HAKUNA MAPENZI YA KWELI DUNIANI. My story 2.


Baadaye nilikuja kugundua kuwa mke wangu hakuwa mwaminifu na alikuwa ameanza kazi ya kuchanganya wanaume. Nilikuwa naambiwa na marafiki zake wa karibu juu ya mambo anayofanya mke wangu lakini sikuwa naamini moja kwa moja, nilihitaji kufanya uchunguzi kwanza ili kujua juu ya jambo hilo. kwanza nilitumia marafiki zangu kuchunguza juu ya jambo hilo, ambao baadaye waliniambia kuwa jambo hilo ni kweli na wakawa wamenieleza watu mbalimbali wanatembea na mke wangu. kwanz tua waliniambia kuwa wapo maaskari wawili na wote wana uhusiano naye na pili yupo mwalimu wa shule ya sekondari ambayo ipo karibu na sehemu ninayoishi.
Pamoja na marafiki zangu kunieleza hilo bado nilikuwa nampenda mke wangu na wala sikuwa tayari kumuacha. Niliamua kufanya uchunguzi mwenyewe juu ya jambo hilo la mke wangu kutokuwa na uaminifu katika ndoa yetu. Kwa ujumla ni kuwa na mapenzi kwenye familia yangu ambayo sikuwa tayari ivunjike maana mtoto wangu angepata shida ya kukosa malezi bora ya lo wazazi wake. sikupenda jambo hitokee kwangu. niliamua kutumia busara kurekebisha jambo hilo. niliwaarifu wazazi juu ya jambo hilo. Cha ajabu ni kwamba mke wangu hakuwa na uhusiano mzuri na wazazi wangu kwa muda mrefu na alishawapiga marufukuja kutembelea familia yetu, wazazi kunieleza juu ya hayo kutokana na kufikiria kuwa wangeivunja ndoa yangu. Nilielezwa yote na kujikuta naumia sana. Wazazi waliniambia kuwa wangewezaa kunisaidia lakini hata wao walishakwaruzana na mke wangu kwa hiyo hawana siano mzuri na mke wangu hivyo kilichopo mbele yangu kwanza ni kurekebisha kasoro hiyo, Nilamua kuwa ni vema kuangalia kwa kina jambo hilo...........



Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: