MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari nchini (TPA), imeanza kutekeleza mradi wa kuboresha gati namba mbili katika Bandari ya Tanga ambao utagharimu Sh bilioni 9.2.
Kaimu Mkuu wa Bandari ya Tanga, Henry Arika amebainisha hayo jana wakati akitoa taarifa ya utendaji wa bandari hiyo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigella wakati alipotembelea.
Mradi huo unaojengwa na Kampuni ya M/S Commarco, unalenga kuongeza uwezo wa bandari hiyo katika kuhudumia shehena ili iendane na kasi ya ukuaji uchumi wa viwanda pamoja na mradi wa bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) kutoka Uganda hadi bandari ya Tanga.
Alisema utekelezaji wa mradi huo, utawezesha mamlaka hiyo kuhudumia meli nyingi na kubwa zaidi pamoja na kuongeza shehena zinazopitia kwenye bandari hiyo, vikiwamo vifaa vya mradi wa ujenzi bomba hilo unaotarajiwa kuanza hivi karibuni.
Mkuu wa Mkoa Shigella, akizungumza wakati wa ziara hiyo, aliwataka wananchi wa mkoani huo kujipanga, ili waweze kunufaika na fursa za uwekezaji zilizopo katika bandari hiyo, ambao utachochea ukuaji wa shughuli za kilimo, biashara na viwanda.
Awali, Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi, Ally Sankole, ameiomba Serikali kuongeza vitendea kazi katika bandari hiyo ili kukabiliana na ushindani na bandari nyingine
Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
0 comments:
Post a Comment