FUNDI CHEREHANI
Sehemu Ya 1
Mtunzi..... MoonBoy
Simu No. +255714419487 WhatsApp
Ilipoishia Jana →↓↓
JAMANI NDUGU WASOMAJI WA STORY ZANGU,.... STORY HII YA FUNDI CHEREHANI, NI STORY ILIYO TOKANA NA STORY ILIOPITA... IITWAYO SECONDARY SCHOOL NA NADHALI HILO CHOMBEZO WENGI MLILISOMA VIZURI NA PIA NATUMAINI MTAKUA MUMELIMALIZA MPAKA MWISHO.....
ILA KWA WEWE AMBAE HUKUISOMA SECONDARY SCHOOL, BASI NAKUAMBIA KUA HILI CHOMBEZO LA FUNDI CHEREHANI HUTOLIELEWA KABISA, MAANA MAUDHUI YOTE YALIOPO HUMU YAMETOKANA NA HIO STORY AU CHOMBEZO LA SECONDARY SCHOOL.... HIVYO KWA USHAURI WANGU KWAKO NINGEONBA UKAIANZE KUISOMA HIO KISHA UJE KUISOMA NA HII... MAANA NI SAWA NA KUANGALIA MUVI PART 2 WAKATI PART ONE HUJAIONA.....
UTANGULIZI WA CHOMBEZO AU STORY AU SIMULIZI AU HADITH... VYOVYOTE UTAKAVYOIITA LAKINI KITU NI KILE KILE
FUNDI CHEREHANI NI SIMULIZI INAYO MHUSU KIJANA MMOJA AMBAE ALIYACHEZEA MAISHA PINDI ALIPOKUA KWAO JIJINI ARUSHA, KIJANA HUYO ALIKUJA KUFIRISIJA BAADA YA KUHONGA MALI ZOTE KWA MWANAMKE... NA KUFIKIA HALI YA KUANZA MAISHA MAPYA KIJIJINI KWAO HUKO TANGA AMBAPO NI ZAO LA MAMA YAKE.... KIJANA HUYO ALILAZIMIKA KUA FUNDI CHEREHANI KWAKUA ALIPOFIKA KIJIJINI KWAO HUKO ALIONA KAZI ITAKAYO MFAA NI HIO KULIKO KULIMA,
NA KAMA UNAVYOJUA WAMAMA WA TANGA WALIVYO NA MAKUSUDI, KIJANA HUYO ATAPATA TABU SANA KATIKA KAZI YAKE, NA KIJANA HUYO KWA SASA ANAYAOGOPA SANA MAPENZI KWAKUA NDIO YAMEMSHUSHA KIUCHUMI KATIKA SIMULIZI ILIOPITA NADHANI MLIONA KIJANA HUYO ALIVYOFILISIWA MALI ZAKE KIUJANJA UJANJA NA MWANAMKE AMBAE ALIKUA NI MWALIMU WAKE KATIKA SHULE ALIOKUA AKIISOMA....... JE KUFILISIWA HUKO KUTAMFANYA AJIZUIE KUKUTANA NA WANAWAKE TENA?? MIMI SINA JIBU ILA JIBU LIPO HAPA
SASA TUIANZE STORY YETU RASMI KABISA......
HIIIII NI SEHEMU YA MWISHO YA STORY ILIOPITA, SASA HAPA NI MAHALI ILIPOISHIA........ TWENDE KAZI
Dokta alirudi katika chumba ambacho mimi nipo, lakini ghafla nilijihisi kuchomwa sindano, kisha nikafunikwa shuka mpaka usoni,.... Huku dokta akisema
"mungu akulaze mahali pema peponi"
Dokta alitoka taaratibu nje huku akionekana kujifuta futa machozi kwa kuashiria uchungu juu yake,.... Maafande pamoja na mama angu walimkimbilia dokta na kumuuliza...... Lakini dokta alimuita mama
"mama nakuomba ofisini kidogo"
Kabla mama hajaenda, mara afande mmoja akasema kua,
"dokta, huyo dogo ni muarifu, hivyo tunapaswa nasi kujua hali yake ili usalama uwepo juu yake hapa hospitalini"
"ok sawa njoeni kwa wote ofisini kwangu"
Waliingia wote, mama na wale askari katika ofisi ya dokta........ .
"mama, nafikiri kua yule kijana ni mtoto wako"
"ndio baba ni mtoto wangu"
"aaaaaaa kiukweli kijana yule alipoteza damu nyingi sana, na kwa bahati nzuri aina ya damu yake ilikuepo, lakini kwa bahati mbaya, duuuuuuuu pia tunapaswa kumshukuru mungu.... Kwa kila atendalo juu yake... Kifupi ni kwamba kijana wetu amepoteza maisha"
Niliskia kishindo cha kuanguka mtu, na si mwingine bali alikua ni mama angu ndio alidondoka na kukata moto..... Nae akawa mgonjwa papo hapo na kupelekwa katika wodi za wagonjwa wa kawaida...... Kwa upande wa maaskari walikuja kuniona na kunifunua,..... Walikuta tayari nilishawekewa pamba katika tundu zangu za pua na masikio...... Askari walitoka huku kila mmoja akisikitika kwa staili yake,
Kwa upande wa mama yangu kule alizinduka maana alipata mshtuko wa ghafla.... Sasa baada ya kuzinduka alianza kuwatupia lawama wale askari, huku mama yangu akilia kwa kugala gala hapo hospitalini
"mama, hupaswi kutulaumu sisi, kwani nasi tuliagizwa na wakuu wetu tuje tumkamate mwanao, na katika ajali nadhani tuliona wote kua ni piki piki ndio ilimgonga mwanao"
"hapana, kama sio nyie mwanangu leo ningekua naeeee"
"mama, nasi pia tunaumia juu ya mwanao kupoteza maisha, kwani nae ni binadamu kama sisi"
Mama yangu alikua akilia sana mpaka askari wakajua anaendea kua chizi,
Muda si mrefu manesi walikuja kunichukua na kunipeleka mochwali kuniweka katika jokofu, ili nisiharibike..... Huku familia ikinifanyie mipango ya kunisafirisha kwa ajili ya maziko katika mkoa wa tanga mahali walipozaliwa. Wazazi wangu......
Nilisikia sauti ya mama ikimuambia dokta kua
"usimueke huko mi nataka nikae nae hapa hapa"
"mama, huyu kijana aliumia sana hivyo akiwekwa mahali penye joto ataharibika"
"sitakiiiiiiiiiiii nimtaka mwanangu uuuuuuwiiiiiiiiiii sadiki baba umeniacha mwanangu. . Uuuuuuwiiiiiiiiiii"
HAPA SASA NDIO TUNAIANZA RASMI FUNDI CHEREHANI SEHEMU YA 1
wale askari baada ya kusikia mama analia waliingia kule mochwali ambako ndipo mama yangu alipokua akilia, walikuja na kumbembeleza huku wakimpa pole nyingi na nyingi pamoja na kumuomba msamaha,
"mama pole sana mama angu, tumuachie mungu ndio muweza wa yote mama etu ee"
"mumemfungulia mwanangu kesi zenu za kishenzi kwanini lakini, kwani kamtia mimba huyo msichana wenu... Niachieni pumbavu nyie"
"mama, kesi ya mwanao tumeshaifuta, maana yeye ndio mtuhumiwa, sasa amefariki tutampeleka nani mama angu"
"mchukueni mkamzike sasa si ndio mlivyotaka, na ninawasusia hii maiti pumbavu nyie"
"ah ah mama unifanye hivyo, utatukua umetuachia laana kubwa mama etu"
"tokeni hapa na staki kuwaona, wana haramu nyie"
Sawa mama.... Oyaa afande twenzetu"
Kuliskika muondoko wa gari aina ya difenda, huko nje.... Huku mama yangu akiendelea kulia kwa uchungu.... Dokta alimfuata mama yangu na kumpa pole
"pole sana mama angu ila tusimlaumu mwenyezi mungu kwa kile alichokifanya"
Mama alipoambiwa hivyo niliisikia sauti kwa mbaali ikimuambia dokta kua
"heeee hebu kelele na wewe, au unataka mwanangu afe kweli"
"ok samaani mama... Ila inabidi tumuamishe kwenye hii wodi"
"sawa muamishe ila hakikisha mtu yeyote asijue dokta"
"sawa kwa hilo ondoa shaka na mwanao atakua mzima wa afya... Ila kwanza tuelewane mama"
"tuelewane mara ngapi doktaa eee.... Si tumekubaliana nikupe milioni moja"
"hapana mama hii ishu ni ngumu sana mama, tena ukizingatia tunaifichia serikali makosa, huoni ni hatari hii"
"ok sawa, basi nitakupa milioni moja na nusu"
"mama, ongeza nusu mama ziwe hata mbili"
"dokta, unataka tushindwane"
"mama hatuezi kushindwana ila ukinipa milioni mbili nitampeleka nyumbani kwangu na nitampa matibabu yote mpaka atapona mwanao"
"heee umpeleke kwako? Kwani huko kwako hakuna watu watakaijui hio ishu"
"hapana, maana watoto wangu wapo shule boding, na mke wangu yupo bize sana na kazi zake, na pia nina mfanyakazi"
"hapana huko hakutokua na usalama kabisa"
"mama, huko usalama upo, kwani nina vyumba vya siri na vipo kwa ajili ya binadamu na vina kila kitu... Na pia nina rumu moja nimeifanya wodi, hivyo hakuna shida, na hata hivyo ni nani atajua kua mwanao ana kesi ya kumpeleka jela"
"ok hapo basi nakubali, ila atahudumiwa na nani wakati ukiwa huku hospitali"
"nina nesi wa kike ambae namuamini sana"
"dokta dokta dokta, angalia mwanangu asirudi kwenye mikono ya serikali.... Maana akionekana kua yupo hai basi lazima kesi ianze upya, tena wewe na mimi lazima tuhusishwe, kwahio kua makini sana dokta"
"usijali mama angu, tena utamkuta mwanao ana afya nzuri kabisa"
"ok... Vp umeshamtoa zile pamba za maskioni"
"oooohhh shit nilijisahau mama angu sorry"
"hebu mtoe haraka, tena naomba tumhamishe sasa hivi"
"ok ngoja nikasogeze gari yangu"
"ok fanya hivyo dokta"
Dokta alienda kusogeza gari yake ili nipakiwe nipelekwe huko nyumbani kwa dokta, kweli walifanya hivyo hivyo kisha dokta alienda ofisini kwake na kutoka na box liliojaa dawa za kila aina...... Nilipakizwa kisiri siri sana utafikiri wanapakiza dawa za kulevya.... Mtoto wa kiume nilikua sijitambui hata kidogo maana nilikua nimeumia sana maeneo ya kichwa na kwenye mgongo, yaani shuka lenyewe lilikua limeloa damu,
Baada ya robo saa hivi, nilihisi kama tumefika maana nilikua nashushwa kutoka kwenye gari,
Waliniingiza ndani na cha kwanza ni kufanyiwa usafi maana nilikua nimeloa damu na vidonda kila mahari hivyo nilianza kufutwa damu kisha nikaogeshwa vizuri kabisa... Baada ya kuniogesha sasa kuanzia hapo nikaanza kuwekewa madripu ya damu na maji
"Dokta mbona mwanangu hata hakushtuka au kafa kweli nini Dokta?"
"mama ondoa shaka mwanao yupo hai, sema kuna sindano ya usingizi nilimpiga ili asije akastuka mbele ya wale askari, na dawa hio ya usingizi itamchukua siku mbili nzima, ndio ashtuke"
"heeeeee doktaa hapana bwana siku mbili? Hapana"
"ok basi ngoja nimchome sindano itakayopunguza makali ya hio dawa, ila kuamka kwake ni masaa mawili, ila hata akiamka haitaji usumbufu wowote ule"
"sawa"
"kwahio sasa kama utakua ukija kila siku sawa ila kama utakuja mpaka akipona pia sawa"
"weeeeeeeeee doktaa nije mpaka akipona kweli nitakua nina akili kweli? Nakuja kila siku tena nashinda nae mchana kutwa mpaka apone"
"ok sawa unakaribishwa"
"ok sawa...... Sasa dokta mi naona nikuache kwa leo maana kule nyumbani kuna wasichana tu na wanaogopa sana kwakweli"
"mama we usijali, yaani huyu namtibu kama mwanangu niliomzaa, yaani chakula atakula atakacho"
"sawa, namuombea mwanangu apone"
"mimi pia napenda apone"
Basi nilisikia tu milango ikifungwa fungwa kuashiria mama angu ndio alikua akiondoka huku dokta akimsindikiza, na hapo kitandani nilibaki mimi na mtu mwingine ila sikumtambua kwakua nilikua nasikia tu, kwani hata mapigo yangu ya moyo yalikua ni madogo sana...... Na ukumbuke kua sikio la kufa halisikii dawa.... Yani Hata mtu aliekufa anasikia yote hata umtukane kasikia lakini kukujibu au kujitikisa ni ngumu, hivyo kwa upande wa mimi nilikua ni mzima ila nina asilimia chache sana za kupona, kwani ilibaki tu kidogo nipumulie mipira.......
Sasa baada ya muda dokta alirudi na kunitundikia drip lingine la damu, huku akimuachia maagizo yule nesi ambae yeye anamuamini sana katika kazi zake za siri kama hizi,
"fatu, hii ni kazi kama zile kazi zingine, huyu mtoto hatakiwi mtu yeyote kujua, na huyu mtoto ana dau kubwa kutoka kwa mama yake kuliko wagonjwa wote tulio wapa huduma za siri, kwahio kua makini na huyu mtu.... Na pia hutakiwi kukaa nje au kwenda sebureni kuangalia tv, unatakiwa ukae hapa hapa na mgonjwa, ili hata anapojigeuza uwe unamuona... Afu kama kawaida ya kuongeza damu ikifikia hapa milimita 2 unalitoa dripu na kumuekea lingine ambalo litakua la mwisho na kwa upande wa maji, madripu haya mawili yatamtosha, sawa fatu"
"sawa dokta"
"na pia kuusu chakula huyu mfanyakazi atawapikia na ataleta huku huku, ila hakikisha mgonjwa anakula ili dawa zisimzidi sawa"
"sawa dokta"
Baada ya dokta kumuachia maagizo yote nesi wake, aliondoka na kwenda kuimalizia siku yake hospitalini kunako wagonjwa wengi kuliko mimi.....
Sasa kumbe nesi nilioachiwa ni mcharuko mtupu japo sikua nikimuona, kwa macho ila kwa maskio namsikia kwa mbali
"haaa siamini kama mahensam pia mnaumiaga, yaani mtoto una sura nzuri kama mwanamke,.... Natamani nilijue jina lako, maana kwa uhensam uliokua nao, hapa siondoki bure, yaani nakuombea upone haraka, maana nimekupenda bure tu"
Mimi niliisikia tu sauti akijisemea mwenyewe, lakini sikua na fahamu ya kumjibu wala kumuona mwanamke huyo ambae ndio nesi alie achiwa majukumu yote kuusiana na mimi....
Je? Nini kitaendelea? Usikose sehemu ijayo kujua mpango mzima wa nesi huyu
Itaendelea..... after Tomorrow
Ludewa yetu na maendeleo yetu posted by barnabas njenjema, kutoka Ludewa
0 comments:
Post a Comment