TUJIKUMBUSHE:HII SHULE BADO HAIJAIISHA FILIKUNJOMBE KUJENGA UPYA SHULE YA MSINGI LUDEWA MJINI BAADA YA KUKUMBWA NA KIMBUNGA ,WAZIRI PINDI ACHANGIA TSH 15000









  • Wananchi  wa Ludewa  wakishusha  bati  15o zilizotolewa na mbunge wa  Jimbo la Ludewa  Deo Fikunjombe kwa  ajili y  kusaidia kuezeka katika vyumba vinne  vya madarasa katika  shule ya msingi Ludewa  mjini vilivyoezuliwa na kimbunga 
    Wanafunzi wa  shule ya msingi Ludewa mjini  wakikusanya bati chakavu 
    Katibu  wa  mbunge wa Ludewa Bw Stanley Gowele  akipita kando ya vyumba vya madarasa  vilivyoezuliwa na kimbunga 
    Mbunge  wa  jimbo la Ludewa  Deo Filikunjombe akisaidia  kushusha bati 
    FIlikunjombe kulia akibeba bati alizozitoa  kwa ajili ya shule ya msingi Ludewa mjini 
    Baadhi  ya  walimu wa  shule ya msingi Ludewa  wakimpongeza mbunge Filikunjombe kwa  msaada  wake 
    Mbunge wa  jimbo a Ludewa Deo FIlikunjombe akifafanua  jambo 
    Wanafunzi  wa  shule ya Msingi Ludewa mjini  wakisomba bati  zilizotolewa msaada  wa mbunge Filikunjombe 
    Mbunge Filikunjombe kushoto  akishirikiana na  wanafunzi  wa  shule ya Msingi  Ludewa mjini kusomba bati 
    Filikunjombe akishiriki  kusomba bati 
    Mbunge  Filikunjombe na viongozi  wengine wakisomba bati 
    WAnanchi  wakishiriki  kusomba bati 
    Mbunge Filikunjombe akitazama vyumba  vya madarasa  vilivyoezuliwa 
    Filikunjombe akitembelea jengo  hilo 
    Filikunjombe  akizungumza na wazazi na  walimu  wa  shule ya msingi Ludewa mjini 
    Walimu na  wazazi  wakimpongeza mbunge Filikunjombe kwa msaada  wake mkubwa 
    Filikunjombe  akitoa  maelekezo kwa  kamati ya  shule na  wazazi 
    Mkuu  wa  shule  hiyo Bi Agnes Magazi  akimwongoza  mbunge Filikunjombe  kutazama vyumba vya madarasa  vilivyoezuliwa 
    Wananchi wakishirii kusomba saruji iliyotolewa na mbunge  Filikunjombe 
    Diwani  wa kata ya  Ludewa mjini MOnica Mchilo kushoto na afisa maendeleo ya jamii  Ludewa mjini Teopista  Kayobo wakishiriki  kubeba  saruji 
    Katibu  tawala  ya Mawengi Bw Dames Kavindi na fisa maendeleo ya jamii  Ludewa mjini Teopista  Kayobo wakishiriki  kubeba  saruji 
    Mbunge  Filikunjombe  akishuhudia mchanga ukishushwa 
    Filikunjombe  akitoa maelekez o
    Filikunjombe akishiriki  kuchanganya mchanga na  wananchi 
    Filikunjombe akishiriki  kusomba mbao 

    Mbunge  wa  jimbo  la  Ludewa  Deo Filikunjombe akishiriki  kusoba mbao kwa ajili ya kujenga vyumba vya madarasa vitatu katika  shule ya msingi Ludewa mjini vilivyoezuliwa na kimbunga mwanzoni mwa mwaka huu kabla ya kujitolea zaidi ya Tsh milioni 13  kujenga upya vyumba hivyo 
    Mbunge  wa  Ludewa  Deo Filikunjombe  kushoto na katibu  wake Stanley Gowele   wakipata  chakula cha machana eneo la ujenzi pamoja na  wapiga kura wake  
    Katibu  wa  mwenezi wa CCM mkoa wa Njombe Bw Honaratus Mgaya  kulia na katibu wa mbunge Bw Gowele na mbunge Filikunjombe  wakipata  chakula 

    ..........................................................................

    UONGOZI   wa   serikali ya  tarafa ya  Mawengi wilaya ya  Ludewa mkoani Njombe umempongeza naibu waziri  wa maendeleo ya jamii njinsia na  watoto Pindi  Chana kwa  kuchangia kiasi cha Tsh  15000 katika  shule ya msingi Ludewa mjini baada ya  shule  hiyo kupatwa na maafa ya kuezuliwa vyumba  vitatu   vya madarasa mwanzoni  wa  mwaka  huu.

    Afisa  tarafa ya  Mawengi  Bw Damas Kavindi  alitoa pongezi hizo  leo wakati akipokea  msaada wa mbunge wa  jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe aliyejitolea  kujenga  upya vyumba   hivyo  vya madarasa kwa  kwa  zaidi ya Tsh milioni 13 .

    Katibu  tarafa  huyo  alisemakuwa   majengo  hayo yaliezuliwa na  kimpunga toka februari 28  mwaka   huu na kiongozi wa kwanza  kufika  kutoa  pore  alikuwa ni Pindi  Chana ambae ni mbunge wa viti maalum mkoa  wa Njombe na mjumbe wa kamati kuu ya CCM Taifa .

    " Kweli  tunamshukuru  sana Pindi Chana  kwa  kufika mapema  zaidi  na yeye  nyumba yake na  shule ni kama mita  200 hivi kwa maana ya kuwa  kingozi  pekee anayeishi jirani na  shule hiyo ......mbali ya  kutupa pore kwa maafa hayo aliweza kutuchangia  kiasi cha Tsh 15000 kwa  ajili ya pore na kutuunga mkono kwa  zoezi  kubwa lililokuwa  mbele yetu"

    Pia  aliwapongeza  wananchi kwa  kuchangia kiasi cha Tsh milioni 1.8  kabla ya  mbunge  wao  kujitolea  kujenga  shule  hiyo kisasa zaidi ili   kuwaondoea adha  ya  kuchangishana kwa  wananchi wanaozunguka  shule  hiyo .

    Alisema  kuwa Kutokana na mahafa hayo wanafunzi 200 kukosa sehemu ya kusomea hivyo kulazimika mikondo miwili kukaa chumba kimoja.

    Akishukuru kwa niaba ya walimu wa shule hiyo mkuu wa shule hiyo Bi Agnes magazi alisema msaada huo ni mkubwa na utapelekea wanafunzi hao kupata sehemu ya kusomea.

    Alisema kuwa kutokana na vyumba hivyo vitatu kukumbwa na kimbunga pia wanafunzi wa darasa la nne ambalo lipo Jirani na vyumba hivyo vitatu pia walilazimika kuhama vyumba vyao.

    Huku kwa Mwenyekiti wa Kamati ya shule Francis Nkwera alisema kuwa Kamati yake baada ya tatizo hilo ililazimika kuzunguka kwa wadau mbali mbali kuomba msaada ili kupata kiasi cha Tsh milioni 13 .1 ili kujenga Nyumba hivyo fedha ambazo hazikuweza kupatikana zaidi ya kupata kiasi cha Tsh milioni 1.8 kwa kipindi chote cha zaidi ya miezi 10 kabla ya mbunge kuingilia Kati .

    " msaada wa mbunge wetu ni mkubwa sana kwani pasipo kuingilia Kati kujitolea kujenga vyumba hivi vya madarasa vingemalizika baada ya miaka miwili mbele kutokana na kasi ndogo ya uchangiaji"

    Kwa upande wake mbunge Filikunjombe alisema kuwa ameguswa kujitolea baada ya kuona watoto wanapata shida kubwa hivyo kama mbunge asingependa kuona wanafunzi hao wakisoma kwa shida zaidi.

    Hivyo alisema kwa upande wake atahakikisha anajenga upya vyumba vyote vilivyokumbwa na maafa hayo na kuwa Ujenzi wake utakuwa wa kisasa zaidi tofauti na majengo mengine shuleni hapo .

    Alisema Pindi Ujenzi huo utakapomalizika atahakikisha anaingiza umeme ili kuwawezesha watoto shuleni hapo kusoma kwa raha zaidi.

    Hivyo alitaka wazazi kujitolea nguvu zao na suala la mafundi,vifaa vyote vya madukani zikiwemo bati 150 za kutosha kuezeka vyumba hivyo ni jukumu lake .



Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: