Mara nyingi watu hukutana na neno hili> hujafa hujaumbika. lakini neno hili linaweza kutafsiriwa na kila mtu kadri anavyoweza kulielewa. na jinsi anavyoishi. Mimi binafsi naomba kueleza mambo ambayo nilikutana nayo katika maisha yangu ambayo naamini kuwa itakuwa changamoto nzuri kwa wenzangu ambao wapo katika pilikapilika kama zangu.
Jambo kuu na la msingi juu ya kuamua kuelezea historia yangu yote ni kuhusu hasa suala la Ndoa. Maisha ya ndoa na kuhusu mapenzi ya kweli katika ardhi hii ya Muumba wetu wa Mbinguni.
Nianze kwa kujitambulisha kwanza ili kila mtu aweze kunifuatilia katika story yangu hii, na naamini kuwa ndani ya maelezo yangu haya kuna changamoto mbalimbali za kuifundisha jamii, na kama huyo mlengwa mkuu aliyenifanya kufikia hatua hii ya kuweka hapa kila kitu akisoma hapa anaweza kujua kuwa ni kiasi gani alivyoweza kuyaharibu maisha yangu na malengo yangu yote ya maisha
Mimi naitwa Josephat Ernest Msoffe na nimezaliwa miaka 30 iliyopita katika kijiji cha Kisangara kilichopo wilaya ya Mwanga mkoani kilimanjaro. Ndani ya familia yetu yenye watoto 7 mimi ni mtoto wa pili kutoka mwisho. yaani mtoto wa sita kati ya saba wa familia ya mzee Ernest Msoffe. Familia yetu ilikuwa na watoto wawili wa kiume na watano wakike, Ndani ya hao wawili wa kiume mimi nilikuwa mmoja wapo ambayendiye ninayehadithia haya yalionipata katika maisha yangu baada ya kaka yangu kufariki au kuuwawa baada ya kuvamiwa na majambazi katika mkoa wa Arusha mwaka 1995. shule ya msingi na seminary YA CHANJALE Ndipo nilipopata elimu yangu ya msingi na hadi kufikia elimu ya juu yaani sekondari. Mwaka 1998 niliamua kutoa maisha yangu kuwaasaidia wagonjwa mbalimbali ambapo nilijitolea kwa muda wa mwaka mmoja na ndipo nikaweza kujiunga na cha maabara kuchukua mafunzo ya ufundi sanifu maabara katika chuo cha Ikonda kilichopo Iringa. mwaka 2002, niliweza nkupata ajira katika Zahanati moja ijulikanayo kama Neema Rc Dispensary iliyokuwa inamilikiwa na Shirika la Wanagrail Tanzania na hapo ndipo nilipoanza maisha ya kujitegemea pia nikijua kuwa siku moja nitakuwa na familia yangu itakayo nitegemea.
Hayo yalikuja kutimia baada ya mwaka mmoja wakufanya kazi niliweza kumpata mwenzangu ambaye tuliahidiana kuoana na kujenga familia yetu. Kwa kweli baada ya muda mfupi ndoto yetu ilitima baada ya kukubaliana kwa pande zote mbili tuliweza kufunga ndoa katika kanisa la Katoliki Parokia ya Chanjale ambayo pia ipo katika kijiji hicho cha Kisangara. Baada ya ndoa hiyo tulianza maisha ya ndoa na mwenzangu ambaye alikuwa akiitwa Shanni kabla ya kubadilisha dini na kuwa Mkatoliki hivyo kupewa jina la Rose. Naomba kusema kuwa huyu mwenzangu alikuwa ni mkazi wa kijiji cha Usangi wilaya ya Mwanga. na mwaka huo huo Mungu alitujalia kupata mtoto wa kiume ambaye tulimpa jina la Maxmilian.n Nilimlea mwanangu kwa upendo mkubwa hadi alipoifikisha miaka miwili ambapo nilitenganishwa na mwanangu niliyempenda na familia yangu yote kusambaratishwa, hakika sitaweza kuzisahau siku hizo, na ninapokumbuka machozi yananitoka. Sikuweza kufikiri hata siku moja kuwa kuna wanadamu wenye roho mbaya huku duniani ambao wapo tayari kutoa uhai wa mtu ili waweze kumiliki mali au mapenzi. Hakika hiki ndicho kimenifanya kuandika makala haya na kama unaweza kunipa mawazo yako, nakukaribisha maana kwa kweli maji yamenifika SHINGONI.
.................ITAENDELEA>>>>>>>>>

Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
0 comments:
Post a Comment