni mweza wa yote na kweli alinisimamia hadi mwisho Tuliendelea na maisha kama kawaida hadi nilipomaliza Novena yangu siku ya 9, hakuna jambo lolote baya lililonipata. Nilimshukuru sana Mungu wangu kwa Neema ya ulinzi ambayo aliniwekea kwa kunilinda na wanadamu hasa wa familia yangu kama mke wangu mwenyewe kujaribu kutaka kuniua ili aweze kuwa huru na maisha ya kuwa kahaba kama alivyokuwa anataka.

Maisha yaliendelea kama kawaida na hakuna hata siku moja niliweza kusikia mipango yake tena ndani ya wiki ya tatu lakini mwanzoni mwa wiki ya Nne aliniomba kuwa anataka kwenda kwa wazazi wake usangi kusalimia kwani kaambiwa Bibi Mzaa baba ni Mgonjwa Pamoja na babu yake. Sikuwa na pingamizi yoyuote niliamua kumruhusu siku ambayo ataona ni sahihi kwenda basi ruksa kwenda. aliniambia kuwa bado ahajapanga ataenda lini lakini alikuwa akinijulisha tu, kuwa anaomba ruhusa ili aweze kwenda. Niliondoka kwenda kazini, mchana nilivyorudi kwa ajili ya lunch nilikuta chakula mezani lakini mke wangui hakuwepo. Nilifika mezani nikaanza kula chakula bila kujua kuwa niko kwenye hatari ya kupoteza maisha, kwani chakula kile kilikuwa kimewekwa pale spesho kwa ajili ya kuyatoa maisha yangu, Ndio kilikuwa kina sumu kali ya Panya. nakumbuka , kijiko cha kwanza nilimeza lakini baada ya kuchota kingine nile nilishtuka hasa baada ya kusikia harufu tyofauti na ya chakula nilishtuka zaidi baada ya kuona tumbo linauma, nilitupa kijiko na kutoka nje ya nyumaba. nilihitaji kuwahi kazini kwani pia ni Hospital, lakini niliishiwa na Nguvu baada ya tu ya kufika nje ya nyumba nilianguka chini, majirani walikuja na waliweza kuniokoa kwa kuwahi hospital haraka.


Kati ya yote niliyotendewa hili silisahau maisha yangu yote, namshukuru Mungu wangu maana niko hai hadi sasa naendelea kupumua. Sifa na Utukufu ziende kwake. Nilirudi nyumbani ilikuwa ni saa 5 usiku na kumkuta yupo barazani mwa nyumba yetu kama vile alikuwa ameogopa sana mimi kuchelewa kwani baada ya kuona watu wanakuja alitufuata na kuuliza kulikoni sijarudi nyumbani mpaka usiku wote ule? nilimwambia kuwa nilikuwa naumwa ndio maana nilichelewa, Hakuuliza tena ila aliamua kubaki kimya nami niliogopa hata kulala kitanda kimoja usiku ule bali nilikaa sebuleni nikiangalia mikanda ya kwaya hadi asubuhi kulivyopambazuka, Pamoja na hali niliyokuwa nayo ya kubanwa sana na kifua kutokana jinsi nilivyotapika l;akini sikuwa tayari kulala. Asubuhi ndo alikuja barazani na kunieleza kuwa asubuhi hiyo ndo alikuwa anaenda kumpa pole Bibi na babu yake huko Usangi Nilishukuru kwanza aondoke ili niweze kuyatafakari na kutafuta hatua ya kuchukua baada ya kutulia kweli aliondoka yeye na mtoto, nikamwacha aende.
Baada ya kufika siku ya pili nilipigiwa simu na kujulishwa kuwa Babu yake alifariki Dunia, ikabidi nami nipange tena kwenda kwenye msiba baada ya mazishi nilirudi nyumbani na kumwacha kwao. alikaa na Bibi yake kwa muda wa mwezi mzima bila kurudi kwangu, nilijua ni kwa nini harudi, watu waliamini baada ya jaribio la kuniua kushindikana basi alikimbia Alikuja baada ya mwezi mmoja alikuja usiku saa mbili nilikuwa nasoma vitabu vyangu vya dini na kutunga nyimbo mbalimbali za kwaya kwani nilikuwa mtunzi na mwalimu wa kwaya Kanisani kwetu. tulilala hadi asubuhi bila kuzungumza chochote kile naye asubuhi ndio aliniambia kiuwa nilikuwa nasalimiwa na wazazi wake pamoja na Bibi. Nilimwambia nashukuru kisha nikampa pesa za matumizi ya mchana na mimi kuelekea kazini. NILIRUDI MCHANA Nilifika ndani , mlango ulikuwa wazi na cha ajabu kabisa ndani nilikuta nyumba tupu hakukua na nguo wala vitu vya ndani, vilibaki vichache sana na kwenye meza ndogo nilikuta barua iliyokuwa imeandikwa hivi......

Baba Max, Mjomba amekuja kunichukua ili niende kusoma maana nimeona sitaweza kuendelea kuishi na wewe tena. Upatapo barua hii jua huo ndio utakuwa mwisho kati yangu mimi na wewe. Nakuomba usinitafute na kama utanitafuta ujue kuwa unatafuta kifo chako, naomba nirudie kuwa sio kwamba nimeshindwa kukuondoa duniani baada ya kuokoka mara mbili, ila sasa kama ukihitaji nikuue basi nitafanya hivyo Nakupa ruhusa ya kuoa kama unataka kama hutaki pia hilo ni shauri yako byee.
NIliisoma ile barua na kuirudia mara mbili mbili bila kupata majibu , ila nilifurahi kwamba aheri kutengana kuliko kuishi kwenye ndoa ya aina ile ambayo kwa hakika ndani ya miaka mitatu nilionja joto ya jiwe UPENDO UPO WAPI, MAPENZI YA KWELI YAPO WAPI, HAKUNA NASEMA HAKUNA KABISA KITU KAMA HICHO HUMU DUNIANI NA SEMA TENA. HAKINA MAPENZI YA KWELI HUKU DUNIANI 


Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: