Siri za mwanamke



Mwanamke anahitaji nini kutoka kwa mwanaume?

KUTATULIWA MATATIZO

Wanawake wengi hutegemea kuwa wanapokuwa na wapenzi watasaidiwa katika matatizo ya kimaisha na migogoro ya kimawazo. Kwa mfano ushauri juu ya maisha yao, kulindwa na hatari za kimaisha, kusaidiwa katika shida na kuongozwa pale wanapohisi kushindwa kufanya jambo. Kama mwanaume hatamfanyia mpenzi wake hili atakuwa amekosa sifa za kuteka penzi la mwanamke.

KUBEMBELEZWA

Wanawake hupenda kubembelezwa pale wanapokuwa na huzuni, wengi wao hawapendi kukaripiwa, mara nyingi hupenda kuungwa mkono wanapokuwa na misuguano na wengine. Ili mwanaume amteke kimapenzi mwanamke lazima awe nyuma yake hata kama atakuwa na kosa. Wanawake wengi hupenda kuelimishwa zaidi kuliko kufokewa.

KUWA NAMBA MOJA

Safari ya penzi la mwanamke haishii kwenye kumpata na kumliki, kisha kujisahau kwa kisingizio kuwa umemuoa au umemvisha pete ya uchumba, ni zaidi ya hapo. Jambo la tatu ambalo wanawake wengi huhitaji ni kuwa namba moja au kupendwa.
Wanapenda watangulizwe katika mapenzi na kusiwepo na mwingine wa kuchukua nafasi yao katika mazungumzo na mapenzi kwa ujumla. Wanawake hawapendi kuitwa majina mabaya kwa mfano mjinga, Malaya au kulinganishwa na wanawake wenzao wabaya.

KURIDHISHWA KWENYE TENDO

Hata kama utakuwa na kiwango kikubwa cha mapenzi juu ya mpenzi wako kwa kiwango gani, ukiwa dhaifu katika tendo la ndoa utayumbisha penzi lako. Ni wajibu wa mwanaume kuhakikisha kuwa anamtosheleza mpenzi wake katika tendo hilo. Utundu unahitajika ili kumkata kiu mpenzi wako.

MAZUNGUMZO

Wanawake wanatajwa kuzungumza maneno 25,000 kwa siku, huku wanaume wakibaki na kiwango cha maneno 5,000 kwa siku, hii ikiwa na maana kuwa wanawake hupenda zaidi kujieleza walivyo mbele ya wengine. Kwa msingi huo wakizuiwa wasiongee hujiona kama wanakosa nafasi muhimu ya kueleza mawazo yao. Kama una mpenzi wako mpe uhuru wa kuzungumza na kumsikiliza bila kumkatiza kwa ukali.
Mikono.JPG

Wanawake wanavutiwa na nini zaidi kwa wanaume

Kama mwanaume lazima upate wakati wa kujua unatakiwa kufanya nini kwa ajili ya kulifanya penzi lako lizidi kuchanua.

USAFI BINAFSI

Asilimia kubwa ya wanawake wanapenda sana usafi. Ni aghalabu sana kukutana na mwanamke asiyejipenda. Ndiyo maana wanaitwa mapambo ya nyumba au la nyumba! Ni kwa sababu ya hulka yao ya kupenda sana usafi.
Mwanamke anavutiwa sana na mwanaume mtanashati. Usafi wako unamfanya ajiamini kuwa na wewe. Hata nyumbani kwako, lazima uishi katika nyumba safi. Hata anapokuja kukutembelea, anakuta mazingira masafi kuanzia sebuleni hadi chumbani.
Anapokukuta katika hali ya usafi, inakuwa rahisi zaidi yeye kuanzia hapo alipokukuta na kuendelea mbele.

KUJIAMINI

Mwanamke anajisikia salama zaidi akiwa na mwanaume ambaye anajiamini – mwenye uwezo wa kutetea hoja zake na kujieleza sawia. Siyo anayebabaika. Suala la msimamo binafsi, kwa mwanamke ni kubwa kuliko hata kumnunulia manukato mapya!
Mathalani unakuwa naye katika mtoko, angependa kukuona ukiwa katika hali halisi ya maisha yako, usiyeyumbishwa na mwenye kutoa maamuzi yasiyoyumba.
Wakati mwingine, mwanamke anaweza kukupima hata katika jambo ambalo amekosea yeye, ataangalia unavyotoa maamuzi yako, lakini pia atafuatilia kuona kama utakuwa mwepesi wa kuyabadilisha.
Anataka kuona msimamo wako muda wote. Mwenye kujiamini na mawazo yasiyo na matege wala makengeza!

KUJITETEA

Kipengele hiki hakina tofauti kubwa sana na kilichopita, lakini hapa ni kwenye upande wa kujitetea zaidi. Wakati unapodai haki yako mbele ya mwanamke wako, suala la kujitetea linapewa nafasi kubwa sana.
Wanawake hawapendi kuwa na wanaume ambao wapo tayari kuonewa. Wanataka wenye uwezo wa kusimama kidete kuona haki zao hazichukuliwi kirahisi.
Hili si suala la kutetea tu haki yako pekee kama mwanaume, bali inapobidi kusimamia haki ya mwanamke wako. Nisieleweke vibaya katika hili, lakini mwanaume imara ni yule ambaye ana nguvu – anafanya mazoezi na ambaye yupo tayari kwa lolote!
Inapowezekana, uwe na uwezo wa ‘kuzichapa’ ikiwa mtakutana na vibaka au watu wabaya wenye lengo wa kukudhuru/kuwadhuru au kumdhuru mpenzi wako.
Mwanaume aliye ‘fiti’ ni chaguo la wanawake wengi. Si mnyonge. Mpole kupitiliza na aliye tayari kuonewa! Huyu hana nafasi.

KUJALI

Wanawake wanapenda sana wanaume wanaojali. Wanawaona wao ni kila kitu na wanaotoa kipaumbele kwao. Kama huna tabia hiyo, ujue upo katika nafasi kubwa ya kumkwaza mpenzi wako. Mjali mpenzi wako kwa kila hali.
Kumjulia hali kila wakati na kutaka kujua maendeleo yake, kutakupa nafasi kubwa sana ya kuendelea kudumu katika uhusiano hai.

UKARIBU

Kati ya vitu vinavyowapa mshawasha mkubwa wanawake ni pamoja na kusogezwa karibu. Hapa ni kuwa naye katika mambo mengi unayoyafanya kila siku.
Ni vizuri kuwasiliana naye mchana, ukitaka kujua aina ya chakula alichokula siku hiyo au ikiwezekana mchagulie. Ni mambo madogo sana lakini yanayoongeza nakshi katika mapenzi.
Yapo mengi sana ambayo kwa kuyafanya utakuwa umemsogeza mpenzi wako karibu yako. Hebu tumia ubunifu wako ili uweze kuteka hisia za mwenzi wako kisawasawa!

KUMSIFIA

Wanaume wengi hupuuzia hili, huona kama ni jambo lisilo na maana sana kwao na wenzi wao. Hali ni tofauti sana kwa wanawake ambao hupenda kuwasifia wanaume zao. Nitakupa mifano miwili ya namna wanandoa wa jinsia mbili tofauti wanavyotambulishana kwa jamaa zao.
MWANAUME: “Peter kutana na mke wangu, anaitwa mama Diana. Nipo naye mwaka wa tatu sasa, tuna watoto wawili, huyo Diana na mwingine anaitwa Cris. Mama Diana, huyu ni Peter nilisoma naye A – Level, Tosamaganga Sekondari.”
MWANAMKE: “Suzan, huyu ndiye mume wangu mpenzi…anaitwa Elifaraja lakini mimi napenda zaidi kumuita Elly. Kiukweli nampenda sana mume wangu jamani, tuna mtoto wetu mmoja, anaitwa Agness. (Akimgeukia mumewe) Baby, huyu hapa ni rafiki yangu Suzan. Yaani tumekua naye mtaa mmoja huko Arusha.”

ANGALIA TOFAUTI

Bila shaka kwa namna wawili hao walivyotambulishana unaweza kuona tofauti kubwa. Mwanaume amemtambulisha mkewe kawaida kabisa, hajaonesha manjonjo au namna anavyompenda na kumthamini mwenzake, lakini mwanamke amefanya hivyo.
Sikia nikuambie, KUMSIFIA mwanamke, kuna nafasi kubwa sana kwake. Chunguza kwa makini, hata kunapokuwa na mgongano katika familia, halafu wakatokea wageni, baada ya utambulisho na mazungumzo ya hapa na pale, wageni wakiondoka kunakuwa na uwezekano mkubwa zaidi wa kumaliza mpasuko katika familia.
Jenga utamaduni wa kumsifia mpenzi wako, unamuweka katika kilele cha upendo. Anajiona kamili, peke yake na mwenye nguvu kwako. Anajiamini na unamfanya azidi kukupenda kwa kuwa anaamini yupo na mwanaume ambaye anajivunia kuwa naye.

MALENGO

Wanaume wengi wana ulemavu mmoja; hawapendi kuwashirikisha wanawake katika mambo yao. Wanapenda kufanya mambo yao kwa siri na wakati mwingine ikilazimika kumwambia mkewe basi kwa mshtukizo baada ya kukamilisha jambo husika.
Hii si sahihi. Dunia ya leo imebadilika rafiki zangu. Inawezekana wazee wa zamani walikuwa sahihi, maana ilikuwa ni suala la kununua ng’ombe na kuwaweka katika zizi kwenye kijiji cha jirani, halafu wanapewa malisho mazuri, baada ya miaka miwili wanazaliana, hapo ndipo anamweleza mkewe.
Siku hizi dunia imebadilika, kuna mambo mengi. Kuna suala la hasara katika biashara, utapeli n.k. Mkeo ndiye rafiki yako mkubwa kuliko wote, ndiye ndugu yako wa karibu zaidi kuliko yeyote. Yes! Mkeo ndiye ndugu yako maana umetengeneza naye familia. Mmeshirikiana kuzaa watoto na kujenga maisha pamoja.
Yeye anapaswa kujua mambo yako, ndiye mtetezi wako nambari wani. Mweleze juu ya malengo yako, wakati mwingine anaweza kukusaidia sehemu ambayo hukutarajia.
Hata hivyo, kumshirikisha katika malengo yako, kunampa nguvu na nafasi ya kujiona mama katika familia yenu. Msaidizi kamili wa nyumba yenu.

KIPAUMBELE

Kuna wakati wanawake huwa na mambo yao binafsi. Kazini au kifamilia. Inawezekana akatatizika katika eneo fulani ambalo kwa namna moja ama nyingine atahitaji usaidizi wako. Ikitokea mkeo akawa katika hali hiyo, msikilize.
Mathalani ana tatizo la kifamilia, amekuambia mmoja wa wazazi wake anaumwa, msaidie. Si lazima kifedha, lakini kuonesha kujali kwako tu, kutampa matumani kwamba anaishi na mtu sahihi. Acha kupuuza mambo yake; hata yale madogo, kama ya ‘mtoto wa dada amerudishwa ada shuleni’.
Msikilize, mshauri panapofaa kufanya hivyo na ukiweza msaidie hata kifedha. Katika upande wa pili ni hivyo hivyo. Labda una tatizo binafsi, kazini kwako au kifamilia, mshirikishe.
Unaweza kushangaa jambo ambalo uliamini unaweza kulimaliza peke yako, kwa kumshirikisha likawa jepesi zaidi na mambo yakaendelea vyema. Kipaumbele kwa namna yoyote ile, kunaongeza mapenzi zaidi kwa mwanamke.

TENDO LA NDOA

Hiki ni kipengele nyeti, kinachohitaji lugha nzuri ya kirafiki kukifafanua. Hakuna siri, tendo la ndoa ni moja ya kiwakilishi cha ndoa. Maana hata maandiko yanasema: “Mwanamke ataacha wazazi wake na kwenda kwa mumewe, nao watakuwa mwili mmoja.”
Kimsingi tendo la ndoa lina nafasi yake. Ni muhimu likaheshimiwa na kutengewa muda maalum wa kufurahia. Si papara. Kwa bahati mbaya wanaume huwa si wafuatiliaji sana wa kujua namna ya kuwafurahisha zaidi wenzao. Wenyewe wanajiwazia wenyewe. Wanafikiria namna ya kuwakomoa wenzao.
Si sahihi. Tendo la ndoa halina maana ya kukomoana. Jenga mazoea ya kufanya maandalizi kamili kabla ya tendo. Sikiliza hisia za mwenzako. Ukiweza kumjulia mke wako katika eneo hili, ni wazi kwamba utazidisha upendo wake kwako, lakini pia atakuwa katika kuta za uaminifu. Akatafute nini nje wakati wewe ndiye mganga wake unayeweza kumtibu barabara?
Kuna kitu nimesahau kweli? Kama kipo nitafute pembeni, kwa hapa haya yatoshe kukufanya uelewe nilichotaka kukuelekeza. Nikuache na neno moja; uamuzi wa kuijenga ndoa yako upo mikononi mwako. Ukitaka iwe shaghalabaghala, pia ni wewe tu!
Tafuta%20marafiki

Wanawake wanatamani wanaume wajue mambo yafuatayo wakati wa kufanya mapenzi

Kuna baadhi ya vitu ambavyo wanawake hutamani sana wanaume zao wawe wanajua katika mambo mengi, ili wasipate shida ya kumwambia mara kwa mara, jambo ambalo si wanawake wengi huwa na guts za kumwambia mtu, hapo ndipo unakuta mara nyingi mwanamke anaanza kuchepuka na kwenda kwa mtu mwingine wa kawaida tu kupata mahitaji yake. Basi usikonde, haya ni baadhi tu ya mambo ambayo wanawake wengi hutamani wanaume wawe wanajua kabisa bila hata ya kuambiwa.

Hupendelea tendo la ndoa lidumu zaidi ya dakika mbili

Wanawake hupenda hata ikibidi ifanyike siku nzima, ila cha zaidi si muda ambao una-matter, imetokea wanaume wengi kujali kujizuia, ilimradi wa-last muda mrefu katika tendo, but kutokana na tafiti hili sio ishu kabisa, wanawake wengi hupenda zaidi ya muda mrefu, hupenda ku-establish connection wakati huo, ambao unafanyika through Kissing etc vitu ambavyo wanaume wengi huwa hawafanyi na kukazania tu kukaa muda mrefu kujua kuwa ndio wanawake wanachotaka.

Ujasiri si sawa na kutumia nguvu

Kuna wanaume wengi huwa hawajui tofauti ya ujasiri na kutumia nguvu, hivyo wasikiapo kuwa inabidi uwe na ujasiri wanadhani kuwa kuna kutumia nguvu, wanawake wengi wamekuwa wakikerwa na kuogopeshwa na mambo ambayo hufanyiwa na wanaume zao, kipindi ambacho wanaume wakufikiri kufanya hivyo ni kuwa na ujasiri. wanawake hutamani sana wanaume wangejirekebisha na kujua maana halisi ya kuwa na ujasiri.

Sio wanawake wote hupenda vitu sawa

Hapa inatokea wanaume wengi kukariri kuwa, sababu tu ex-wake alikuwa anapenda kufanyiwa vitu fulani, basi na huyu wa sasa atakuwa hivyo hivyo, hii inatokea kuwachanganya sana wanawake, na kukereka kwa baadhi ya mambo, huku mwanamke akiwa hana jinsi bali kuvumilia tu, na mwisho wa siku ndio unakuta, ananza kutafuta way-out ya kukukwepa.

Wanawake wanapenda ufuate anachokitaka

Iko wazi sana kuwa mara nyingi kujua kuwa mwanamke anahitaji nini, ni kitendawili kwa wanaume walio wengi, hivyo ni vizuri kuwa makini na kugndua ni kitu gani hapendi, hii hutokea cause mara nyingi si wanawake wote wanaweza kukwambia ni nini hasa kinawauzi, kuogopa kukuudhi, hivyo inawafanya wapate shida sana na kuweka maisha yao yawe magumu, ila hupenda sana kuwa makini na matendo yao ili kujua tofauti ya vitu ambavyo hawapendi na vile vinavyowapa furaha.

Ni zaidi ya mapenzi na sio ufundi

Ni kweli wanawake wengi hukubali kuwa kuna wanume wenye ufundi/uzoefu katika haya mambo, ila hiyo sio ishu zaidi, kinachotakiwa ni mapenzi, kuonyesha mapenzi na dalili zote za kumjali ndio jambo muhimu sana. Baadhi ya wanawake wamewahi kufunguka na kukiri kuwa tztizo la wanaume zao si kitandani, ila ni mapenzi kwa ujumla yanapungua.
Mikono.JPG

Dalili au tabia za mwanamke kicheche, mwanamke asiyemwaminifu

Anamarafiki wakiume kwa faida

Kwa mwanamke kuwa na marafiki wa kiume siyo ishu, ila ishu ni pale ukute mwanamke ana marafiki wa kiume, na kila rafiki yake huyo anajukumu lake katika maisha yake, kifaida zaidi na siyo tu rafiki wa story za hapa na pale, ila kila mtu anahudumia na wote unaambiwa ni marafiki tu, unaweza kusikia huyu wa kulipia saloon, mwingine wa vocha n.k, basi ujue huyo cheche.

Anakasirika haraka usipompa anachotaka.

Wanawake kama hawa wamezoea kupata kitu chochote watakacho kutoka kwa mwanamme, na ukibahatika kupendwa na mtu kama huyu ujue si bure, ameona kuna kitu utakachoweza kumsaidia, wengine utakuta wanapohitaji kitu wanazunguka na story nyingi ila mwisho wa siku kama mtu muelewa utajua tu anataka nini, tena hata kubembelezwa hashindwi, ila usimpe sasa anachohitaji, unaweza usiongeleshwe week nzima hadi pale utapokamilisha hitaji lake.

Siyo rahisi kupenda.

Wanawake vicheche huwa mara nyingi hawataki mambo ya mahusiano, wanataka siku zote wawe available ili kwa mtu yeyote mwenye uwezo zaidi ya aliyenaye akitokea, iwe rahisi kwake kujihusisha naye, na hata akiamua kupenda, huwa hakai sana, labda kama unamsaidia asilimia 90% ya matatizo yake.

Anachukulia mahusiano kama biashara.

Watu kama hawa huwa hawaingii katika mahusiano kwa sababu wamependa, siku zote wanakuwa na agenda ya siri nyuma yake, unaweza kuita faida, kiujumla kwa kitu chochote atakachokupa katika mahusiano, ujue hapo anatarajia faida yake, utakuta anakuchangamkia na kukufanyia vitu ambavyo hukutarajia, ila lengo lake mwisho wa siku utakuta anaishia kukuomba kitu Fulani kutoka kwako.

Anategeka kirahisi kwa vitu vidogo.

Kwa mwanamke kicheche, pale tu utapomchekea na kumpa zawadi, au hela kila akuombapo unamsaidia, ni rahisi sana kukubali chochote utakacho mwambia afanye, haijalishi kuwa unamalengo gani nae ya baadae au la, ilimradi tu unampa anachotaka.
Mikono.JPG

Jinsi ya kujua kama mwanamke anakupenda kweli ni kama ifuatavyo

Ni muhimu sana kwako mwanaume kujua kwa uhakika kuwa mwanamke anakupena kweli kweli,utajuaje kuwa mwanamke anakupenda? Zifuatazo ni ishara ambazo wewe kama mwanaume unapaswa uwe makini ili uweze kuziona na kuzifanyia kazi;

1. Mwanamke anayekupenda atakuwa tayar kujitoa muhanga kwa ajir yako yaan kujitoa kafara,vipo v2 ambavyo wa2 hawawez kuvifanya ila icpokuwa kwa wale wanaowapenda kwa moyo wote. Je ww ni sehemu mojawapo ya v2 vichache anavyovipa kipaumbele?,je ww unakuwa wa kwanza mbele ya rafiki zake?,je anakufanyia v2 ambavyo hawez kuwafanyia wanaume wengne?,je ameacha mambo mengine ili aweze kuwa na ww?,ni kwa v2 kama hivi unaweza kutambua ww ni wa muhimu kwake.

2. Mwanamke anayekupenda atahangaika juu yako,m2 anayekupenda atahangaika juu ya usalama wako,raha yako,heshima yako na maendeleo yako.Hii ni moja kati ya ishara kubwa kuwa mwanamke uliyemlenga anakupenda kwel.

3. Mwanamke anayekupenda atakuonea wivu mara kadhaa,ingawaje wivu mara nyngne unaweza kuvuruga penz endapo utazidi.Wivu ni ishara kuwa anakupenda ww na anataka akulinde usiibiwe au asije akakupoteza,anaogopa usije ukatoka katika maisha yake,au kwa maneno mengine usije ukamtoa moyoni mwako na nafas yake ikachukuliwa.

4. Mwanamke anayekupenda atakapokuwa mbele ya marafiki zake au watu wengine atacheka nao lakini atakugeuzia ww macho namaanisha uso wake haraka sana. Kufanya hivi ni kuonyesha kuwa anakuhesabia ww kuwa utaweza kumletea furaha katika maisha yake,zaidi ya hilo ni kwamba anatumaini kuwa utamuona kuwa yeye ni mtu aliye rahisi kufurahishwa kwa kuwa yeye ni mtu wa furaha.

5. Mwanamke anayekupenda ataendelea kukuangalia usoni kwa muda mrefu kuliko ilivyo kawaida ya wanawake wengine,mara nyingi atakuangalia na kutabasamu vizuri. Hii huenda ni ishara moja muhimu sana ya kukuambia kuwa " ANAKUHITAJI".

6. Mwanamke anayekupenda atajitahidi apendekeze kwa kuvaa vizuri pale anapojua kuwa atakutana na wewe,atajali sana juu ya nywele zako,nguo zake na hata anavyonukia,yaani atajipulizia pafyumu.

7. Mwanamke anayekupenda ataonyesha dalili za kupenda kuwa karibu yako katika mazungumzo au maeneo mengine,atapenda mara nyingi kuwepo katika maeneo unayopendelea na pia sauti yake itabadilika kuashiria hali ya kukupenda na kutaka kukuvuta kwa sauti yake.

Tafuta%20marafiki

Tabia za Msichana Anayekupenda Kimapenzi Lakini Hawezi Kusema

1. Atakutega kupata attention yako.

Hufanya mambo ambayo yatamfanya kuona kama unampenda au lah! Mf wa mambo hayo ni kujifanya anaumwa na kuangalia respond yako kwake ni kiasi gani unamjali na kiasi gani utahangaika kwa ajili yake au

2. Haoni aibu kugusa sehemu yako ya mwili.

Msichana anayependa haoni aibu kukushika mkono ama kukutomosa au hata kukumbatia. Kwa kufanya hivyo hujua kuwa kwa asilimia kubwa hisia za kushikana kwenu kutamrahisishia kazi ya kuwa na wewe

3. Kucheka kwa nguvu hata kwa kitu kisicho chekesha endapo wewe umezungumza.

Mara nyingi ataonesha uso wa furaha hata kama si furaha ya kweli

4. Wivu.

Hujisikia wivu anapokuona na wasichana wengine. Ukiwa unachart nao na ukiwaita majina ya kimahaba. Hapendi.

5 anakumbuka siku zako muhimu.

Hukumbuka kama vile siku yako ya kuzaliwa hatowez kuisahau kufanya ipite bila kukutakia heri ya siku ya kuzaliwa kama sivyo ukifaulu mtihani au chochote katika maisha yako atakuwa mbele kukupongeza

6. Eye contact anapenda kukuangalia machoni muda wote ambao mtakuwa mkizungumza pamoja akidhani kuwa utaelewa ni kiais gani anakupenda kupitia vile ambavyo anakuangalia.

Ila wengine huona aibu kuwatazama wavulana wanaowapenda si wote wana ujasiri wa kuwatazama wapenzi wao.

7. Hupenda kukaa mmuda mwingi na wewe.

Hawezi kupoteza hata sekunde ukimuhitaji kwa mazungumzo. Anajisikia furaha kukaa na wewe muda mrefu bila kuchoka. Anaweza akaacha kila kitu anachokifanya ili ajumuike na wewe.

8. Yupo tayari kuangamiza.

Kama msichana anakupenda yupo tayari kusacrifice. Ni kitu ambacho hakuna mtu ambaye anaweza akafanya kwa mtu mwingine. Utaona vipi huyo msichana alivyo kwako na wa wengine. Yaani yupo tayari yeye akose lakini wewe upate na kwa mwingine anaweza akamwamba hana alichoombwa lakini akakupa wewe kama pesa na vitu vingine.

9. Anachukulia matatizo yako kama ni yake.

Unapomueleza kuwa ana tatizo anajali tatizo lako kama vile ni lake na hujisikia vibaya sana na kuhuzunika na atafanya lolote ili aweze kukusaidia utoke katika hilo tatizo.

10. Mikwaruzano ikitokea katika urafiki wenu hayupo tayari kukupoteza kabla hajakuambia anakupenda.

Kwa kuwa anakupenda endapo ikatokea mikwaruzano basi atafanya juu chini kuyaweka mambo sawa ili asikukose
Mikono.JPG

Viashiria vingine vya mwanamke anayekupenda ni kama ifuatavyo,

Siyo kwamba ishara hizi zote anaweza kuwanazo msichana mmoja,ila kila mmoja kwa ishara zake

Hatua hizi zinaweza zikakusaidia kumgundua msichana anayekupenda,wasichana wanatofautiana ila wengi wao wana-share ishara tofauti.

1.Mnapoongea:

Sikiliza sauti yake,kama anaona aibu sauti yake itakuwa ya upole/laini.
anaweza akaanza kushika shika nywele zake au kuweka sawa mavazi yake.
Hawezi akakuangalia machoni atakuwa anakuangalia kwa kuibia.
Msichana anayekupenda anakuwa na tabasamu unapoongea naye kama amekuzoea,
ila kama hajakuzoea anapokuona gafla tabasamu hutoweka maana anakuwa na aibu.

2.Anapenda hugs na kukushika:

Unapotembea naye mahali anapenda kushika mkono wako,au unapokutana naye
anaweza kuhug.

3.Ajali za kijitakia

anaweza akaona kitu kidogo tu au mdudu halafu anakurukia,au anakukumbatia.
anaweza akatafuta sababu yoyote ilimradi tu akushike,atajitahidi usigundue
mbinu zake kwa kupotezea "Ooh i'm sorry i didn't mean it"

4.Anaibia kukuchunguza:

Unapokuwa umetulia zako unakuta anakuangalia kwa kuibia,ukigeuka anajifanya yuko busy na mambo
yake kumbe anakuchunguza taratibu

5.Wangalie marafiki zake.

Anapokuwa na marafiki zake akikuona anaweza akajitenga,hata kama mmeenda out pamoja na marafiki
zake utakuta yupo karibu na wewe,akiwa na marafiki zake halafu mkakutana gafla atakufuata halafu
waangalie marafiki zake utakuta kama wanateta,ukiona hali hiyo kuna siri yao yeye na marafiki zake
kuhusu wewe

6.Anapenda umjali.

Anapokuwa na tatizo au anajisikia vibaya lazima akuambie,mfano mmeenda mahali kukawa na baridi
hata kama si baridi sana atasema anahisi baridi ili mradi umsaidie koti lako,hata kama kuna watu
hawezi kuona aibu kuvaa badala yake atajisikia vizuri anapovaa koti lako.

7.Hawezi kuzuia tabasamu.

Unapomwonyeshea tabasamu lazima na yeye akuonyeshee,hata kama kuna kitu kimemwudhi
atakuonyeshea tabasamu ili mradi aonyeshe umemkuta katika hali ya furaha.

8.Ishara za mwili.

Anapopita mbele yako anaweza akafanya madoido mengi ambayo yatakuvutia ila kama anajiamini.
kama hajiamini anapokuona gafla anakosa amani,utamwona anashtuka gafla.

9.Anafurahishwa na vituko vyako.

Huwezi ukamboa,hata kama ukifanya kituko ambayo haichekeshi utakuta anafurahia.

10.Anakujali:

Anakuwa anakujali,mfano akiona umeumia labda umejigonga,yupo radhi akuhudumie.
unapokuwa naye anaweza kuuliza…"unahitaji chochote?….unaweza ukasema "nina kiu ngoja ninunue maji"
utamsikia "nina maji,kunywa haya yangu kwanza".basi ujue kwamba anakujali.

NB:Kama hujampenda unaweza ukajiepusha naye hatua za mwanzo ili msiende mbali na kuingia kwenye mahusiano ya kumwumiza hapo baadaye,Wengine wanaweza kufanyiwa hizo ishara zote na wasiweze kugundua,Cha msingi unatakiwa uwe na mda wa kumsoma mpaka pale atakapokuzoea kabisa na akaanza kushindwa kuficha hisia zake,siyo rahisi kwa wanawake wengi kumwambia mwanaume direct kuwa anampenda,baada ya kuona dalili zote unaweza kumtongoza na kumtamkia unampendautakuwa umemrahisishia kazi.

Tafuta%20marafiki

Dalili za binti anayeelekea kukubali ni kama zifuatazo:-

1) Ukiona anapenda kuandamana na wewe na anajisikia ufahari kuwa na wewe jua mtihani wa kwanza umepita. Ukiona anajishauri ujue labda anaona class yako ina mushkeli hivi chunga usimbwatukie kilichoko rohoni kwako ukaumbuka bureeeeeeeee……….

2) Ukiona anajishikashika maeneo ambayo yanautangaza uzuri wake kama usoni, nywele zake au hata kurekebisha nguo zake jua anajaribu kuwa mtanashati mbele yako ili akuvutie…………………. …….katika mazingira hayo dalili zote zipo kuwa kuna uwezekano mkubwa kampani yako anaihitaji maishani mwake……………………. .jipange usije ukaachwa kwenye mastima……

3) Ukiona haachi kukuuliza maswali binafsi na kutaka kufahamu unaishije ikiwa na pamoja na kufahamu hobbies zako au hata unapenda vyakula vipi ujue analichungulia jiko………..na anaona anafaa kukukaangia vinono………sasa mkifikishana huko ujue ni mwendo mdundo…………….

4) Ukiona anapenda kukuulizia khabari za ndugu zako na kutaka kuwafahamu basi ujue kesha anza maandalizi ya kujenga mahusiano nao kwani "knowledge is power."

5) Ukiona hupenda kukupasha habari zake binafsi na za ndugu zake wakiwemo marafiki zake basi ujue anakuaandaa kukamata mzigo na visaidizi vyake………….kazi kwako uko tayari kuubeba kama la basi chanja mbuga bado mapema……………khalakhal a lawama kukuta baadaye.



Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: