Leo naendelea kuwaletea kile amabcho kilitokea baada ya wazazi kueleza kuwa hawakuwa tayari kunisaidia baada ya wao kutukanwa.
Nilirudi na kumuuliza mke wangu juu ya jambo hilo aliniambia kuwa haoni sababu ya yeye kupatana na wazazi wangu kwani kila mtu ana familia yake hapo ndipo ugomvi ulipoibuka na kusababishwa hali ya maelewano ndani ya nyumba kupotea, Niliumia sana baada ya kugundua kuwa mke wangu alikuwa na dalili za kuweza kuvunja ndoa yetu kitu ambacho kwangu nilikuwa nakiogopa sana.Nilimweleza paroko wangu naye bila kupoteza muda alimtumia ujumbe kuwa aje kuonana naye lakini mwanamke alikataa kuongea naye na matokeo yake akaniambia kuwa kama nilifikiria kuwa anaweza kwenda kanisani basi nilikuwa nimechemsha kwani hata tu ria ibada ya misa siku ya Jumapili hataenda hata siku moja na kama nitamlazimisha basi atarudi kwao. Nilikaa nikitegemea kuwa Paroko atachukua hatua ili kunusuru ndoa yangu kwani mimi nimehangaika sana bila mafanikio na wakati huo hata unyumba ilikuwa hakuna na kama kaka na dada kwa muda wa miezi saba. nakumbuka siku moja nilikuwa nina OFF duty kazini ya wiki moja nikaamua kwenda kwa mjomba yangu aliyekuwa anaishi Arusha, baada ya kurudi nilikuta hali ya ajabu sana ambayo ilinishangaza sana. Nilikutanguo za Polisi pamoja na viatu vya police ndani ya nyumba nilishangaa hali ile nikahitaji kupata majibu lakini sikua na mtu wa kunieleza kuwa yale mavazi yalikuwa ya nani. Nilingoja hadi jioni ambapo mke alitokea saa tatu usiku na aliponiona alishtuka sana na kuniuliza kwanini nilikuja bila taarifa? Nilimwambia kuwa kwa vile pale ni kwangu nina weza kuja muda wowote ninaotaka bila kufikiria kuwa ni saa ngapi au ni siku gani. kwa nini nitoe taarifa wakati ni nanyumbani kwangu. hayo niliiyaacha na usiku nilimuuliza juu ya yale mavazi ya polisi kuwa ni ya nani na yanafanya nini pale nyumbani akaniambia eti kwani mtu hawezi kuomba kuwekewa mavazi ndani. aliniambaia kuwa ni za mwanafunzi anasoma shule ya sekondari ya Mwanga. nilimwambia kuwa mbona mavazi yale ni ya kiaskari na wala si ya wanafunzi ? aliniambia kuwa hayo maswali ningojee mwenyewe akija ndo nimuulize kwani hajui kuwa ni ya askari au ni ya mwanafunzi. niliamua kunyamaza nikimwahidi kuwa nitakuja kuujua ukweli tu baadaye kwahiyo sina hofu yoyote lazima nijue ukweli wake na chanzo yale mavazi ndani ya nyumba u, hakuwa na wasiwasi wowote juu ya jambo hilo. aliniambia kuwa vyovyote nitakavyoona.>>>>itaendelea kesho>>>>>>>

Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
0 comments:
Post a Comment